TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 30 Desemba 2017

MAJALIWA:- SHOW ZA KIINGILIO KINYWAJI NI MIONGONI MWA ADUI MKUBWA WA KUSHUSHA UBORA WA TASNIA YETU.

Na pambe za taarab.

Mkurugenzi wa bendi ya maja's modern taarab Hamisi majaliwa amesema miongoni mwa adui mkubwa wa muziki wetu huu waliochangia kuuweka hapa ulipo huu muziki ni hizi show za kiingilio kinywaji kiukweli zinatushusha sana hadhi bila wenyewe kujua.

Hamisi majaliwa aliyasema hayo baada ya kuulizwa ni jambo gani limefanya muziki huu kuporomoka na kufika hapo ulipo sasa?, kwanza kabisa alianza kwa kusema kuwa sababu zipo zaidi ya tatu lakini kubwa ni kwa baadhi ya bendi kupiga show kiingilio kinywaji tena bendi zingine ni kubwa nisingependa kuzitaja kwa majina. Mimi binafsi yangu kama mkurugenzi nasema kamwe sitopiga show ya maja's modern taarab kwa kiingilio kinywaji hata siku moja haitokei, kwa sasa hata wale wafadhiri wa makampuni mbalimbali ya udhamini hawataki kutupa udhamini, vipindi vya taarab katika redio kadhaa hazina wadhamini kuna redio zingine wameua kabisa vipindi vya taarab sababu vimekosa wadhamini tena kwa muda mrefu alisema mkurugenzi huyo.

Aliendelea kwa kusema kuwa bado hatujachelewa kama nia yetu ni kuiinua taarab basi tukubali kubadilika na tuseme na njaa zetu ili kuupa hadhi ile ya awali muziki huu.

Kwa sasa bendi kadhaa zimekuwa zikifanya show za kiingilio kinywaji kwenye bar mbalimbali hapa mjini na unapowauliza kwanini wameamua kufanya hivyo jibu wanakwambia khali ya uchumi ni ngumu sana pesa zimepotea na ndio sababu wanafanya hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni