TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 10 Novemba 2017

NYAWANA FUNDIKILA, NI MIAKA MINNE SASA UMETANGULIA MBELE YA HAKI.

Na kais mussa kais.

Waswahili wanasema msiba uusikie kwa mwenzio!, pale inapofikia kipindi mwenza wako ambae mlikuwa mkishauliana, mkila pamoja, mkijifunika shuka moja, mkikoga pamoja, mkicheza na kutaniana matani ya hapa na pale anapoiaga dunia tena kwa kifo cha ghafla kwa kuumwa siku mbili tu! machungu yake yanakuwa hayasemeki kiukweli.

Nyawana umezimika kama mshumaa pembezoni mwa upepo wa bahari huku ukiwa bado unahitajika sana na jamii inayokuzunguka nikiwemo mimi mumeo!, ni mengi tuliyazungumza na kuyapanga yakiwemo ya kimaisha na mengineyo lakini hayakutimia mwenyezimungu aliamua kukuchukua na kutangulia mbele ya haki, sina nitakalo lisema zaidi ya kukuombea dua na kumuomba Allah akupe kivuli miongoni mwa vivuli vya peponi inshallah.

Tarehe kama ya leo mida ya saa saba mchana ukiwa kitandani kwetu uliniaga dunia na kuniachia usia ambao sitokaa nikusahau, nakumbuka uliniambia "kais mume wangu, mimi nakufa lakini nakufa nikiwa nakupenda sana! roho yangu inauma kwakuwa najua utapata shida sana kwakuwa mapenzi yetu ni ya dhati na hakuna ambae anapenda kuwa mbali na mwenzie" kauli hii inaendelea kujirudia masikioni mwangu kila wakati...mungu akurehemu na akusamehe madhambi yako kwani naamini ipo siku tutaja onana tena.

Kikubwa napenda ujue kwamba Nakukumbuka sana, nakufanyia sana visomo vya dua ili Allah akufanyie wepesi katika mitihani yako, siku zote kazi ya mungu haina makosa, lala salama Nyawana, mashabiki, wapenzi, wadau viongozi mbalimbali wa taarab, watoto wako, ndugu jamaa na marafiki pamoja nami mumeo tumekuwa mstari wa mbele kukukumbuka na kufanya dua kwa ajili yako, hii yote ni kuonyesha mapenzi ya dhati tuliyonayo kwako...mwisho kabisa nasema upumzike kwa amani nyawana isale fundikila kwani siku na wakati wowote nasi pia tutakufa kwani kila kilichozaliwa na kupewa pumzi basi siku ikifika kitakufa. Mwenyezimungu akurehemu inshallah.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni