TANGAZA NASI

Breaking

Jumapili, 17 Desemba 2017

BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA JAHAZI MODERN TAARAB YAPANIA KUFANYA MAKUBWA!.

Na pambe za taarab.

Bendi yako pendwa ya jahazi modern taarab imeamua kubadili mfumo wa uongozi na sasa itakuwa ikiongozwa na bodi ya wakurugenzi wanne akiwemo mwana mama shupavu na jasiri Betty huku Hamisi Boha akibaki kama mmiliki wa bendi hiyo yenye mashabiki lukuki kulingana na takwimu iliyofanywa na mtandao huu.

Mikakati iliyowekwa na wakurugenzi hao katika kuhakikisha bendi inasonga mbele zaidi ni mikubwa na yenye malengo ya kuwanufaisha wasanii ambao watapata bahati ya kuwepo humo. Kwanza kuna fungu nono kabisa la pesa limetengwa kuhakikisha wasanii wale wa zamani wanarudishwa kwa gharama  yoyote ile bila kusahau hata wale ambao walionyesha uvumilivu katika kipindi chote cha nyuma wakati bendi inapitia katika wakati mgumu nao pia watapatiwa pesa.

Akizungumza kwa kujiamini Betty alisema kwa sasa ndani ya jahazi modern taarab hakuna msanii hata mmoja ambae atalialia njaa au kulalamika masuala ya kodi ya nyumba kwani bodi yetu tumeandaa mikakati ya kutafuta nyumba mbili ambazo tutazikodi kwa ajili ya kukaa wasanii wetu na kuweka maskani maalum kwani kwa sasa bendi yetu haina maskani jambo ambalo hutupa shida ya kufanya mazoezi na kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya nyimbo mpya.

Kwa sasa tupo katika mikakati maalum ya kukisuka upya kikosi chetu ikiwemo kuongeza wasanii wengine ikiwemo kuwarudisha baadhi ya wale walikuwepo zamani na chipukizi kadhaa hususani waimbaji wakiume maana kwa sasa hatupo na Amigo kama ambavyo inafahamika àlizungumza mwanamke huyo asieyumbishwa na lolote.

Alimalizia kwa kujinasibu kwamba kwa sasa bodi yao mpya ya wakurugenzi hao wanne wana uwezo wa kumnunua msanii yeyote yule ambae wao wanamtaka hatushindwi ila kikubwa tunafanya mambo yetu taratibu na kwa uhakika zaidi, nawaomba wapenzi wetu wa jahazi modern taarab wajiandae kupata vitu vizuri sana kwani muda mchache ujao tutaweka kambi kwa ajili ya kutengeneza nyimbo mpya zipatazo nne, huyo ndio Betty mmoja kati ya viongozi wapya ambao wanapatikana ndani ya Bodi hiyo mpya ya Jahazi modern taarab yenye watu wanne wenye mipango thabit na endelevu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni