TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 22 Julai 2017

KHADIJA MBEGU KAIS WA JAHAZI MODERN TAARAB AFUNGUKA YA MOYONI.

Na pambe za taarab.

Muimbaji chipukizi anaekuja kwa kasi katika tasnia ya taarab nchini khadija mbegu kais ambae kwa sasa yupo jahazi modern taarab amefunguka ya moyoni.

   Khadija ambae wapenzi wa jahazi wamempachika jina la "mcharuko Chipolopolo" kwa kuzimudu ipasavyo nyimbo za fatma mcharuko amesema kwamba kwa sasa ana furaha kubwa kwa kufanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaoaminika na viongozi wa jahazi kutokana na uwezo wake wa kuimba alionao.

    Mwanzoni nilipokuwa najiunga na bendi hii kutokea kolombwe nilikuwa na hofu kubwa kulingana na ubora wa bendi hii lakini kadri siku zinavyokwenda najengeka imani ya kujiamini zaidi ndio maana nafanya vizuri kwa sasa. Lengo langu bado halijatimia nataka kuwa zaidi hivi nilivyo sasa na naamini nitafanikiwa sababu kipaji ninacho na juhudi katika kazi ndio msingi wa maisha yangu.

    Nawashukuru sana viongozi wangu Hamisi boha, Awadh na Prince Amigo kwa kuniamini na kunikosoa pale ninapoteleza kwani kama ujuavyo ndugu mwandishi mimi sio malaika kwahiyo kukosea kupo sana tu alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni