pambe za taarab.
Waswahili wanasema udugu sio kuzaliwa tu, wala udugu sio kufanana! wanachama wa group bora kabisa la whatsap "pambe za taarab" jana jumamosi tarehe 10/2/2018 walijitokeza katika shughuli ya kiongozi wao "admin" Bi mkubwa zuberi ambae alikuwa akifutwa jasho na kuupokea umama wa hiari kutokana kwa mmoja wa watu wake wa karibu.
Katika shughuli hiyo ambayo ilifana kwa kiasi kikubwa kwa burudani za muziki wa taarab, live bendi ilihudhuliwa na watu wenye majina yao mjini akiwemo mke wa mzee yusuph, Mamaa Leylah Rashid. Wanachama wa pambe za taarab walijitokeza kwa wingi sana wengine wakitokea mikoani mikoani mfano zanzibar, dodoma, tabora na tanga bila kuwasahau wanachama kutokea hapa dar es salaam. Akizungumza na mtandao huu kiongozi wa group hilo ambae ndie alikuwa mama shughuli Bi zuberi alisema kiukweli walichokifanya wanachama wa pambe za taarab sitokisahau, nawashukuru sana uungwana wao walionionyesha mwenyezimungu atawalipa inshallah.
Pia alitumia wakati huo huo kuwashukuru wale wote ambao walihudhuria shughuli yake na kuifanikisha kwa asilimia mia moja!. Group la pambe za taarab limekusanya wanachama wenye fani mbalimbali kuna ma-mc wa shughuli, kuna wapishi wa shughuli, kuna wasanii, kuna watangazaji wa redio mbalimbali, kuna wafanyabiashara na wengine wana NGO'S mbalimbali. Kwa sasa group hili ukitaka kujiunga nalo unatakiwa kutoa kiingilio cha shillingi elfu tano 5000/= tu kwa pesa za kitanzania na utaratibu mwingine utakutana nao humo humo katika group.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni