TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 13 Februari 2018

SENIOR BACHELOR MWALIMU WA MUZIKI MWENYE NDOTO ZA KUINUA VIJANA WENZAKE!.

Na pambe za taarab.

Nilianza kumfahamu senior bachelor tokea anasoma madrasa pale maeneo ya mburahati jijini dar es salaam na baadae alijiunga na bendi ya king's modern taarab iliyokuwa ikiongozwa na Director kijoka enzi hizo.

Huyu ndie nyota wetu wa leo ambae tutamchambua japo kwa kiasi kidogo nanyi wapenzi na wadau wa muziki wa taarab mumjue ni nani huyu jamaa. Senior bachelor bendi yake ya kwanza kabisa kujiunga nayo ni king's modern taarab na baadae alitoka na kwenda kuungana na Kapten temba na kuunda fungakazi modern taarab bendi ambayo ilipata umaarufu mkubwa hususani ule wimbo wao wa "inzi wa kijani", ndani ya wimbo ule senior aliweka sauti na kurekebisha mashairi  akishirikiana na Kapten temba, hakukaa sana kwani baada ya kutokea mtafaruku baina yake na Kapten temba aliamua kujiondoa na kwenda kuunda bendi yake mwenyewe ambayo inaitwa Bongo stars modern taarab akiwa na wasanii kama salma mikausho, salma sambwanda na wengineo wengi.


Ndani ya Bongo stars modern taarab  Senior alitengeneza nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana mfano wimbo uitwao funga domo na nyingine nyingi, baadae akiwa bado na bendi yake ndipo wakurugenzi kadhaa wa kadhaa wakaona umuhimu wake wakaanza kumtumia katika kuwatengenezea nyimbo zao mpya mfano bendi za jahazi modern taarab, supershine modern taarab, wakaliwao modern taarab na Majaz modern taarab ambapo mpaka sasa ameteuliwa kuwa director mkuu pamoja na kuwa na bendi yake. Ndani ya Majaz ametengeneza takribani album mbili zote akitunga yeye mashairi na kuweka melody yaani "uimbaji".


Katika siku za karibuni Senior bachelor amefungua chuo cha muziki ambacho kinapatikana manzese jijini dar es salaam katika kambi ya bendi ya Majaz modern taarab hapo wavulana kwa wasichana wanafundishwa njia za uimbaji, sheria na kanuni za kuwa muimbaji mzuri, kupiga vyombo vya muziki aina zote na taratibu zingine kama ambavyo vyuo vyote vya muziki vinavyofanya tena ni kwa gharama nafuu mno, kwa yeyote ambae anahitaji kujiunga na chuo hicho ili aweze kujifunza muziki basi anaweza kuwasiliana na Mwalimu huyu wa muziki kwa namba zake za simu zifuatazo:- 0679-600210 au 0719-626805. Mtandao huu unachukuwa nafasi hii kumpongeza senior bachelor kwa juhudi zake anazozionyesha katika kuuinua muziki huu kwa kurithisha vizazi kwa vizazi ili usije ukapotea moja kwa moja.

SENIOR BACHELOR AKIWA KWENYE POZI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni