TANGAZA NASI

Breaking

Jumamosi, 23 Desemba 2017

SICHUKII WAPENZI NA MASHABIKI KUNIITA "KHADIJA KIPOTABO"...KWANGU RAHA TU!.

Na pambe za taarab.

Muimbaji chipukizi na mjanja mjanja mithili ya sungura awapo stejini khadija mbegu tokea jahazi modern taarab amesema yeye kupachikwa jina la "khadija kipotabo" na mashabiki wake wala hana neno ndio kwanza kwake raha tu!.

Khadija mbegu aliyasema hayo baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi kuwa anajisikiaje mashabiki wake kumpachika jina la "kipotabo"  na je anajua maana ya neno kipotabo?, unajua ndugu mwandishi labda nianze kwa kusema kwamba nawashukuru sana wapenzi kwa kunipokea vyema na kukubali uwezo na kazi yangu niwapo stejini, kupachikwa jina hilo mimi naona raha sana vile vile najua maana ya neno kipotabo, hili lina maana ya "kidogodogo" yaani kipotabo na mimi kweli ni mdogodogo na niwapo stejini shughuli yangu si ya mchezo alisema huku akicheka.

Unajua ukiona mpaka mashabiki wanakupachika jina basi juwa wazi wanakuelewa sasa nami nawashukuru kwahilo, ninapotangazwa kwenda mbele kuimba huwa nakuwa na mizuka mingi sana hivyo huanza kuimba na kucheza bila kuchoka, sasa wepesi ninao uonyesha pale kwa kulimudu jukwaa vyema ndio sababu ya wao kuniita khadija kipotabo yaani khadija kidogodogo alimaliza kwa kuzungumza khadija mbegu muimbaji wa bendi ya jahazi modern taarab.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni