TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 1 Februari 2018

GUSAGUSA MIN BENDI WAFALME WA OLD IS GOLD TAARAB TANZANIA.

Na pambe za taarab.

Unapoingia nchini tanzania hususani jiji la maraha Dar es salaam na kutafuta sehemu uka-enjoy taarab asilia jibu ni moja tu Gusagusa min bendi ambayo hufanya yao ndani ya ukumbi mwanana usio na bugudha wa Hugo house uliopo kinondoni.

Gusagusa ni bendi inayopiga taarab asilia na kwa sasa ndio inakamata namba moja kwa mafanikio ambayo wameyapata tokea kuanzishwa kwa bendi hiyo!, bendi hiyo tayari imeshafanya show zake katika nchi mbalimbali duniani kama uingereza, marekani, Comoro, mombasa kenya na hivi karibuni wana safari ya ujerumani, ushahidi huu wote unadhibitisha ubora wa bendi hii kuliko zingine ambazo zipo hususani hapa dar.

Zipo bendi zingine ambazo zinapiga old is gold taarab kama vile Raha original chini yake Ostaadh mohamedy pia Kongamoyo bendi chini yake Iqbary ambazo nazo zinafanya vizuri lakini kamwe hazijafikia mafanikio ya gusagusa min bendi. Na jambo lingine ambalo nadhani wadau wa muziki huu wa taarab asilia walikuwa hawajui ni kwamba bendi hizo zote za Raha original na Kongamoyo zimezaliwa kutokana na bendi ya gusagusa yaani viongozi wa bendi hizo hapo kabla walikuwa ndani ya gusagusa min bendi.

Unapolitaja jina la gusagusa min bend juwa kuwa umetaja jina kubwa sana tanzania, burudani wanayoishusha vijana hawa kila siku ya ijumaa na jumamosi ndani ya ukumbi mwanana wa Hugo house kinondoni sio mchezo, hebu fanya hamu siku moja ili uweze kufika na kupata raha hizi, hongera sana gusagusa min bendi...hongera mkurugenzi Hassan farouk "Achun baa".
GUSAGUSA MIN BEND WAKIWA STEJINI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni