TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 23 Desemba 2017

GROUP LA PAMBE ZA TAARAB WHATSAP, KUUAGA MWAKA KWA PARTY BAB- KUBWA!.

Na pambe za taarab.

Group bora kabisa la whatsap ambalo lina-deal na kuinua muziki wa taarab nchini liitwalo pambe za taarab "wadau" kwa pamoja na viongozi wao wanatarajia kufanya party ya nguvu katika kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi admin wa group hilo Bi rukia ndege mtangazaji wa taarab ndani ya Abood redio na Abood televisheni ya mkoani morogoro alisema, sherehe hizo tumepanga kufanya mkoani dar es salaam siku ya jumamosi tarehe 27/1/2018 katika ukumbi ambao tutautangaza baadae ila katika party hiyo wasanii maarufu wataalikwa, watangazaji wa vipindi vya taarab sambamba na viongozi wa BASATA hii yote ni katika kuleta ukaribu na pia kufikisha salamu zetu kwa serikali ni kwa jinsi gani sisi wadau tunapambana katika kuufanya muziki huu utambulike kimataifa zaidi.

Aliwaomba wamiliki wa vituo vya televisheni na redio pindi watakapopata barua za kuwaombea ruhusa wanachama watangazaji wa group hili ambao wapo mbali na dar es salaam basi waweze kuwaruhusu  mara moja ili kuja kuhudhulia kwa pamoja na wenzao, kuhusu barua hizo za kuwaombea ruhusa tayari zimeandaliwa na hivi karibuni tutaanza kusambaza kwa wakurugenzi hao alimaliza kwa kusema.

Group la pambe za taarab whatsap linaendeshwa na viongozi makini ambao wamebuni segment mbalimbali ambazo zimekuwa zikiendeshwa ktk group hilo kwa siku tofauti tofauti, ni matumaini yetu hili litawezekana na kupisha mengine yajayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni