TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 23 Julai 2017

KHADIJA YUSUPH AKATAA KUMZUNGUMZIA LEYLA RASHID MBELE YA KADAMNASI.

Na pambe za taarab.

Khadija yusuph muimbaji wa wakaliwao modern taradance leo hii amekataa kabisa kumzungumzia wifi yake Leyla rashid mbele ya kadamnasi.

   Hayo aliyasema wakati akifanya mahojiano na Gea habibu ndani ya clouds fm, kipindi kwa raha zetu. Unajua kitendo cha kuzungumza issue ya Leyla na mimi kila wakati huleta hisia kwamba ugomvi ndio umeanza upya na kuamsha matusi toka kwa wadau na wapenzi sasa nasema sitaki maswali kama hayo maana maswali yapo mengi tu, kwanini tusizungumzie ujio wangu mpya nje ya wakaliwao!.

    Kwa sasa nandaa album yangu binafsi chini ya meneja wangu dokta albino wapenzi wangu waisubiri kwani itakuwa pambe sana tu. Alipoulizwa kama amehama wakaliwao alikataa na kusema bado  ila hiyo ni kazi yake binafsi.

     Khadija yusuph amekuwa katika wakati mgumu tokea sana tokea ilivyosemekana amekataa mkono wa wifi yake msibani, lakini yeye amesema hakuwa ameuona mkono wa wifi yake. Mtandao wa pambe za taarab unamuomba khadija yusuph kumaliza tofauti zao na wifi yake Leyla Rashidi ili maisha yaendelee.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni