TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 10 Mei 2016

PRINCE BLACK KOPA ALUMBANA NA MWAJUMA WA RAS FM MBELE YA WATANGAZAJI 98 NDANI YA KIKAANGONI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

PRINCE BLACK KOPA.

             Kile kipengele chetu cha "kikaangoni wiki hii" ambacho hurushwa kila jumatatu saa moja kamili ndani ya group la watangazaji wa taarab liitwalo "ubuyu wa taarab" kiliendelea tena wiki hii na mgeni alikuwa prince black kopa tokea pale ogopa kopa classic bendi na kama kawaida baada ya kusalimia maswali yakaanza kama ilivyo ada.

 

DIVA WA HITS FM ZNZ:- Mambo vipi black kopa, nataka kufahamu toka kwako hivi ni kweli yule wifi uliekuwa nae na mwisho wa siku kupigana chini eti alisutwa na mama mkwe I mean khadija omary kopa? au maneno ya watu tu? lakini pia kuna siku ulifanyiwa interview katika redio flani ukaulizwa kuhusu yeye ukamkana kuwa humfahamu licha ya kumpandisha juu ya jukwaa kwenye show flani hivi, naomba majibu.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Sikiliza Diva, huyu mwanamke mimi sikuwa nae na mahusiano, mambo hayo ya kuposti kuhusu mimi anajua mwenyewe alivyofanya, mimi najua matatizo ya kuwa na mahusiano na mtangazaji na kuhusu hiyo kusutwa na mama mkwe hakusutwa wala nini, na kupanda juu ya jukwaa ni kawaida sababu ile show pia nae alishiriki kuandaa kule dodoma kwahiyo alikuwa anapanda juu kuimbaimba kuchezacheza lakini hakuna chochote mimi sina mahusiano na mtangazaji jibu ni hilo.

 

AISHA WA BARMED'S TELEVISHENI MWANZA:- Ningependa kujua ni skendo gani ambayo uliwahi kukutana nayo tangu umeingia katika tasnia hii ambayo ilikukwaza sana na je ilikuwa ya ukweli?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Mimi sipendi sana maskendo na wala skendo sina, zaidi nina skendo moja ambayo ndio hiyo imetokezea juzi ya kutembea na mtangazaji na iyo skendo sio ya ukweli, jibu ni hilo.

 

FORTINA WA CG FM TABORA:- Juzi mmezindua bendi sambamba na albam mpya, je kuna project yoyote mnategemea kuiachia hivi karibuni?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Sasa hivi kuna project ya nyimbo zetu hizo mpya kama nimempata mwenye maslahi ambayo niliimba pale dar live na kuna wimbo wa mama yangu khadija kopa ambao unaitwa hakuna mwenye mji wake, kuna wimbo wa shadya shombeshombe, kuna wimbo wa bi eshe mohamedy kuna wimbo wa mwamvita shaibu kuna mambo mengi tumeandaa huko katika siku zijazo na muda si mrefu mtaona wenyewe kwasababu sisi ogopa kopa huwa hatupendi kuongea hapa ni vitendo tu.

 

SHARIFA WA KAYA FM BAGAMOYO:- Ni kwanini uliamua kujikita kwenye muziki wa taarab kwa kipindi hiki ulikuwa unapenda tokea utoto au ulipoona mama anaimba na wewe ukataka kuimba?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Hapana mimi nilikuwa ni muimbaji tokea zamani sababu kabla ya kuimba taarab, nimeimba sana bongo fleva wakati nipo zanzibar, hivyo muziki upo kwenye damu kuanzia kizazi na kizazi.

 

       Wakati mahojiano yakiendelea Mwajuma wa ras fm dodoma aliingilia kati na kutuma voice note kujaribu nae kuweka wazi na kutolea ufafanuzi kwa yale anayo yazungumza black kopa na watangazaji wenzie yaani mwajuma, alianza kwa kusema kuwa yeye hana shida ya kumnadi mwanaume eti aonekane ametoka na superstar, au aonekane ametoka na mtoto wa flani nakumbuka huyu huyu black kopa ambae anasema eti mimi hajawahi kuwa na mahusiano na mimi kashfa kibao, kunitolea dharau kibao na kunidhalilisha pia mbele za watu kwamba hajawahi kuwa na mahusiano na mimi, siku alipokuwa akinitongoza kuna swali nilimuuliza wewe unanifuata mimi, lukini kumbuka kuwa mimi ni mtu ambae hali yangu ni ya duni sana hata wazazi wangu pia ni maskini hakuna hata anaewajua kwanza wazazi wangu wanaishi kijijini, mimi mwenyewe maisha yangu ndio kama haya unayoyaona ndio kwanza naanza kutafuta maisha, nakumbuka nilimuuliza huwezi kuhisi litakuja tokea tatizo hapo mbeleni itaonekana kama natoka na wewe ili nitafute kiki?.

 

        Lakini black kopa hakujibu swali hili la mwajuma zaidi ya kulalamika kwa admin kwamba asimamie utaratibu kwani anaetakiwa kurekodi voice note ndani ya kipengele cha kikaangoni ni yeye tu black kopa na wala si mtangazaji yeyote na ukweli upo hivyo hivyo kama alisema black kopa.

 

      Mwajuma aliendelea kueleza kuwa naumizwa sana na hayo unayo endelea kuyazungumza black, ni kweli mimi na wewe hatupo pamoja kimapenzi kwa sasa lakini sio kukataa kwamba hukuwahi kuwa nami kimapenzi au unataka niziposti humu kwa watangazaji sms zako za mapenzi ulizokuwa ukinitumia wazione? sikung'ang'anii no! ila naumizwa na kashfa zinazoendelea juu yangu, hizi sms niliziifadhi kama ushahidi kama lolote baya litatokea juu yangu, unachofanya black kopa ni kitu cha kitoto, binadamu sisi black kopa kuna kukoseana na mimi sijawahi kukukosea hata mara moja hujawahi kunifuma nipo na mwanaume wala kuifuma sms ambayo mimi nimetumiwa na mwanaume chochote kile hujawahi kufuma toka kwangu, kuachana ni kitu cha kawaida, kwani ukisema kuwa mimi na wewe tulikuwa na mahusiano tumeachana utakuwa umekufa?.

 

    Kikaango kilikuwa kimepamba moto na maswali yalikuwa yakiendelea toka kwa watangazaji wengine na black kopa alijibu kwa ufasaha mkubwa, kuhusu issue ya mwajuma black kopa alishikilia msimamo wake kwamba sio mpenzi wake na hakuwahi kuwa nae kimapenzi, habari ndio hiyo...kwaleo naona niishie hapo ila wiki ijayo kikaangoni tutakuwa na Hashim said mzee wa majanga, mwanamuziki ambae ameondoka pale wakaliwao modern taradance.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni