TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 21 Novemba 2017

SAADA NASSOR AMTABILIA MAFANIKIO MAKUBWA KHADIJA MBEGU!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji bora tanzania visiwani ambae mpaka sasa anaendelea kushikilia zile tuzo tatu za ubora wa uimbaji wa muziki huu wa taarab Saada nassor amemsifia na kumpongeza muimbaji chipukizi khadija mbegu kwa uimbaji wake baada ya kukutana nae katika show ya bendi ya gusagusa ijumaa na jumamosi pale Hugo house kinondoni jijini dar.

Unajua nilipomuona msichana huyu akiimba pale katika steji ya gusagusa nilivutiwa nae sana maana ananikumbusha mimi nilipokuwa naanza kuimba nilikuwa kama yeye...nilikuwa ni mwenye kipaji kikubwa kama yeye, nilikuwa na mwili mdogo kama wake, kiukweli anaimba vizuri sana! ana kipaji kikubwa sana ambacho kinatakiwa kuendelezwa na viongozi wake na pia juhudi zake binafsi zinahitajika.  Atakutana na vikwazo vingi sana, atavunjwa moyo, atakatishwa tamaa, atanyanyasika lakini ajue hayo yote yatamkuta kwakuwa hao wabaya wake wamegundua kuwa ana kipaji na muda wowote anaweza kuwazidi.

Mimi nimepitia katika mazingira magumu sana mpaka leo hii watu wananifahamu na napata mialiko kadhaa wa kadhaa nje ya nchi na pia nina kazi yangu serikalini nimeajiliwa lakini nilisimama imara na kumuomba mungu na kweli leo nakula kivulini. Unajua zamani zanzibar mimi sikuwa lolote mbele ya Latipha salum muimbaji mwenzangu lakini hilo halikunikatisha tamaa niliendelea kupambana na kuonyesha umahiri wangu kwenye kuimba sikukata tamaa na mwisho wa siku leo hii namshukuru mungu nimefika hapa nilipo, sasa khadija mbegu namuasa kwanza awe mvumilivu na aongeze juhudi asiridhike na kiwango alichonacho cha uimbaji wake ajifunze zaidi na zaidi, mimi namkaribisha unguja akipata nafasi anaweza kuja maana kule ni kama chuo kwa uimbaji wake akikaa miezi michache na kurudi huku bara watu watamshangaa zaidi, nampongeza sana huyu msichana ana kipaji kikubwa sana mimi najua alimaliza kwa kusema Saada nassor.

Saada nassor alialikwa kuja kuimba hapa dar es salaam katika bendi bora ya gusagusa ndipo alipoweza kukutana na msichana huyu mdogo, mwembamba, akiwa ktk jukwaa la bendi hiyo, juhudi za kumtafuta khadija mbegu mwenyewe ili azungumzie pongezi hizi alizopewa na muimbaji nguli Saada nassor anazizungumziaje zinaendelea na tutawaletea humu humu mtandaoni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni