TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 30 Januari 2018

ABDUL MISAMBANO:- NINA NDOTO YA KUANZISHA BENDI YANGU YA TAARAB HAPO BAADAE.

Na pambe za taarab.

Muimbaji nguli wa TOT bendi Abdul misambano amezungumza na mtandao huu na kuweka wazi dhamira ya moyo wake hapo siku za usoni katika muziki huu wa taarab nchini tanzania, Misambano ambae ametamba sana na wimbo wa Assu hapo nyuma, sasa hivi ndio tegemeo ndani ya bendi ya chama TOT.

Unajua ndugu mwandishi nimetumika kwa kipindi kirefu sana katika bendi kadhaa wa kadhaa tokea huko Burundi mpaka hapa nyumbani tanzania, hivyo ndoto yangu ni kuwa na cha kwangu mwenyewe. Na plan zangu bendi ambayo nitaianzisha maskani yake siwezi kuweka hapa dar es salaam, mimi nitakuwa mikoani haswa! kama kuja dar labda kwa show maalum ila sitokuwa hapa.

Mwandishi wetu alimhoji kuwa inasemekana misambano ana mipango ya kuiacha bendi yake ya TOT na kujiunga na bendi ingine ya taarab lakini alikanusha taarifa hizo na kusema hajafikilia na wala wazo hilo halipo kabisa kichwani kwakwe, unajua hapa TOT mimi nalipwa mshahara napata posho nikitaka kukupa kimaendeleo nakupa kifupi TOT ni taasisi kubwa hakuna bendi yoyote ambayo inalipa mshahara msanii zaidi ya TOT sasa nitakuwa mjinga niache Neema niende katika shida brother alisema Abdul misambano.
ABDUL MISAMBANO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni