TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 17 Julai 2017

HASHIM SAID:- SIKIHITAJI CHEO CHA UFALME, MUNGU PEKEE NDIO MWENYE HADHI HIYO.

Na pambe za taarab.

Muimbaji wa mashauzi classic Hashim said "igwee" ameibuka na kukataa kabisa kuitwa mfalme katika muziki wa taarab na kudai ni mungu pekee ndio mwenye hadhi hiyo.

     Aliyasema haya baada ya kuulizwa swali inakuwaje wadau wanamhusisha yeye na baadhi ya wasanii wakiume kupigana vikumbo kugombea jina la mfalme ambalo limeachwa na mzee yusuph alieacha kuimba taarab na kumrejea mungu kwa ibada mbalimbali.

    Unajua ndugu mwandishi, niliwahi kuona katika mtandao mmoja wakinihusisha mimi na baadhi ya waimbaji wenzangu wa taarab toka bendi tofauti kuwa tunagombea jina hilo la mfalme na kuhoji ni nani anafaa kuwa na cheo hicho?, labda mimi nifunguke kuwa sihitaji cheo cha ufalme na nisihusishwe katika mjadala wowote unaohusu jambo hilo...sitaki...alisisitiza Hashim.

    Sifa ya ufalme ipo kwa mungu pekee iweje leo mja kama mimi nijipachike cheo hicho?, kwa upande wangu siwezi na sitaki kabisa kabisa alimaliza kwa kusema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni