Mtafaruku unaoendelea baina ya malkia wa mipasho nchini tanzania bibie khadija omary kopa na mkurugenzi wa fungakazi modern taarab Kapten temba wa kudaiana pesa za malipo ya nyimbo ambazo kwa madai ya Kapten temba anasema alimtungia muimbaji huyo nguli kwa makubaliano ya kulipwa lakini mpaka sasa hajalipwa, kama utaachwa pasipo kuingiliwa na busara kutumika utafikia pabaya sana na kufanya mchezo hata damu inaweza kumwagika kwa wapenzi na mashabiki kupigana.
Kapteni temba ameandika katika ukurasa wake wa facebook unaojulikana kwa jina la "karya temba" akilalamika kudhurumiwa pesa zake na malkia huyo ambazo walipatana baada ya kumtungia mashairi ya nyimbo zipatazo nne ndani ya bendi yake ya ogopa kopa classic, lakini jambo ambalo sisi kama mtandao wa taarab nchini tumeona si busara ni kauli na maneno makali yasiyo na tafsida ambayo Kapten temba ameyatumia kwa mama huyu alie na mashabiki wengi tanzania na nje ya mipaka ya tanzania unapomuita mtu mzima kama khadija omary kopa kuwa ni mtu dhuruma ni kumshushia hadhi yake, malkia huyu ni "icon ya tanzania" vile vile ni icon ya muziki wetu huu wa taarab kumdhalilisha katika mitandao kwa umri wake tunaona si vyema hata kama ni kweli malkia anadaiwa basi zipo njia sahihi ambazo zingeweza kutumika kwenye kudai haki hii anayoizungumza Kapten temba.
Ukimsikiliza malkia wa mipasho nchini tanzania bibie khadija omary kopa katika clip zake alizotuma kwenye group la fans wake whatsap anakiri kudaiwa pesa na kapten temba kiasi cha shilingi laki tatu na tayari mwanzoni kabisa alimtumia shilingi elfu hamsini na akamuomba hizo zingine amvumilie kwanza sababu anashughuli ya harusi hapa kati lakini itakapokwisha basi atampatia pesa zake zilizobakia lakini temba hakuonekana kuridhika na majibu hayo ya malkia ndipo akaanza kwenda katika redio mbalimbali kuomba interview ili amchafue malkia huyo lakini alikuwa akikataliwa kufanya mahojiano, anaendelea kusema malkia huyo kuwa juzi tu hapa kuna pesa akawa amepata na nia ilikuwa ni kumlipa Kapten temba lakini ajabu mara anasikia amechafuliwa huko mtandaoni kwamba anadaiwa na Kapten temba na amepanga kumdhurumu!, sasa mimi nasema muacheni aendelee kuandika mimi simjibu na wala sitompa pesa yake iliyobakia kwanza mpaka amalize kunichafua ndipo nami nitampa pesa zake maana ameandika huko facebook kwamba huo ni Mwanzo tu habari kamili zitakuja alimaliza mama huyo asie na makuu.
Ukiingia katika account ya facebook ya Kapten temba na kusoma alichokiandika na ukapitia comment za mashabiki utaelewa ni kwanini nilisema damu zinaweza kumwagika, mashabiki wa khadija omary kopa wamechukizwa sana kwa kitendo alichofanya Kapten temba kumdhalilisha malkia huyo mitandaoni hivyo wametokwa povu la maana vijana wanasema, sasa hapa imehamia kwa wapenzi na imekuwa vita baina ya wanaompenda Kapten temba na wale wanaompenda khadija omary kopa je tunaupeleka wapi muziki wetu wa taarab?, suruhu ilishindikana mpaka tuletane mitandaoni?, hapa ndipo ninapokumbuka haki za msanii kama chama cha muziki wa taarab nchini kingekuwepo haya yote yangemalizwa na hakuna ambae angejua. Mtandao huu unapenda kuwaomba wadau wenye hekima zao kuingilia kati tatizo hili na kulipatia ufumbuzi ili maisha mengine yaendelee kwa pamoja tunasema tunalaaini vitendo kama hivi ndani ya muziki wetu wa taarab nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni