TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 27 Julai 2017

ILE SEGMENT YA MJUE MTANGAZAJI WAKO WA TAARAB INARUDI HEWANI LEO.

Na pambe za taarab.

Katika kile kinachoonekana kuiboresha zaidi blog hii bora ya pambe za taarab, leo hii ile segment pendwa ya "mjue mtangazaji wako" inarudi rasmi kupitia group la whatsap la wadau, watangazaji viongozi na wasanii wa taarab.

Segment hii hapo kabla ilikuwa ikirushwa na mtandao wa ubuyu wa taarab ambayo kwa sasa imebadilishwa jina na kuitwa pambe za taarab, kwenye segment hii mtangazaji husika anatakiwa ajieleze historia yote ya maisha yake then baadae wanachama wa group hilo la whatsap wanapata nafasi ya kuuliza maswali ya papo kwa papo kwa mtangazaji huyo nae kujibu.

Itakapofika saa moja kamili ya usiku leo ndipo rasmi itakuwa inaanza ile segment yetu pendwa ya mjue mtangazaji wako na kwa kuanza mgeni wetu leo atakuwa ni Brandina lukindo mtangazaji toka TK fm redio iliyopo mkoani tanga!. Hii ndio pambe za taarab...Ahsanteni sana!.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni