TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 6 Februari 2018

THABIT ABDUL "MKOMBOZI" MUASISI WA TARADANCE ALIEWATOA WAIMBAJI WENGI!.

Na pambe za taarab.

Kipindi naanza kulisikia jina la Thabit Abdul mtoto wa ilala ilikuwa ni pale TOT bendi enzi hizo akiwa na akina marehemu Banza stone bila kumsahau Leylah Hatibu wakifanya vizuri katika wimbo wa mtaji wa masikini ni nguvu zake na nyingine nyingi.

Naamini safari ya muziki ya Thabit Abdul haikuanzia hapo isipokuwa alianza chini zaidi kama ilivyo taratibu za wasanii wengi mpaka wanafikia mafanikio. Ila kwa mimi wacha nianzie hapo TOT maana naweza kusema ndipo mafanikio yake yalipoanza kuonekana, Msanii huyu kwa sasa naweza kudiriki kumuita ndio "mfalme halisi wa miondoko ya taradance nchini" amepitia bendi kadhaa za taarab tukiondoa dance ambapo alipita twanga pepeta, extra bongo bila kuisahau TOT.

Wakati marehemu Mariam hamisi anatokea five stars modern taarab na kujiunga TOT taarab pale alikutana na Director Thabit Abdul na akamtengenezea wimbo uliomrudisha katika ramani ya muziki huu wa taarab wimbo uitwao "sidhuriki na lawama" katika huu wimbo thabit Abdul alipiga kinanda na kuweka njia za uimbaji yaani melodie, mariam akaanza kutajika tena midomoni mwa wapenda taarab maana huu wimbo ulifanya vizuri sana, baadae Mariam na thabit walipanga kuandaa album yao binafsi ndipo alipomtengenezea wimbo mwingine nje ya TOT taarab uitwao "mti wa ridhiki upo kwa mungu" ambao nao ulikuwa moto si mchezo mpaka umauti unamfika mariam bado walikuwa hawajaweza kuitoa album hiyo.

Tukija kwa marehemu nyawana isale fundikira, thabit Abdul ndio mtu wa kwanza kabisa kugundua kipaji chake wakati anatokea tabora kuingia dar na akamtengenezea wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha kwa mashabiki uitwao "nipo kamili nimejipanga" hapa thabit kila kitu alifanya yeye kuanzia mashairi, uimbaji, muziki mpaka kupiga vyombo hapo ndipo utajua kuwa thabit ni mtu wa aina gani!, baadae wakati nyawana yupo tanzania motto modern taarab thabit alipendekezwa na nyawana aende akamtengenezee wimbo, kipindi hicho thabit yupo bendi ya mashauzi classic na alienda na kumtengenezea nyawana wimbo uitwao "behind the scene" au nyuma ya pazia kama ambavyo wapenzi wanauita, wimbo huu ulifanya vizuri mno katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Lakini kabla nyawana hajafariki thabit abdul alimtengenezea wimbo mwingine nje ya bendi ya T motto uitwao "shetani kataja jina" wimbo ambao mpaka sasa bado ni kipenzi cha mashabiki wa taarab.

Thabit abdul amewasaidia wasanii wengi mno hiyo ni mifano michache sana, mtu kama Aisha Othman Vuvuzella, Aisha mtamu kabisa, Asya utamu, Isha mashauzi, malkia khadija omary kopa na wimbo wa Full stop bila kusahau Mjini chuo kikuu, Hamuyawezi kondo, Mwalimu nassor na wengineo wengi sana!. Falsafa yake ya kuifagilia sana taradance ndio inayomfanya kuonekana ni tofauti na wenzie ingawa wapo wanaompa challenge mtu kama Chidy boy wa yah tmk na Ally J wa jahazi modern taarab ni wapinzani wake wakubwa katika upigaji wa kinanda.

Huyo ndio Thabit abdul mkombozi mkurugenzi wa wakaliwao modern taradance baba wa watoto watatu wakike Hawa, Radhia na Hafsa thabit, mtandao huu kama kawaida yake unampongeza kwa kile anachokifanya kuwainua wasanii wachanga na kufanya waheshimike zaidi katika tasnia hii ya taarab nchini.

THABIT ABDUL "MKOMBOZI" MKURUGENZI WA WAKALIWAO MODERN TARADANCE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni