TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 19 Desemba 2017

FATMA KASSIM:- SINA MPANGO WA KUIHAMA JAHAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab

Muimbaji wa siku nyingi wa bendi ya jahazi modern taarab Fatma kassim ameamua kufunguka na kuweka bayana baada ya tetesi nyingi kumuhusisha kwamba yu mbioni kujiunga na bendi moja mpya ambayo kwa sasa ipo ktk mipango ya kuisuka kwa kuchukuwa wasanii mbalimbali toka bendi tofauti.

Akizungumza na mtandao huu makini Fatma alisema kwanza hizo taarifa sijazipata na nazisikia kwako sasa hivi ila kama kweli zipo na hazijanifikia, napenda tu niwatoe wasiwasi viongozi wangu wapya wa jahazi modern taarab kwamba mimi nitaendelea kuwa ndani ya jahazi daima milele wala sijaona kwengine pakwenda ikiwa kila ninachohitaji napata toka kwa viongozi wangu, wapenzi na mashabiki wangu nawaomba wasiyumbishwe na maneno ya tetesi watakayo yasikia au wanayoendelea kuyasikia...mimi ni jahazi damu sina mpango wa kuhama wala sitarajii kuhama kabisa alimaliza kwa kusema muimbaji huyo ambae kwa sasa amejaaliwa kupata mtoto.

Hizo ndio sarakasi ambazo zinaendelea kwa upande wa wasanii wa taarab nchini Tanzania, tokea prince amigo aamue kujiondoa ndani ya bendi ya jahazi na kwenda kuanzisha chake mwenyewe kumekuwa na taarifa kadhaa wa kadhaa zikizungumzwa juu ya kikosi ambacho amigo atakitumia ndani ya bendi yake hiyo mpya wengine wakihusisha na waimbaji kadhaa ambao amigo alikuwa nao pale jahazi. Jambo la kusubiri ni kuona nini kitatokea kwa baadae.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni