TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 23 Julai 2017

ALLY STAR:- TAARAB YA SASA INAYUMBA, IMEPOTEZA MVUTO NA MSISIMKO.

Na pambe za taarab

      Mwanamuziki mkongwe katika miondoko hii ya taarab nchini ally star ameuambia mtandao wa pambe za taarab kuwa kwa sasa muziki huu wa taarab umekosa mvuto na hata ule msisimko wa kiushindani umepotea kabisa.

ALLY STAR
   Akiendelea kuzungumza Ally star alisema kuwa enzi zetu sisi tulikuwa tukiumiza vichwa haswa kuanzia katika utunzi mpaka kwenye kutengeneza muziki wenyewe na ndio maana taarab ya zamani itaendelea kufanya vizuri daima, inashanga kuona nyimbo za sasa hivi hazidumu katika media kabisa, angalia wimbo wangu natanga na njia ni wa kitambo sana lakini mpaka sasa ukienda katika kumbi mbalimbali bado unapigwa na watu wanacheza, wakati umefika kwa wahusika wa muziki huu kubadilika alimaliza kwa kusema.

      Ally star kwa sasa ni mwanamuziki wa bendi ya TOT taarab ambayo inamilkiwa na chama cha mapinduzi CCM, sisi kama mtandao wa pambe za taarab tunawaomba wahusika kufanyia kazi yale yote yaliyo zungumzwa na mkongwe huyu wa taarab nchini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni