TANGAZA NASI

Breaking

Alhamisi, 21 Desemba 2017

ALJAZEERA OLD IS GOLD TAARAB, NDANI YA UKUMBI WA SPLENDED TANGA CHRISTMAS DAY!.

Na pambe za taarab

Bendi yako pendwa ya Aljazeera old is gold taarab siku ya sikukuu ya Christmas tarehe 25/12/2017 wanatarajia kushusha burudani yangu ambayo haijawahi kutokea jiini tanga ndani ya ukumbi mwanana wa splended kwa kiingilio cha shilingi 4000/= kwa mtu mmoja.

Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo mr Dot Do! alisema vijana wake mpaka sasa wapo kambini na wamepania kuwaonyesha wapenzi na mashabiki wao burudani maalum ambayo hawajawahi kuiona ikifanywa na bendi karibia zote za mkoa wa tanga, unajua taarab asilia ina ufundi wake hususani kwa kwenye uimbaji na upigaji wa vyombo hii ndio sababu nimeamua kuwaweka kambini wasanii wangu ili siku hiyo ya Christmas wafanye vitu vikubwa zaidi na zaidi.

Kwa upande wake muimbaji salma sambwanda akiwa kambini alisema ana usongo sana wa kuwanyamazisha wale wote wanaozungumza sana juu ya bendi yao na pia alichukuwa nafasi hiyo kumshukuru mkurugenzi kwa kuwaweka kambini na kuwapa huduma zote zinazostahiki kupewa msanii alimazia kwa kusema ahsante sana mkurugenzi Dot Do!.

Mtandao huu unawaomba wapenzi na mashabiki wa taarab mkoani tanga kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Christmas tarehe 25/12/2017 katika ukumbi wa splended kuwaona wana Aljazeera kwa kiingilio kidogo sana shilingi 4000/= kwa mtu mmoja na hautojutia pesa yako kwa burudani nzuri itakayotolewa na vijana hao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni