TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 25 Julai 2017

HASSAN ALLY:- USHOGA NI TABIA YA MTU WALA HAIHUSIANI NA TAARAB.

Na pambe za taarab.

Ile segment bab-kubwa iendayo kwa jina la "sindano za motto" ndani ya group la wadau wa taarab whatsap liitwalo pambe za taarab jana ilianza rasmi na mgeni alikuwa ni young hassan ally muimbaji toka ogopa kopa classic bendi.

   Katika maswali ambayo aliulizwa na kujibu lilikuwepo hili " inasemekana waimbaji wengi wa taarab wakiume wana tabia za ushoga je hili limekaaje kwa upande wako?" Hassan ally au mzee wa ngenga anavyojulikana kwa sasa alianza kwa kucheka kisha akajibu kama ifuatavyo:- unajua hao wanaohusisha taarab na ushoga wanakosea sana mbona mashoga wapo katika bongo fleva, dansi, bongo movies mpaka viongozi wakuu wapo pia mashoga.

Ushoga ni tabia ya mtu ila ushoga haupo katika taarab tu, unajua sometimes ushoga unaweza kusababishwa na mtu alivyozaliwa na hommon nyingi za kike au wakati mwingine ni tamaa za maisha mazuri hupelekea mtu kuharibika, nawachukia sana wale wanaohusisha ushoga na huu muziki wetu kiukweli hawatutendei haki na nawaasa waache mara moja wasipende kumzushia mtu kitu wasichokifahamu, maana sasa hivi mtu ukijipenda tu kwa kuvaa vizuri wanakwambia muangalie yule shoga kitu ambacho sio kweli alilalama Hassan ally.

  Mtandao huu unampongeza Hassan ally kwa kushiriki vyema katika sindano za motto na tunamtakia mafanikio katika vipindi vyake vya ngenga ambavyo amekuwa akifanya redioni na katika televisheni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni