TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 13 Julai 2017

THABIT ABDUL AAHIDI KUTOTAJA MDAU YEYOTE KATIKA NYIMBO ZAKE MPYA ZINAZOKUJA KUANZIA SASA!.

Na pambe za taarab.

      Mkurugenzi wa wakaliwao modern taradance Thabit abdul ameahidi mbele ya wadau kutotaja tena majina ya wadau katika nyimbo zake mpya zinazofuata.

      Aliyasema hayo wakati mjadala ukiendelea ndani ya group la pambe za taarab whatsap, mada ya leo ilikuwa ikihoji ni nini faida wazipatazo bendi za taarab kwa kutaja majina ya wadau kwenye nyimbo zao?, Thabit alisema kuwa hakuna faida yoyote ingawa nae hapo kabla alikuwa ni mfuasi wa mfumo huo lakini kwa sasa amejifunza kitu na kamwe hatoruhusu muimbaji wake yeyote ataje majina katika nyimbo zake mpya zinazokuja.

    Zamani wadau walikuwa wakitudanganya kwamba unapomtaja basi ndio atachagua sana nyimbo hiyo redioni, lakini kwa sasa nimegundua ubora wa nyimbo ndio unaomfanya mtangazaji na msikilizaji kwa pamoja kuchagua na kuicheza. Mimi sitaki tena kutajataja mdau yeyote atakaetaka ataichagua nyimbo yangu na asietaka basi aiache lakini naamini nyimbo ninazoziandaa mimi zote ni nzuri na zinapendwa.

     Wadau na wanachama wa group hili la pambe za taarab walimshukuru Thabit abdul kwa kuonyesha ushirikiano wa khali ya juu na kumtakia mafanikio yeye sambamba na bendi yake ya wakaliwao modern taradance.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni