TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 2 Februari 2018

HAMISI CHIZI MPIGA KINANDA ASIE IFAGILIA TARADANCE TAARAB.

Na pambe za taarab.

Hamisi chizi ni jina maarufu sana katika muziki wa taarab hususani taarab asilia, ukienda visiwani zanzibar, hapa dar es salaam na hata huko Dubai na oman ukilitaja jina la msanii huyu basi utaambiwa tunamfahamu vizuri.

Alipewa jina hilo la Hamisi chizi kutokana na umahili wake katika chombo hicho (kinanda) kwa jinsi anavyokipapasa kwa style mbalimbali huku akitabasam na kucheza, huyo ndio Hamisi mtu ambae hata siku moja huwezi kumsikia akikwambia anavutiwa na style hii iliyozuka hivi sasa ya taradance! anasema watu walioleta mtindo huu wana nia ya kuipoteza kabisa taarab, sisi tumelelewa katika muziki huu wa taarab na wazee wetu tokea utotoni hatujawahi kusikia muziki wa aina hii! mimi nawashauli ni vyema wakapeleka style hiyo katika singeli au mduara kama sio Baikoko lakini sio taarab wanaidhalilisha kabisa taarab alisema Hamisi chizi.

Hamisi ambae kwa sasa anapatikana hapa jijini la dar ingawa yeye ni mzanzibar halisi, mara kwa mara huwa na bendi ya Kongamoyo ama gusagusa min bendi, mwezi mmoja uliopita alikuwa Oman akifanya kazi ya muziki ambapo aliingia mkataba wa miezi mitatu na ilipokwisha alirudi nyumbani tanzania.

HAMISI CHIZI AKIPAPASA KINANDA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni