TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 31 Januari 2018

NEW SONG ACHENI POROJO YA PRICE AMIGO YAENDELEA KUBAMBA AFRIKA MASHARIKI.

Na pambe za taarab.

Wimbo mpya wa "acheni porojo" toka kwa Abubakary soud au Prince amigo umeendelea kufanya vizuri katika media mbalimbali afrika mashariki na kufanya mtangazaji mmoja wa pwani fm ya mombasa kenya aitwae Barisa kutabiri kwamba wimbo huu unaweza kuwa ndio bora kwa mwaka huu 2018.

Prince amigo ametoa wimbo huo takribani wiki moja sasa na kwa juhudi zake na mitandao kadhaa umeweza kusambaa takribani katika media zote afrika mashariki na nje ya mpaka ya afrika. Akizungumza na mtandao huu Amigo alisema kuwa wimbo huo ni maalum kwa wapendanao ambao wamekuwa wakipendana mno ila kuna maneno mbofumbofu toka kwa wambea kadhaa ambao hawataki kuona wanaendelea kupendana, unajua kwa sasa nimepania kuirudisha taarab katika zile anga zake kama zamani, baadae ya wimbo wangu huu natarajia mwezi ujao nitatoa wimbo mwingine wa wasanii wangu wengine na itakuwa ni mwendo wa dozi kila mwezi toka katika bendi yangu mpya nataka niwathibitishie watu kuwa mimi ndie mfalme wa muziki wa taarab kwa sasa.

Wapenzi na mashabiki wangu nawaambia wakae mkoa wa burudani kwani huu ni wakati wa burudani muendelezo toka kwa Prince amigo na kikosi changu na mimi sijaumbwa kushindwa watashindwa wao wanaonifuatilia lakini sio mimi alisema Amigo kwa kujigamba. Mtandao huu unapenda kumpongeza prince amigo kwa harakati zake kwani tokea ameachana na bendi ya jahazi ameendelea kupambana na kuonyesha ukomavu wake ndani ya tasnia hii ya taarab nchini tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni