TANGAZA NASI

Breaking

Ijumaa, 9 Februari 2018

HASHIM SAID IGWEE 2018 KUJA NA SONG JIPYA NDANI YA MASHAUZI CLASSIC.

Na pambe za taarab.

Muimbaji tegemeo na asie na makuu ndani ya mashauzi classic Hashim said "igwee" amezungumza na mtandao huu na kueleza matarajio yake kwa mwaka huu 2018 ndani ya bendi yake hiyo inayoongozwa na Queen of the best melodies Isha ramadhan wa makongo.

Hashim alisema kwa sasa ana wimbo mpya kabisa ndani ya mashauzi ambao tayari wameanza kuufanyia mazoezi na mwanzoni jina la wimbo lilikuwa ni mapenzi mubashara ila mkurugenzi wangu Isha mashauzi amesema tubadili jina hilo maana limeshatumika katika bendi nyingine, kiukweli ni wimbo mzuri sana na naamini utanirudisha katika ramani ya muziki wetu maana ni muda mrefu sasa sijatoa wimbo mpya, jambo kubwa nawaomba wapenzi na mashabiki wangu kujiandaa kupata kitu kitamu maana sina historia ya kutoa wimbo mbaya tokea east african melody, dar modern, mashauzi yenyewe, wakaliwao mpaka sasa mashauzi tena alisema muimbaji huyo.

Bendi ya mashauzi classic inatarajia  kuondoka dar es salaam na kwenda kanda ya ziwa kwa show kadhaa hivyo wapenzi na mashabiki mnaombwa kuhudhulia kwa wingi katika show hizo kwani miongoni mwa nyimbo ambazo mtazisikia zikichezwa live ni huo wa Hashim said sambamba na ule wimbo mpya kabisa wa Isha mashauzi usemao "Nibembeleze".

HASHIM SAID " IGWEE" MUIMBAJI WA MASHAUZI CLASSIC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni