TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 29 Desemba 2017

SAID KESSY:- SIWEZI KUMRUHUSU MKE WANGU FATMA MCHARUKO AKAJIUNGA NA JAHAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

Meneja wa bendi ya Yah tmk modern taarab Said kessy ambae pia ni mume wa muimbaji Fatma mcharuko amepiga simu katika dawati la habari la mtandao huu na kusema hayupo tayari kumuona mkewe Fatma mcharuko akijiunga na bendi ya jahazi modern taarab.

Said kessy aliyasema hayo kufuatia tetesi ambazo ziliandikwa jana na mtandao huu zilizokuwa na kichwa cha habari "jeuri ya pesa wasanii wawili nguli wa yah tmk kutimkia jahazi modern taarab". Unajua ndugu mwandishi labda mimi niseme kitu kimoja najua kila kinachoendelea kati ya mke wangu na baadhi ya viongozi wa jahazi, lakini napenda niwaambie tu kwamba itakuwa ngumu kwa mke wangu kujiunga jahazi modern taarab nawaomba waachane nae tu alisema meneja huyo wa yah tmk modern taarab.

Vile vile sio huyo tu, msanii yeyote wa yah tmk modern taarab hawezi kujiunga na bendi ya jahazi modern taarab, kwanza pale bendi hakuna muda wowote inakufa ile sasa uende pale ukafanye nini? sana sana itakufia alafu ukae eda aliongea kwa majigambo.

Mtandao huu wa pambe za taarab unasema wazi kuwa tutakuwa tukiandika kila habari ambayo ni ya ukweli ili kuwapa wasomaji wetu kitu roho inapenda, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya viongozi wa bendi hizi za taarab kupiga simu ofisini kwetu na kulalamika pindi tu wapoona wameandikwa vibaya, ukiwa binadamu ni lazima utakuwa na makosa hakuna aliemkamilifu sasa tukiwa tunaandika habari nzuri tu ina maana hakuna mabaya ambayo yanafanyika katika tasnia hii ya taarab nchini?...hebu badilikeni na muende na wakati wa sayansi na teknorojia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni