TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 31 Desemba 2014

09:40

TASMINI YA UZINDUZI WA 5 STAR'S MODERN TAARAB NA G5 MODERN TAARAB HUU HAPA!!

NA KAIS MUSSA KAIS.

      Tarehe 19/12/2014 na tarehe 26/12/2014 kulikuwa na burudani ya uzinduzi wa albam za bendi mbili zilizofanana herufi kama sio majina, five stars wao ndio walianza kuzindua siku ya ijumaa tarehe 19/12/2014, kabla ya tarehe 26/12/2014 nayo ni ijumaa kuzindua albam tatu kwa mpigo bendi ya G5 Modern Taarab, na Bendi hizo zote zilifanya burudani katika ukumbi wa Travetine uliopo jijini Dar. Ifuatayo ni tasmini iliyofanywa na mtandao huu katika kuelekea kuufunga mwaka huu wa 2014.
HAMISI SLIM MKURUGENZI WA G5 MODERN TAARAB.


                                     "FIVE STAR'S MODERN TAARAB".

        Uzinduzi wao wa albam ya "Kichambo kinakuhusu" ulikuwa mzuri ila ulikuwa na mapungufu kiasi jambo lililopelekea maneno maneno kuzungumzwa sana na wapenzi waliohudhulia, kwanza Jokha Kasim ambae alitangazwa kama atakuwepo katika show hiyo hakutokea, Pili malkia wa mipasho nchini pamoja na kwamba alionekana ukumbini lakini hakupafomu na haikujulikana ni sababu ipi iliyopelekea mama yetu huyu kutopanda stejini. vyombo navyo vilisumbua sana, lakini tathimini inaonyesha kwamba Ally J aliwahi sana kufanya uzinduzi ule kwani tokea amezitoa nyimbo zake na kuanza kuchezwa redioni sio muda mrefu sana hivyo wapenzi bado hawajazizoea.


                                       "G5 MODERN TAARAB".

            Uzinduzi wa bendi hii inasemekana ulijaa ujanja ujanja watoto wa mjini wanasema, kwanza bendi zote zilizotangazwa kwamba zitakuwa zikisindikiza uzinduzi huo nikiwa na maana ya Extra Bongo na East African Melody ziligomea kufanya lolote ijapokuwa zilifika eneo la tukio, mtandao huu ulifanya mazungumzo na viongozi wa bendi zote mbili na madai yao yalifanana kwamba hawawezi kupanda steji mpaka wakabidhiwe pesa zao, hilo likawa tatizo kubwa ambalo kwa kiasi kikubwa lilileta usumbufu kwa wapenzi waliohudhulia onyesho hilo, lakini ukiondoa kadhia hiyo G5 wenyewe waliungurumisha muziki mpaka majogoo ijapokuwa watu baadhi walirudi majumbani kwao wakilalamika na haswa wakimtupia lawama mkurugenzi wa bendi hiyo Hamisi Slim.

ALLY J, MKURUGENZI WA FIVE STAR;S MODERN TAARAB.
 
                                                           "HITIMISHO".

             Ni wazi kabisa kwamba kwa asilimia themanini zinduzi zote hizi hazikufanya vizuri, swali la kujiuliza nini sababu iliyopelekea mapungufu haya kujitokeza?. Na ni kwanini iwe kwa bendi zinazofanana? yaani G5 na 5 STAR'S? Tafakari katika kuelekea mwaka mpya wa 2015!.

Jumanne, 30 Desemba 2014

23:22

SAIDI MITUTU AJIUNGA NA GUSAGUSA MIN BENDI, ASEMA KILICHO MBELE YAKE NI KAZI TU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

               Mpiga gitaa la besi ambae amewahi kufanya kazi katika bendi mbalimbali zikiwemo Dar Modern, Coast Modern Taarab, Aden Modern Taarab na nyinginezo nyinyi "Saidi Mitutu" amejiunga rasmi na bendi ya Gusagusa min bend.

         Akizungumza na mtandao huu Mitutu alisema kwa ridhaa yangu nimeamua kujiunga na bendi hii ili kujiendeleza zaidi na taaluma yangu, jambo lingine ujio wa Meneja Kais Mussa Kais katika bendi hii umenishawishi kwa asilimia kubwa zaidi mimi kufanya maamuzi ya kuja huku, Kais ni kiongozi mwenye historia nzuri hususani katika kila bendi aliyoiongoza imekuwa ikifanya vizuri sana

SAIDI MITUTU.
           Kwa upande wa meneja Kais alisema kwamba hizo ni rasharasha tu mvua kamili inakuja, nimepanga kukisuka upya kikosi changu na tayari nimeshafanya mazungumzo na viongozi wangu nikiwa na maana wakurugenzi wangu Foni Chupa na Hassan Farouk wao kwa pamoja wamenipa uhuru wa kuchagua msanii yeyote ninaeona anafaa kuwa na sisi basi niwajulishe na mara moja atajumuishwa kundini.

GUSAGUSA MIN BENDI KATIKA POZI.
        Wasanii wa zamani wa bendi hii wataendelea kuwepo ingawa kuna taratibu za kuongeza waimbaji na wapiga vyombo pia, Nataka kuifanya gusagusa kuwa ni bendi tishio zaidi na zaidi alimalizia kusema meneja Kais.

                                           "WAKATI HUO HUO"

            Bendi yako ya Gusagusa min bendi siku ya leo katika kuukaribisha mwaka 2015 wanatarajia kufanya show ya nguvu katika ukumbi wa Lango la Jiji uliopo magomeni mikumi jijini Dar wakishirikiana na Aljazira, Raha Original, Sabaha Muchacho pamoja na Bi Mwanahawa Ally. na siku ya tarehe 2/1/2015 Gusagusa min bendi itakuwa Kilwa kivinje katika ukumbi wa kivulini au almaarufu jumba la dhahabu katika kuwapa burudani wakazi wa huko.

Alhamisi, 25 Desemba 2014

05:47

HII NI MPYA KABISA:- KAIS MUSSA KAIS, NI MENEJA MPYA WA GUSAGUSA MIN BENDI

NA MWANDISHI WETU.

             Mkurugenzi wa mtandao huu makini wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Kais Mussa Kais au ukipenda unaweza kumuita "mzee wa fitina mjini" amejiunga na bendi ya Gusagusa yenye maskani yake magomeni jijini Dar katika nafasi yake ile ile ya umeneja.

          Akizungumza na mtandao huu Kais alisema kwamba ameamua kuhamia Gusagusa Min Bendi ili kupata uzoefu zaidi kwani anaamini ana safari ndefu sana katika muziki huu na mafanikio hayawezi kuja pasipo kujituma zaidi, Nilipokuwa meneja wa Supershine Modern Taarab, nilijitahidi kufanya mambo makubwa sana, ikiwemo kuifanya bendi hiyo kuwa miongoni mwa bendi tano bora kwa mwaka 2013-2014 na kuingia katika tamasha la mitikisiko ya pwani.

KAIS MUSSA KAIS MENEJA MPYA WA GUSAGUSA MIN BENDI.
       Vile vile nimefanikiwa kufanya video ya albam "huna style" ambayo kwa sasa inaonyeshwa sana katika vituo mbalimbali vya televisheni nchini, nyimbo zao pia zimekuwa zikichezwa sana redioni mara kwa mara na hii inanifanya kutembea kifua mbele huku nikijivunia baadhi tu ya mafanikio ambayo nimeyawezesha pale Supershine Modern Taarab.

      Naomba ieleweke sina tatizo na kiongozi wala msanii yeyote katika bendi ya Supershine Modern Taarab na ndio maana hata wakati nataka kuondoka pale sikuondoka kienyeji, nilienda kuwaaga viongozi wenzangu pamoja na wasanii kwa ujumla na kikao maalum cha kuagana kilifanyika pale pale club baada tu ya kumalizika mazoezi. Nashukuru nao walinipa baraka zao na kunitakia kazi njema huko niendako, kwa sasa mimi ni meneja wa Gusagusa Min Bendi Chini ya mwana mama wa haja kabisa BI AFUA SULEIMAN, MZEE SULTAN NA SABAHAH SALUM MUCHACHO hawa ndio wasanii waandamizi japo BI MWANAHAWA ALLY nae yupo yupo kwa mbaaali! alimalizia kusema meneja huyo mpya Kais Mussa Kais.

KAIS MUSSA KAIS, MENEJA WA GUSAGUSA MIN BENDI NA MMILIKI WA BLOG HII.
      Sisi dawati zima la habari la mtandao huu wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com Tunapenda kumtakia mafanikio mema huko aendako sasa Bosi wetu, na tunamuomba mwenyezimungu amuwezeshe kufanya makubwa zaidi akiwa na Gusagusa ili kupandisha zaidi na zaidi C.V. yake katika kuongoza bendi mbalimbali za taarab hapa nchini tanzania, ikumbukwe kwamba Kais Mussa Kais ameshaongoza bendi zaidi ya tatu akiwa kama meneja, ya kwanza ni T MOTTO, ya pili ni KING'S na ya tatu ni SUPERSHINE na kwa muda huu ndio amekamata usukani katika kuifikisha pazuri GUSAGUSA MIN BEND.....mungu akubaliki sana Bosi wetu!.
04:01

JE WAIJUWA HII?:- TAARAB NI NENO LITOKANALO NA NENO LA KIARAB! "TARAB?".

 NA KAIS MUSSA KAIS.

UDD NI KINANDA CHA KIARABU KINACHOPENDWA KATIKA

 TAARAB YA UNGUJA.
Taarab ni muziki ya Waafrika wa pwani iliyopokea athira kutoka tamaduni nyingi hasa muziki ya Waarabu na Wahindi. Kimsingi ni uimbaji wa mashairi unaofuata muziki wa bendi. Bendi hizi hutofautiana kieneo; katika taarab wa Unguja vinanda vya kulingana na tarab za Kiarabu hupendelewa; katika taarabu wa Mombasa aina za ngoma ni muhimu; katika taarab wa Tanga gitaa inapendwa. Siku hizi vyombo vya kisasa vimetumiwa pia.

HISTORIA.

Neno "taarab" laaminiwa lina asili katika Unguja ambako mnamo 1870 Sultani Sayyid Bargash alialika kundi la wanamuziki kutoka Misri kuja Zanzibar walioleta uimbaji wao aina ya "tarab". Alipopenda muziki hii sultani alimtuma Mzanzibari Mohammed bin Ibrahim kwenda Misri ajifunzi vyiombo vya huku. Mohammed aliporudi alikuwa mwanashairi wa Sultani akaendelea kuwafundisha marafiki vinanda vyake. Pamoja waliunda kundi la Nadi Ikhwani Safaa inayosemekana ni bendi ya kwanza iliyotumia jina la "taarab".[1]. Kundi limeendelea hadi leo na kujulikana sasa kwa jina la "Malindi Taarab"[2].
Hata hivyo muziki ya Waswahili inayojulikana leo kwa jina la taarab lina asili ya kale kushinda jina hili ambalo ni kawaida siku hizi. Kuna kumbukumbu kutoka Lamu ya muziki iliyoitwa "kinanda" iliyounganisha uimbaji pamoja na chombo cha kibangala na ngoma ndogo na waimbaji wake walihamia Zanzibar wakaitwa "taarabu" huko.

TAARAB KATIKA UTAMADUNI WA USWAHILINI.

Katika utamaduni wa Waswahili taarab ilikuwa utamaaduni wa pekee kwa sababu ilikuwa mahali pa pekee ambapo wanawake walifika kwenye jukwaa pamoja na wanaume na kuimba. Kwa sababu hii taarab imepingwa mara kwa mara na viongozi wa kidini walioona aina kadhaa za taarab ni haramu hazilingana na masharti ya dini hasa wakati wa mwezi wa Ramadhani na kama watu wanaanza kucheza.[3]
Miaka ya nyuma muziki ya taarab imesambaa hata barani nje ya utamaduni wa Waswahili inavuta wasikilizaji katika miji mikubwa kote Afrika ya Mashariki hadi Burundi na Rwanda. Bendi mbalimbali zimeingiza vyombo vya kisasa vya muziki katika mtindo wao kama vile keyboard na gitaa ya umeme.

03:39

NURU MOSHI:- "WAFADHILAKA WA PUNDAKA...LIKIKUCHOMA LAKO HILO!!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

            Nuru Moshi ukipenda muite "mamaa wafadhilaka wapundaka" ni muimbaji wa bendi ya Supershine Modern Taarab yenye makazi yake magomeni jijini Dar, Msichana huyu ambae anasema ameanzia kuimba katika bendi hiyo na mpaka sasa yupo hapo, Anamshukuru sana marehemu mama yake mzazi kwani yeye ndio ambae amegundua kipaji chake na kumpeleka katika bendi hiyo kumuombea nafasi ya kuimba, mungu amrehemu sana mama yangu.

NURU MOSHI "MAMAA WAFADHILAKA WA PUNDAKA".
             Wakati najiunga na bendi hii nilikuwa ni mtu mwenye uoga sana ukizingatia sijawahi kuimba katika bendi yoyote ile kwahiyo kila kitu nilikuwa nakiona kigeni kwangu, nilipokelewa vizuri na Queen Salma mlezi wetu akanionyesha misingi ya uimbaji na nilifuata maelekezo mpaka sasa nipo hapa japo kwa mafanikio machache niliyopata, Mwaka jana nilifanikiwa kurekodi wimbo wangu wa kwanza kabisa uitwao "WAFADHILAKA" katika studio za soundcrafters temeke, na namshukuru mungu kwani wimbo wangu umekuwa ukifanya vizuri sana katika vituo vya redio na televisheni hapa nchini na nchi za jirani.

NURU MOSHI WA MWISHO KULIA AKIWA NA WASANII WENZIE WA SUPERSHINE.
       Kuna watu huwa wanapenda sana kujihisi, sasa mimi nawaambia kwamba wimbo wangu sikumlenga mtu, ni ujumbe tu nimeufikisha kwa jamii kwani walimwengu wamekuwa hawana shukurani hata uwanunulie ndege!, ila kama kuna mtu anajihisi wimbo huo unamlenga yeye, na limemchoma haswaa!...basi hilo lake limemganda.

          Nuru amewashukuru sana viongozi wake kwa kuweza kumuamini na kumjali mpaka kufikia kurekodi wimbo huo, amewaasa wasanii wenzie kuvumilia kwani yeyote mwenye subira basi ategemee heri toka kwa manani.


Jumatano, 24 Desemba 2014

01:01

JE UNAJUA MZEE YUSUPH ALIANZA VIPI MUZIKI WA TAARAB?...BASI USIPITWE MSOME HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS

          Katika muziki wa taarab, Mzee yusuph ni mtu alieleta changamoto kubwa sana mpaka sasa, lakini je unajua alianzaje kuimba muziki huu?, ungana nami katika mahojiano haya:-

SWALI: Sasa turudi upande wa historia yako, labda tueleze ulizaliwa lini ukakulia wapi, maisha yako kwa ujumla.

JIBU: Nimezaliwa miaka 1977 na nimezaliwa Zanzibar. Nimelelewa kulekule nimekulia kulekule na kazi zangu nilianza kule kule za usanii, na nimemaliza darasa la 10 Zanzibar katika shule ya Haile Selasie.
Sikuwa nataka tena kuendelea na shule sababu niliona hali ngumu, si unajua maisha? nkaona hata! Hii ndio itanipeleka hii, sa niache huku. Niache moja nikamate moja.

Kwa hiyo niliacha shule, sikuendelea darasa la kumi na moja. Nikaanza mziki. Nilikuwa nafanya mziki nafanya maigizo, niko na shule, sa ilifika pahali sa nikachukuliwa na bendi ya melody.
Sa nkaona kidogo hapa kuna maslahi japo nilikuwa ‘napigwa buku kwa siku’ (nalipwa shilingi elfu moja kwa siku), lakini nilikuwa nashukuru sababu nilikuwa siipati ile buku,
MFALME MZEE YUSUPH PICHANI.
SWALI: Sasa umeingia katika mziki wa taarabu. Ni muziki ambao kwa kweli unapendwa. Wengi wakisema mziki wa mwambao, wengine hivi, alimradi kila mtu na lugha yake anavyouita mziki huu. Ulipata ushawishi gani mpaka ukaingia katika ulimwengu huu wa mziki wa taarabu?.

JIBU: Kwa kweli labda unajua kwa nilipokuwepo taarabu ndio ilikuwa inapendwa na nilikuwa na uwezo wa kuimba taarabu si vingine.
Na sikutegemea kama mtakuwa labda nami naweza kutunga nini mm’kh! Nilikuwa nahisi naweza kuimba. Sababu hata tulikuwa tunakaa nyumbani, tulikuwa tunamsikiliza mother (mama) anaimba, anaimba taarabu, tunakaa naye anatufahamisha hii inaimbwa hivi, hii ndio hivi, hii ndio hivi.
Sa ikafika mahali yani ile muziki ukawa unanijaa. Unanijaa sana kiasi ikafika mahala kwenye mazoezi ya mpira nawaambia wenzangu mimi ntakuwa naimba taarabu.
Basi kwa sababu nilikuwa napenda, halafu ni kwamba uwezo nilikuwa nao. Pale ndo nilipokuwa na ilo nivutia, lakini sio kuwa nilifikiria labda kumuona mtu mmmhkh! Sababu nilikuwa naweza.
Halafu mama yangu mzazi alikuwa mwimbaji wa taarabu.
00:36

GUSAGUSA MIN BENDI NDANI YA IKWETA GRILL MTONI, SIKU YA CHRISTMAS USIKOSE!.

NA KAIS MUSSA KAIS

               Bendi yako ya Gusagusa Min Bendi, katika kusherehekea sikukuu ya christmas, wanatarajia kushusha burudani ya nguvu katika ukumbi wa ikweta grill mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar, Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Mr Hassan Farouk alisema maandalizi ya show hiyo yamesha kamilika na vijana wana khali kubwa ya kuwaonyesha wakazi wa mtoni ni nini Gusagusa wanafanya.

WAIMBAJI WA GUSAGUSA MIN BENDI WAKIWA KATIKA POZI.
       Gusagusa ni bendi iliyojizolea umaarufu mkubwa kutokana na style yao kubaki pale pale wala hawayumbi kuwafuata wale wenzao wa taradance, bendi hii mara kwa mara imekuwa ikipata mialiko ya nje nchi kwa kuwa ni wao tu ambao wamebakia wanaopiga taarab asilia na modern taarab ukiziondoa bendi za zanzibar.

VIONGOZI NA WASANII WA GUSAGUSA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.
      Kwa sasa bendi hii ipo mbioni kuandaa vibao vipya na vibao vingine vipo tayari na vitapigwa kwa mara ya kwanza katika sikukuu hii

ya christmas pale ikweta grill, wadau na wapenzi mnaombwa kujitokeza kwa wingi kuja kupata raha za Gusagusa Min Bend.

Jumapili, 21 Desemba 2014

20:14

BIRTHDAY YA JAHAZI MODERN TAARAB, UMATI MKUBWA WAHUDHULIA, NI HISTORIA HAIJAPATA KUTOKEA!.


NA KAIS MUSSA KAIS.
          "KWA MSAADA WA MTANDAO WA SALUTI 5.COM".


MZEE YUSUPH NA HADIJA YUSUPH.

 Sherehe za miaka minane ya Jahazi Modern Taarab, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, jijini Dar es Salaam, zimefana kupita kiasi.
KHADIJA YUSUPH NA MZEE YUSUPH.
ONYESHO LA MIAKA 8 YA JAHAZI MODERN TAARAB LATIA FORA …pata picha 30
Ilisisimua pale wasanii wa zamani wa Jahazi kama vile Fikirini Urembo (mpiga solo wa kwanza wa kundi hilo), Jumanne Ulaya, Bi Mwanahawa Ali na mpiga kinanda Ally Jay walipopanda jukwaa la Jahazi na kushiriki kwenye baadhi ya nyimbo.
Sherehe hizo ambazo licha ya kuandamana na onyesho kabambe la Jahazi, pia zilisindikizwa na ‘babu’ zao East African Melody, zikashuhudia wasanii waliodumu kwa miaka hiyo minane bila kuhama wakizawadiwa tuzo za utumishi uliotukuka.
Si hivyo tu, wasanii waliodumu kwa muda mrefu japo waliwahi kuhama, nao pia wakajumuishwa kwenye zawadi nono zilizotolewa.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa wasanii waliodumu kwa muda mrefu na wale ambao hawajahama kabisa ni pamoja na friji, TV na music system (Home Theatre).
Kimahudhurio, onyesho hilo lilihudhuriwa na umati mkubwa ambao haujawahi kuonekana ukumbini hapo kwa miezi ya hivi karibuni.
Mpangilio wa nyimbo za Jahazi ulikuwa ni wa kuvutia sana ambapo waliweza kugusa karibu kila albam yao kuanzia albam ya kwanza kabisa  “Two in One” hadi “Chozi la Mama”.
Mzee Yussuf akakamua nyimbo tatu mfululizo: “Nakula kwa Nakshi Nakshi”, “VIP” na “Mahaba Niue” ambao ni mpya kabisa.

Pata picha kadhaa.
 Bi Mwanahawa akiwa na Melody jukwaani
 Bi Mwanaidi Shaaban wa East African Melody 
 Khadija Yussuf wa Jahazi
 Hassan Soud mkali wa kinanda wa Melody akifanya yake
 Taswira ya jukwaa la show ya  miaka 8 ya Jahazi
 Keki ya Birthday ya Jahazi
 Mzee Yussuf amkimlisha keki mkurugenzi msaidizi wa Jahazi, Hamis Boha
 Hivi ndivyo keki ilivyoingizwa jukwaani kwa mashasham
 Kessy Mbasha akimkabidhi Hadija Yussuf zawadi kwa niaba ya uongozi wa Jahazi
 Leila Rashid akiimba "Fanya Yako"
 Juma Mbizo akimkabidhi Babu Ali cheti maalum
 Hamis Boha akimkabidhi Mussa Mipango zawadi ya Home Theatre
 Mwanahawa Ali akiimba "Roho Mbaya Haijengi" na Jahazi
 Mtangazaji Mwanne Othman wa East Africa Radio akiwa na mtangazaji kutoka Kenya Fathiya Omar
 Mzee Yussuf akimlisha keki Bi Mwanahawa
 Mzee Yussuf akimkabidhi Leyla Rashid cheti utumishi uliotukuka  
 Mzee Yussuf akiimba "VIP"
 Umati uliofurika Travertine
 Watu walikuwa wengi sana
 Ramla wa Meledy akifanya yake na kundi lake
Miriam Amour (kulia) akapewa na bendi yake zawadi ya friji, aliyepewa jukumu la kubidhi zawadi hiyo ni Said Mdoe (kushoto)
 Seif Magwaru akimkabidhi cheti Fatma Ally "Shobo"
 Ally Jay akipapasa kinanda kwenye wimbo VIP
 Hamis Boha akimkabidhi mpiga kinanda Chid Boy zawadi ya TV ya kisasa
 Jumanne Ulaya akipiga solo kwenye wimbo VIP
 Ummy Suleiman kutoka Time FM ndiye aliyekuwa MC wa onyesho hilo
 Ummy akifanya yake
 Fikirini Urembo akipiga solo katika "Nakula kwa Nakshi Nakshi"
 Waimbaji wa Jahazi
 Waimbaji wa Jahazi
08:38

FADHILA MNOGA, MDOGO WA HADIJA MNOGA KIMOBITEL ANAESUMBUA G5 MODERN TAARAB KWA SASA.

NA KAIS MUSSA KAIS

         Kuna msemo wa kiswahili usemao 'Maji hufuata mkondo", Fadhila Mnoga ni muimbaji wa bendi ya G5 Modern Taarab yenye makazi yake mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar, Huyu ni mdogo wa Khadija Mnoga kimobitel ambae anaimba miondoko ya Dansi kwa sasa. Unapotembelea pale Flamingo Night Club ukamuona Fadhila akiwa steji na bendi ya G5 utakubaliana na mimi kwamba huyu msichana anaweza sana na ni hazina ya baadae katika muziki huu wa taarab nchini Tanzania.

FADHILA MNOGA AKIWA KATIKA POZI.
          Fadhila Mnoga amezunguka bendi nyingi ndogondogo kabla mwaka jana hajajiunga na bendi ya Dar Modern Taarab, lakini kwa bahati mbaya hakukaa sana kwani alikuwemo katika wale wasanii 13 ambao walifukuzwa katika bendi hiyo baada ya kurudi safari na Dar Modern toka mikoani, iliniuma sana kufukuzwa bendi kwa kosa nisilotenda lakini mungu alikuwa na mipango yake kwangu, na kwa sasa nipo hapa G5 Modern Taarab maisha yanaenda kama kawa kama dawa!.

      Taarab ni muziki niupendao sana na nafanya kwa mapenzi makubwa mnoo!, hapa G5 Modern Taarab nipo na ndugu yangu anaitwa Sharifa Mnoga nae ni muimbaji mzuri sana, sisi katika familia yetu wengi ni waimbaji ukimtoa Dada Hadija ambae tayari anafahamika lakini tupo na sisi tunafuata nyayo zake pia.


FADHILA MNOGA AKIWA NA DADA YAKE HADIJA MNOGA "KIMOBITEL".
         Fadhila Mnoga bado hajarekodi wimbo wowote G5 ila yupo mbioni kupewa wimbo mpya ambao ndio atatoka nao na watu kuelewa uwezo wake, kwa sasa anaimba sana nyimbo za G5 ikiwemo wimbo uliorekodiwa na dada yake Hadija Mnoga uitwao "Naepuka Mifarakano". njoo umuone akiimba ndani ya bendi hiyo pale Flamingo Night Club magomeni mwembechai Dar.
06:55

LEO NDIO LEO...NI USIKU WA MIAKA MINANE YA JAHAZI MODERN TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS

              Ile siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa muziki wa taarab nchini hususani wale wanazi haswa wa Jahazi Modern Taarab imefika, ni pale katika ukumbi wa travetine magomeni jijini Dar, bendi kubwa na yenye mafanikio katika tasnia ya muziki wa taarabu kwa sasa Jahazi Modern Taarab leo inasherehekea kutimiza miaka minane ya mafanikio tokea kuanzishwa kwa bendi hiyo.

          Akizungumza na mtandao makini na bora kwa sasa kwa habari za taarab ubuyuwataarabutz.blogspot.com, Director wa bendi hiyo Mohamedy Mauji amesema kwamba siku ya leo kutakuwa na surprise nyingi sana kuanzia kwa wadau, wapenzi mpaka wasanii wa zamani ambao waliwahi kuitumikia bendi hii kipindi cha nyuma, uongozi kwa kuwaheshimu na kuthamini mchango wao umewaalika na kutakuwa na vitu maalum kwa ajili yao.

JAHAZI MODERN TAARAB NA EAST AFRICAN MELODY
          Show itaanza mapema ili kuweza kuwapa burudani mpaka zile nyimbo za Jahazi za muda mrefu, kikubwa tunawaomba wapenzi wetu wajitokeze kwa wingi tuje kula keki kwa pamoja, wapenzi wetu waliokuja toka kenya, Comoro, kongo, Uganda na kwingineko nawaomba wasogee travetine mapema ili wapate burudani.Mtandao wa ubuyuwataarabutz.blogspot.com unapenda kuchukuwa nafasi hii kuupongeza uongozi wa bendi hiyo kwa kuweza kuandaa sherehe kama hiyo.

Alhamisi, 18 Desemba 2014

19:39

MWILI WA AISHA MADINDA WASHINDWA KUFANYIWA UPASUAJI, MAZISHI YAKE BADO NI KITENDAWILI.



NA KAIS MUSSA KAIS.


Kile kinachoonekana kama aina fulani ya urasimu, upasuaji (postmortem) wa mwili wa dansa Aisha Madinda uliokuwa ufanyike jana mchana (Alhamisi) umeshindikana na sasa utafanyika leo (Ijumaa) asubuhi.
Meneja wa Aset, Hassan Rehani ameiambia Saluti5 kuwa mwili wa Aisha aliyefariki Jumatano asubuhi ulihamishwa kutoka Mwananyamala Hospitali kwenda Muhimbili kwaajili ya upasuaji ili kujua chanzo cha kifo, lakini ikashindikana kwa madai ya muda wa kufanya upasuaji umekwisha.
UPASUAJI MWILI WA AISHA MADINDA WASHINDIKANA, SASA UTAFANYIKA IJUMAA ASUBUHI …huenda ikabadili muda wa mazishi
Hassan Rehani amesema Muhimbili wamedai mwisho wa kufanya ‘postmortem’ unakwisha saa nne asubuhi na hivyo zoezi hilo sasa litafanyika Ijumaa asubuhi chini ya usimamizi wa polisi.
Kwa hali ilivyo, kama utatokea urasimu au ucheleweshaji wowote wa kuufanyia uchunguzi wa mwili wa Aisha Madinda, basi ni wazi kuwa ratiba ya mazishi inaweza kubadilika.
Aisha Madinda alitarajiwa kuzikwa Kigamboni Ijumaa mchana mara baada ya sala ya Ijumaa. Mwanzoni kabila ilikuwa azikwe Alhamisi saa 10.

Wakati familia ya Aisha Madinda ilikuwa radhi kumzika ndugu yao bila ya uchunguzi zaidi, polisi iligoma kabisa na kusema kwa mazingira ya kifo chake, upasuaji ni suala la lazima.
19:25

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KIBAO KATA NA BAIKOKO?.

 Na pambe za taarab

Ngoma ya (Kibao Kata),ni ngoma ambayo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kumfunda mwali na kumpatia maadili mazuri pindi anapokwenda kwa mume wake, lakini kwa sasa ngoma hiyo imebadilishwa na kuwa ni moja ya ngoma zinazopotosha kabisa maadili ya kitanzania,hii ni  ngoma yenye asili haswa ya watu wa ukanda wa pwani, vijembe vya hapa na pale huwa vinatawala sana mpaka kufikia kuvuana nguo na kubaki utupu!

HAPO KIBAO KATA KIMEKOLEA MBAYAAA!!

Kufuatia hali kama hiyo, mara nyingi msimamizi wa shughuli huwa anasimamisha shughuli alafu huingilia kati na kusema kama kuna mtu ana kisasi na mwenzake akamalizie nyumbani kwao na siyo hapa.
MUIMBAJI KIVURANDE JUNIOR AKIFANYA YAKE.
“Jamani hii  ni shughuli ya fulani anamtaja jina lake na si ya mtu mwingine, hivyo kama kuna mtu ana tatizo na mtu ni bora aende kumalizia nyumbani kwake lakini siyo hapa, haihusu,” na akina mama humalizia kwa vicheko vya umbe, haloooooooooooh!!.
HIYO INAITWA MPAKA CHINI STYLE!.

Hata hivyo, katika hali ya kustaajabisha mastaa wengi wakike Dar huingia  kati na kushindana kukata nyonga huku kila mmoja akijivunia jinsi alivyoumbwa na Muumba, ngoma hii haina tofauti sana na Baikoko katika asili ya uchezaji maana wote wanatumia nyonga zao katika kunyumbulisha maungo yao manene yaliyojazia, pata baadhi ya picha za ngoma hiyo ni vipi wanavyocheza!!.
STYLE YA MMOJA MMOJA KATIKA KIBAO KATA.
HATAREEEEEE!.
HAPO, HAPO, HAPO CHACHAAAA!.