TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 13 Julai 2017

WADAU NA MASHABIKI WA GROUP LA PAMBE ZA TAARAB WHATSAP WALALAMA KUTAJWATAJWA MAJINA KATIKA NYIMBO ZA TAARAB.

Na pambe za taarab.

Wanachama wa group jipya la pambe za taarab whatsap wamelalama kukerwa na tabia za waimbaji kadhaa wa taarab nchini kujaza majina katika nyimbo zao hali inayopelekea kukosekana radha halisi ya taarab kama ilivyokuwa zamani.

     Wadau hao waliyasema hayo kupitia mada mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na admin kais mussa kais kila siku ndani ya group hilo. Fatma jumbe alisikika akisema kuwa inakera sana kwa sasa kusikiliza muziki wa taarab kulingana na majina wanayoyataja, nae Hija alishauri aitwe kundini malkia wa mipasho ndani ya group ili aweze kuulizwa maswali "live" na wadau hao juu ya jambo hilo.

     Kwa upande wake Da shija alisema tabia hiyo inamkera sana mpaka inampelekea kufunga redio kila inapofikia sehemu ambapo majina yanatajwa. Admin wa group hilo kais mussa kais ameahidi kumtafuta malkia wa mipasho nchini na kumjumuisha kundini kwa muda ili aweze kujibu maswali ya wadau hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni