TANGAZA NASI

Breaking

Jumatatu, 5 Februari 2018

WADAU WA MUZIKI WA TAARAB NCHINI, MNAONA TUENDAPO NI SALAMA?.

Na pambe za taarab.

Wadau mara nyingi wamekuwa na thamani kubwa sana katika kuliendea jambo lolote lile ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa haraka na udhibiti  mkubwa.

Katika siku za karibuni muziki wa taarab umekuwa ukionekana kukosa ule msisimko wake uliozoeleka na kufanya baadhi ya redio kuondoa vipindi vyake hewani kwa kukosa wadhamini, kuna baadhi ya redio mfano kings fm ya njombe tanzania wameondoa kabisa kipindi cha taarab na redio zingine watangazaji ndio wamepewa majukumu ya kutafuta wadhamini ili kuweza kufanya vipindi wanavyoviendesha kuwa na uhai zaidi.

Ndipo nilipotazama na kuuliza hivi wadau wa muziki huu wanaona thamani ya tasnia yao inavyoporomoka kwa kasi ya ajabu? na nini wanapanga kuhakikisha muziki huu haupotei kabisa masikioni mwa wengi?, zamani nakumbuka wadau wa muziki wa dansi walikuwa na uwezo hata wakumsimamisha msanii ambae alikuwa anaonekana anakwenda kinyume na sheria za bendi yao! vile vile hata kama kuna msanii wanamtaka basi wadau wanaweza kuchangishana pesa na kumchukuwa msanii huyo na kumjumuisha ndani ya bendi yao...huo ni mfano tu!.

Nikirudi kwenu ndugu zangu mnafikili nini kifanyike ili muziki wetu wa taarab urudi ktk thamani yake kama zamani enzi za akina marehemu Amina chifupa?. Kwa sasa muziki wetu umekosa mvuto na kuna maneno yanazungumzwa kwamba baadhi ya viongozi wa muziki huu hawapendani kabisa!, nafikili baada ya kuendelea kukaa kimya ni vyema mkaitisha kikao cha wadau wote nchini ili kuzungumzia mustakabari au mwenendo wa muziki wetu ni wapi unapoelekea na nini tufanye ili kuunusuru usiporomoke shimoni kabisa.

Hapa tusiangalie mdau wa bendi gani ila sote ni wamoja tujumuike kwa pamoja ili tulijadili hili, kuwepo na semina elekezi pia kwa viongozi wa muziki huu ili kuwakumbusha kuwa upendo ni kitu bora na upendo unaleta maendeleo ya jambo lolote lile naamini tukifanya haya kwa kuanzia tunaweza angalau kupiga hatua kidogo. Mwisho kabisa tuamini kuwa sisi wadau ndio muhimili mkubwa wa kuifanya taarab iendelee kuwa juu zaidi na zaidi...mapambano bado yanaendelea!.

WAPENZI WA TAARAB WAKISEREBUKA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni