TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 8 Februari 2018

BI MWANAHAWA ALLY:- HICHO CHAMA CHA TAARAB, KIWE NA SURA ZA TANZANIA BARA NA VISIWANI.

Na pambe za taarab .

Muimbaji mkongwe wa taarab nchini tanzania Bi mwanahawa ally au ukipenda muite jembe gumu ametoa maoni yake juu ya uanzishwaji wa chama cha taarab tanzania kuwa ni lazima kuwepo na sura mchanganyiko yaani bara na visiwani ili kuleta ule ushirikiano na isiwe bara peke yake kama inavyoonekana sasa kwa hawa wanaofuatilia suala hili.

Mkongwe huyu aliyasema haya baada ya kupigiwa simu na kuulizwa nini maoni yake juu ya kuanzishwa kwa chama cha taarab nchini tanzania, unajua ndugu mwandishi hili jambo la kuanzisha umoja wetu ni zuri mno kwani naamini sasa haki zetu wasanii tutazipata maana tumekuwa tukinyanyaswa sana na mapromota wanaotuchukuwa tukafanye kazi kwa kutudhurumu stahiki zetu tulizoelewana na hata wamiliki wa bendi yaani wakurugenzi nao katika mikataba tunayosaini wamekuwa wababaifu hawatutimizii kiukweli.

Ila ombi langu kubwa kwa hao wanaofuatilia mchakato huu ni lazima wafuate zile kanuni zetu za muungano tokea wazee wetu nikiwa na maana kwamba viongozi watakao chaguliwa basi ni lazima wawepo wa tanzania bara na visiwani tena wachaguliwe wale ambao wanaijua sana taarab, wapo wazee wetu pale malindi na hata Iqwuani swafaa na huku dar kuna wazee waliobakia pale Egpsion music club na Jkt wakichanganywa na vijana ambao ndio damu changa wataweza kufanya vizuri lakini ikiwa tofauti na hivyo basi hicho chama hakitokuwa na baraka za wazee wetu na kinaweza kupotea kwa muda mfupi tu amini nikwambiayo ndugu mwandishi alisema mkongwe huyo kwa msisitizo.

Chama cha muziki huu wa taarab nchini tanzania kipo katika mipango ya kufufuliwa na mmoja wa watu ambao wapo mstari wa mbele kuhakikisha chama hicho kinaanzishwa upya ni Siza mazongela Mamaa segere original, viongozi, wadau na wasanii wa muziki huu tunatakiwa tutoe ushirikiano wa khali na juu kwa hawa wenzetu ambao wanajitolea kuhakikisha tunapata chama cha kutetea haki zetu kama wasanii na wadau wa taarab nchini tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni