TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 17 Julai 2017

ALLY J:- FIVE STAR'S BADO IPO NA ITAENDELEA KUWEPO INGAWA............

Na pambe za taarab.

     Mpiga kinanda nguli katika tasnia hii ya taarab nchini Ally J alisema kuwa bendi ya five stars haijafa kama wanavyo vumisha watu, isipokuwa yeye ndio amekwenda jahazi na vijana wake wanaendelea kupiga kazi kama kawaida.

     Unajua ndugu mwandishi, watu wamekuwa wakisema mengi sana zaidi ya sana ila yawapasa kukubali kuwa mimi Ally J ni mtu tofauti na wanavyonidhani, kamwe siwezi kuacha au kuuwa kitu changu kwa ajili ya kitu cha mtu! hapa jahazi mimi nafanya kazi tu ila mali yangu haswa ni Five stars. Vijana waliobaki kwenye bendi yangu hawana majina makubwa ndio sababu mnaona kimya.

    Tumekuwa tukipiga show sana sana katika maharusi mbalimbali hapa jijini na vijana wanajifua ili kuleta ushindani zaidi kwa baadae alisema ally j. Aliyasema haya wakati wa mahojiano ndani ya group la whatsap lililosheheni baadhi ya watangazaji wa taarab nchini siku ya jana jumatatu usiku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni