TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 20 Desemba 2017

WAKALIWAO MODERN TARADANCE WATOA ZAWADI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA MASHABIKI.

Na pambe za taarab.

Bendi ya wakaliwao modern taradance imeachia vibao vitatu vipya kwa mpigo, maalum kama zawadi kwa mashabiki wake ndani ya sikukuu hizi za Christmas na mwaka mpya.

Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Thabit Abdul "mkombozi" alisema kuwa ameamua kukonga kiu ya mashabiki wake ambao walikuwa wakisubiri vibao hivi kwa hamu kubwa sana, nyimbo hizo ambazo ni Faraja ni Tunnu ulioimbwa na Aisha mtamu kabisa, Naupumzisha moyo ulioimbwa na Asya Mariam na Wapambe macho kodo ambao umeimbwa na Mohamedy Ally "mtoto pori", kwa sasa nyimbo hizo zote zinapatikana ktk redio zote na mitandaoni ili kila mmoja kwa nafasi yake aweze kuburudika alisema mkurugenzi huyo.

Akiendelea Thabit alisema kwa sasa tumefanya media tours karibia redio zote za dar kusambaza nyimbo hizo lakini nategemea baada ya sikukuu hizi mbili kupita natarajia kuanza ziara za mikoani ili kupeleka huduma za nyimbo hizi mpya kwa mashabiki wa wakaliwao waliopo mikoani alimaliza kwa kusema.

Wakaliwao modern taradance kwa sasa ndio bendi inayofanya vizuri ukilinganisha na bendi nyingine na kikubwa ni umoja ushirikiano na maelewano makubwa walionayo miongoni mwa wasanii na viongozi wao pia! Mtandao wa pambe za taarab unaitakia bendi hii mafanikio zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni