Na pambe za taarab.
Uimbaji ni kipaji changu nilichojaaliwa na mwenyezimungu, haya ni maneno ya Omary Sosha muimbaji tegemeo katika bendi ya halichachi classic yenye maskani yake magomeni jijini dar es salaam.
Omary ameanza kuimba kaswida madrasa maeneo ya tandika, hapo ndipo kipaji cha uimbaji kilipoanza kuonekana na mpaka sasa bado anasoma madrasa na kutunga kaswida kadhaa wa kadhaa ikiwemo na kuimba pia. Sosha katika safari yake ya muziki aliwahi kupitia Dar modern taarab ambapo alikutana na muimbaji mwenzie Twaha malovee ingawa hawakukaa sana, baada ya Omary kuondoka Dar modern alikuwa akiimba katika bendi mbalimbali za taarab zinazoimba old is gold taarab zikiwemo gusagusa min bendi, Raha original, Aljazeera pamoja na Kongamoyo.
Lakini baadae alienda washawasha modern taarab ambapo alikutana na director Amour magulu ambae walikuwa wote Dar modern, lakini kutokana na mgogoro wa kiuongozi bendi hiyo ilivunjika ndipo wakaanzisha bendi hii ya halichachi classic yeye akiwa ni mmoja wa waanzilishi wengine wakiwa ni Amour magulu, mwanahawa Chipolopolo, Amrani na wengineo.
Mtandao huu ulitaka kujua toka kwa Omary Sosha nini matarajio yake katika muziki huu wa taarab?, nae alijibu kuwa nina ndoto ya kuutangaza muziki huu kimataifa zaidi, unajua mimi naimba aina zote za taarab yaani old is gold na hii taarab ya kisasa, naamini nitafanikiwa kwani mwenendo wangu sio mbaya unanilidhisha maana nikiangalia nilipotoka mpaka hapa nilipo sio pabaya namshukuru mungu.
Pia tulitaka kujua ni changamoto gani ambazo huwa anakutana nazo katika safari yake ya muziki?, alijibu kuwa changamoto ni za kawaida na wakati mwingine haziepukiki unaweza kuandaa nyimbo au wimbo kwa gharama kubwa lakini ajabu media zinakuwa hazikusapoti hii inarudisha nyuma sana juhudi zetu sisi wasanii ambao tunachipukia, ila kwa sasa kiasi media zimeanza kubadilika na zinacheza nyimbo zetu alisema Omary Sosha.
Huyu ni muimbaji tegemeo kwa taifa na halichachi classic modern taarab muite Omary Sosha!, mtandao huu unapenda kumpongeza kwa juhudi zake na tunamuasa asivunjike moyo kwani safari siku zote huwa na vikwazo na mitihani mingi kikubwa ni kugangamara na mungu atamfikisha pale anapopataka.
OMARY SOSHA AKIWA KWENYE POZI. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni