TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 28 Julai 2017

BRANDINA LUKINDO:- MIMI NI MTANGAZAJI NISIEYUMBISHWA NA WADAU, NAWAHESHIMU LAKINI...........

Na pambe za taarab.

        Unapofika mkoani tanga hususani katika redio ya TK fm "tanga kunani" ni lazima uvutiwe na sauti tamu toka kwa mtangazaji mahiri aitwae Brandina lukindo ambae pamoja na kuendesha vipindi vingine lakini pia ndie mtangazaji pekee wa kipindi cha taarab katika redio hiyo maarufu mkoani tanga.

  Brandina aliwekwa kiti moto na wadau, watangazaji wenzie wasanii na viongozi kwenye kipengele cha mjue mtangazaji wako ambacho kinapatikana kwenye group la whatsap la pambe za taarab kila siku ya alhamisi kuanzia saa moja usiku, miongoni mwa maswali ambayo aliulizwa jana ni kwamba anakabiliana vipi na kashda za wadau katika kumlazimisha mtangazaji kucheza wimbo na pia zile rabsha za ugombanishi ambazo zimeota mizizi kuchonganishwa kati ya mtangazaji na mtangazaji mwenzie lakini chanzo kikubwa kinakuwa ni wadau?.

Akijibu Brandina alisema ni kweli hizo zipo sana lakini kwangu nachukulia ni changamoto tu maana nimewazoea tokea nilipokuwa mwambao fm, unajua kama mtangazaji hujitambui basi wadau watakuyumbisha sana maana mdau huwa hakai redio moja muda huu utamsikia hapa baadae utamsikia kule yaani ni watu wa kuhamahama! sasa mara nyingi walio wengi huwa wanabeba mambo yasiyo ya kweli na kumpelekea mtangazaji mwenzio wa redio ingine akisema Brandina anakusema, mara Brandina amekuwekea nyimbo za mafumbo! vitu kama hivyo! sasa kama haupo makini utagombana na wenzio kila wakati.

Mimi huwa siwapi nafasi watu wa hivyo kabisa! ninachoangalia nini bosi wangu anataka nifanye, kamwe mdau hawezi kunipangia play list wala kunigombanisha na yeyote maana najitambua na nipo strong sana tu! nawaheshimu sababu ni wasikilizaji wangu wazuri lakini inapofikia kunifundisha kazi hapo sitokuwa tayari kabisa kabisa, huyo ndie Brandina lukindo mtangazaji mrembo ambae anapatikana ndani ya TK fm tanga! je wiki ijayo tutakuwa na mtangazaji gani kwenye segment yetu hii mpya? tuendelee kuwa pamoja...Ahsanteni sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni