TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 25 Julai 2017

FATMA JUMBE:- TAARAB INAKUFA NA UTAMU WAKE.....

Na pambe za taarab.

Mdau mkubwa wa taarab aishie visiwani zanzibar maeneo ya Mpendae Bi fatma jumbe leo amepiga simu katika ofisi zetu na kutoa maoni yake juu ya muelekeo wa muziki wa taarab kwa sasa.

Akizungumza kwa uchungu Bi fatma alisema inasikitisha sana kuona taarab inapotea na kila siku wadau tumekuwa tukilalamika lakini hawa viongozi wa muziki huu wanakuwa kama ni watu walioweka vibanzi machoni, wapo kimya sana na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa katika kuunusuru muziki huu.

Kwa sasa mtu akija huko bara akaamua aende taarab labda jahazi au bendi yoyote utakutana na madudu mpaka utajilaumu kwanini ulienda, kwanza hakuna wapenzi, msisimko umepotea ukija katika uimbaji wenyewe ndio utachoka kabisaa! Ndio pale nikasema taarab inakufa na utamu wake!.

   Malalamiko haya ya wadau yamekuwa kama wimbo wa taifa kwa sasa!, hivyo mtandao huu unawaahidi utafanya mahojiano na kiongozi mmoja wapo mwandamizi wa muziki huu wa taarab ili aweze kuzungumzia tatizo hili kwanini wapo kimya?.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni