TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 20 Desemba 2017

SHANGWE ZA CHRISTMAS NA MASHAUZI CLASSIC KUSINI TOUR!.

Na pambe za taarab.

Mashauzi classic bendi chini ya Queen of the best melodies Mamaa Isha mashauzi wanatarajia kufanya yao ndani ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya huko mikoa ya kusini, kilwa, lindi, masasi na liwale.

Akizungumza na mtandao huu makini Isha alisema wameamua kusikiliza kilio cha wakazi wa kusini baada ya kuwahitaji kwa muda mrefu na sasa wanaelekea huko panapo majaliwa, alizitaja show pamoja na kumbi watakazofanya show kama ifuatavyo, jumamosi tarehe 23/12/2017 watakuwa Bm resort "miwa pub" kilwa masoko. Jumapili 24/12/2017 watakuwa Bwalo la polisi lindi. Siku ya tarehe jumatatu 25/12/2017 watakuwa Rocky city masasi na tarehe jumanne 26/12/2017 watakuwa Samoma liwale wakazi wa maeneo hayo na vitongoji vyake mmetakiwa kujitokeza kwa wingi kwani kutakuwa na utambulisho wa baadhi ya nyimbo mpya za bendi hiyo.

Sisi mtandao wa pambe za taarab tunawatakia kheri mashauzi classic katika tour yao hiyo ambayo naamini itakuwa ya mafanikio kwani siku zote mashauzi huwa haibahatishi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni