TANGAZA NASI

Breaking

Jumatano, 27 Aprili 2022

09:30

BLOG BORA YA TAARAB YAREJEA.

Na mwandishi wako.

            Muziki wa taarab ni alama tosha ya ukombozi katika nchi hii ya Tanzania, katika siku za karibuni tasnia hii imekosa msisimko na hii inatokana na kukosa promo za mitandaoni kama zilivyo fani zingine.

           Lakini sasa kampuni ya Skillman media chini ya mkurugenzi wake Kais mussa kais imeonelea ni vyema kuifufua tena blog yake ambayo ilijizolea umaarufu mkubwa hapo zamani ya Pambe za taarab.

     Upo mpango wa kurudisha kila kitu ambacho kilikuwepo kwenye blog hii na hata jina la blog kuna uwezekano tukarudisha lile ubuyu wa taarab kama ilivyokuwa awali, natumai tutashirikoana wadau na wasanii ili tuweze kuufikisha mbali muziki wetu.

Jumatano, 18 Machi 2020

04:20

Corona yaahirisha safari ya Mzee Yusuph kurudi mjini.

Na kais Mussa kais.



         Hatimae ile hashtag ya narudi mjini aliyokuwa akiitumia mzee yusuph imesitishwa rasmi jana baada ya serikali ya jamhuri ya muungano kuzuia shughuli zote zenye mikusanyiko kwa mwezi mzima kuepuka maambukizi ya gonjwa la corona ambalo ni tishio kwa sasa ulimwenguni.

            Mzee yusuph alitumia mitandao yake ya kijamii kuwahabarisha wadau wake kwamba kutokana na maagizo ya serikali kusitisha shughuli zote za mikusanyiko mbalimbali kwa siku 30 ili kuepusha maambukizi ya gonjwa hili baya nchini, nae amesitisha kwa muda ujio wake mjini mpaka hapo baadae.

      Lakini aliendelea kusema kuwa atawekeza nguvu zaidi studio kurekodi nyimbo zake kwahiyo yeyote ambae atakuwa tayari kudhamini gharama za kurekodi basi awasiliane nae milango ipo wazi kabisa, huyo ndio mzee yusuph ambae watu walikuwa wakisubiri kwa hamu ujio wake mjini kila mmoja akisema lake juu ya ujio wake mpya.

Wakati huo huo serikali ya Jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia kwa waziri mkuu amepiga marufuku matasha yote ya muziki nchini kwa muda wa siku 30 mpaka hapo litakapotoka tangazo lingine.

Jumanne, 17 Machi 2020

06:18

BONGO STAR'S MODERN TAARAB KUISIMAMISHA DAR LIVE KTK UZINDUZI WA ALBAM YAO MPYA!


Na Kais Mussa Kais.


        Bendi yako ya Bongo stars modern taarab yenye maskani yake mbagala jijini dar ipo mbioni kuzindua albam yake mpya inayokwenda kwa jina la bahari ya huba siku ya ijumaa tarehe 20/3/2020 katika ukumbi wa dar live mbagala.

      Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi mtendaji wa bendi hiyo Senior Bachelor alisema katika uzinduzi huo wameialika bendi ya mashauzi classic inayoongozwa na Isha mashauzi, seven survivor mnanda chini yake Baba Aminata, Segu segumbo mtaalam wa miondoko ya singeli, matarumbeta na burudani nyingi sana ambazo zitakufanya uendelee kuburudika kwa kila radha ya burudani.

Aliongeza kwa kusisitiza wadau na wapenzi wa taarab dar na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kwani kiingilio cha show hiyo ni cha kawaida sana shilingi 5000/= kwa mtu mmoja, show itaanza saa mbili usiku hadi majogoo. show itaongozwa na Mc Dokta kumbuka, Mc Jojoo na Maite Hassan mtangazaji wa kipindi cha taarab city redio fm ya dar es salaam.

Ijumaa, 18 Mei 2018

04:38

KHADIJA MBEGU CHIPUKIZI ANAE TINGISHA KWA SASA, JE UNAJUA ALIANZIA WAPI?.

Na pambe za taarab.

    Muziki wa taarab unazidi kushika kasi kwa sasa hususani baada ya kuendelea kuzaliwa bendi kadhaa ambazo nimekuja kuzidisha ushindani ambao ulionekana kupotea kipindi cha kati nazo ni first class inayoongozwa na Prince amigo, five stone iliyo chini ya Juma mkima, halichachi classic ambayo inaongozwa na Amour magulu na nyingi nyinginezo.

Jina la khadija mbegu au ukipenda unaweza kumuita "khadija kais" ni ingizo jipya kabisa katika tasnia hii, msichana huyu mwembamba mrefu kiasi na asiye na majivuno naweza kusema ni miongoni mwa wale waliojaaliwa vipaji vya kuimba na mwenyezimungu na anajua kutumia kipaji chake haswa akiwa stejini, mtandao huu ulimtafuta ili kupata mawili matatu tokea kwake na kwa bahati tulimkuta nyumbani kwao kwa wazazi wake mbagala jijini dar es salaam maeneo ya "kwa dumbalume" na mahojiano yalikuwa yalikuwa kama ifuatavyo:-

Pambe za taarab:- Habari yako khadija, sisi ni wandishi tokea mtandao bora wa taarab nchini tanzania, tunapenda kujua historia yako kimuziki maana wasomaji wetu wamekuwa wakihitaji sana kujua ni wapi umetokea maana wanaona umeibuka tu na kuanza kufahamika, ni wapi ulipoanzia mpaka kufikia hapo?.

Khadija mbegu:- Kwanza nianze kwa kuwashukuru kwa kunitafuta mpaka mmeweza kufika huku kwetu mbali kiasi hiki, mungu awabariki sana, mimi kiukweli sina muda mrefu katika muziki huu wa taarab, nilikuwa naupenda muziki huu toka zamani lakini sikuwaza kuwa ipo siku nitakuwa muimbaji kama hivi, ilikuwa siku moja nimeenda kusuka huku huku kwetu mbagala nikakutana na Salha abdallah yule aliekuwa mke wa hammer Q, sasa kuna wimbo ulikuwa ukiimbwa ktk redio nami nikawa naufuatisha aliponisikia akasema wewe msichana mbona unajua kuimba sana!, kwani unaimbia bendi gani? nikamjibu mimi nipo tu nyumbani wala siimbi popote, ndipo akaniambia kesho twende mazoezini kwetu wakaliwao modern taradance kwa thabit abdul akusikilize unaonekana una kipaji sana basi nami nikamjibu sawa haina shida.

Pambe za taarab:- Ekhe vipi sasa ulifanikiwa kwenda huko wakaliwao au uliingia mitini kwa hofu? funguka mama!.

Khadija mbegu:- Mwenzangu we acha tu!, nilienda ndugu yangu nilipofika thabit abdul akanipigia vyombo kwa mara ya kwanza nikaimba wimbo uitwao "fungu la kukosa" wa bendi hiyo hiyo wakaliwao. Aliponisikia akasema uwezo wangu bado ila niwe naenda mazoezini kila siku nitakuwa vizuri maana kipaji ninacho. Basi nikawa naenda mazoezini na siku zingine naenda mpaka katika show zao! Ila kuna siku sitoisahau tulikuwa tunafanya show pale magomeni maeneo ya mwembechai karibu na shekhe Yahya hussein, thabit alisema kuanzia siku hiyo nisipandishwe stejini wala nisiruhusiwe kuimba sababu sijui. Basi nikarudi nyumbani nikawa siendi tena nafanya issue zangu zingine tu hapa home.

Pambe za taarab:- Sasa ilikuwaje tena mpaka ukaibuka na kuanza kuwa maarufu wakati uliamua kukaa nyumbani khadija?.

Khadija mbegu:- Nakumbuka siku moja nilikutana na kaka kais mussa kais akaniuliza unaimbia bendi gani kwa sasa? nikamjibu kuwa nipo tu nyumbani sina bendi, akachukuwa simu yake hapo hapo akampigia mkurugenzi wa jahazi kolombwe Chollo akamwambia huyu khadija ni ndugu yangu mpokee na umpe kazi, basi hapo ndio ukawa mwanzo wa safari yangu ya mafanikio kiuimbaji. Nilikaa jahazi kolombwe kama miezi nane tu! nikawa vizuri haswa ndipo kaka kais mussa kais tena kwa mara ingine akanipeleka jahazi modern taarab yenyewe sasa baada ya wasanii wengine kuhama na mzee yusuph kuacha bendi.

Pambe za taarab:- Wakati unaenda jahazi modern taarab uliwakuta wasanii gani wakongwe? na vipi hukuhofia kwakuwa umeingia ktk bendi kubwa kuliko uliyotoka?.

Khadija mbegu:- Pale niliwakuta fatma Kasim, mwasiti kitoronto, Mishi zele, zubeda mlamali, Mossi suleiman na wengineo nakumbuka chipukizi nilikuwa peke yangu tu, nilipewa jukumu la kuimba nyimbo zote za fatma mcharuko ambae alikuwa amehamia yah tmk modern taarab, kiukweli nilizitendea haki nyimbo zile maana nilikuwa nikiziimba kama yeye mwenyewe haswaa! jambo ambalo liliniongezea umaarufu zaidi na jina langu kukuwa zaidi na zaidi. Nilianza kutafutwa na wandishi kwa mahojiano na interview mbalimbali za redio nilifanya za nchini na nje ya nchi.

Pambe za taarab:- Sawa sawa!, hapa kati tumepenyezewa ubuyu kwamba umeondoka jahazi modern taarab na unaonekana gusagusa min bendi huku pia ukionekana mazoezini kwa bendi mpya ya amigo first class modern taarab hapa ikoje?.

Khadija mbegu:- Ahsante sana kwa swali zuri sana ambalo nami pia napenda wapenzi na wadau wangu wajue, mimi ni msanii na bado nipo ktk kujifunza kama ambavyo nilikutana na Sada nassor akanipa ushauri. Nyimbo za zamani kama zilizoimbwa na akina fatma issa, malika, bi rukia na wengineo zina njia haswa za uimbaji na muimbaji bora wa taarab ni lazima aweze kuimba nyimbo zile, nami nilikuwa sizijui nikapelekwa gusagusa min bendi na kaka kais mussa kais ili nijifunze zaidi na nashukuru kwa sasa naziimba vizuri sana mpaka nimeshaanza kuwa na wapenzi pale gusagusa!, sasa pale first class nilizungumza na mkurugenzi wangu Hassan farouk akaniruhusu wala haina shida maana first class wanaimba taarab ya kisasa na gusagusa tunaimba old is gold ni vitu viwili tofauti kabisa!. Unajua watu siku zote wanapenda kuona mtu unaharibikiwa nasikia tayari wameanza kupandanisha maneno kwa viongozi wangu bila kujua nini kinaendelea na watu hao nawajua kwa majina sema sina muda wa kuwajibu nawaacha waendelee kuporojoka!.

Huyo ndie khadija mbegu au ukipenda muite khadija kais chipukizi mwenye ndoto ya kufika mbali kimafanikio ndani ya muziki huu wa taarab nchini tanzania, mtandao wa pambe za taarab tunamtakia mafanikio katika safari yake hiyo ya muziki na tunampa ushauri anatakiwa awe mvumilivu kwani sehemu yoyote yenye mafanikio mitihani ni kitu cha lazima inampasa apambane na amuombe mungu zaidi.

Jumapili, 4 Machi 2018

23:01

JE WAJUA KUWA SAKINA LYOKA WA CLOUDS TV NI MKE WA MTU KWA SASA?...SOMA HAPA!.

Na pambe za taarab.



SAKINA LYOKA AKIWA NA MUMEWE ABDILLAH WAKIFURAHIA TUKIO HILO ADHIMU.
Mtangazaji wa clouds televisheni kipindi cha ng'aring'ari Sakina lyoka amezungumza na mtandao huu na kusema kwamba anafurahia mno ndoa yake na mumewe Abdillah kwani naamini kwa sasa nimepata nilichokuwa nakitafuta kwa muda mrefu nasema ahsante mungu kwa kunipatia mume mwema.


Kuolewa sio ajabu ila kikubwa ni pale unapojaaliwa kumpata alie mwema katika ndoa yako nikimaanisha mume! alisema Sakina huku akimlalia mumewe miguuni kwa raha zao!, nae Abdillah kwa upande wake alisema Sakina ni mwanamke wa maisha yangu nilipiga goti kwa mungu aweze kunipa mke bora ambae tutaenda katika maisha na kweli amenipa Sakina wangu nampenda sana na naahidi kumtunza na nitamlinda kwa kila khali alisema Abdillah.


SAKINA LYOKA AKIMSHUKURU MUNGU KWA NDOA YAKE KUTIMIA.
Ndoa hii ambayo ilifungwa mwezi wa kumi na mbali mwaka jana na kumaliziwa na shetehe kubwa katika ukumbi uliopo mbezi, mtandao huu uliamua kumtembelea sakina LYOKA nyumbani kwako na kutaka kujua ni kwa kiasi gani anaona ndoa yake hiyo mpya tokea aolewe na huu utakuwa ndio utaratibu wa mtandao huu kutembelea ndoa za mastaa wetu ili kumfahamu je kunani?. Sisi tunampongeza Sakina pamoja na mumewe kwa maelewano mazuri na tunawatakia mafanikio makubwa katika ndoa yao.

Jumapili, 25 Februari 2018

20:45

KHADIJA KOPA ASEMA, KAPTEN TEMBA HANIDAI CHOCHOTE...SINA DENI NAE!.

Na pambe za taarab.


Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa jana jumapili akiwa ndani ya east africa redio na bibie Mwanne Othman mtangazaji wa kipindi cha taarab amejibu kiaina  shutuma zilizozagaa mitandaoni kwamba anadaiwa shilingi laki tatu za kitanzania na mtunzi wa mashairi Kapten temba mchaga wa kwanza kuimba taarab nchini.


Mkongwe huyo wa taarab nchini alisema kwamba sipendi kumzungumzia huyo mtu sababu naona kama nampa kiki kutajwa na mtu maarufu kama mimi ila naomba ieleweke kwa wapenzi na mashabiki zangu kwamba sidaiwi chochote na mtu huyo, sina shida ya mashairi, watunzi ninao kibao pia ndani kwangu nina mashairi mengi ambayo sijayaimba hivyo sina muda ya malumbano na mtu!, wacha aendelee kuandika tu huko mitandaoni ila nasisitiza tena sina deni na mtu huyo!, kama kuna sehemu tuliandikishiana deni hilo basi anaweza kwenda katika vyombo vya sheria nami nitakwenda kujibu hoja alisema mama huyo kwa kujiamini.


Takribani wiki tatu sasa mkurugenzi wa fungakazi modern taarab Kapten temba aliandika mitandaoni na kufanya mahojiano na vituo kadhaa vya redio hapa nchini akisisitiza kwamba anamdai khadija omary kopa shilingi laki tatu kama malipo ya mashairi yake manne ambayo alimuandikia malkia huyo katika album mpya ya ogopa kopa classic bendi. Na hayo ndio majibu ya malkia huyo kwamba hadaiwi chochote na temba!. "Chanzo tamtam za pwani east africa redio".


KHADIJA OMARY KOPA MALKIA WA MIPASHO NCHINI TANZANIA.
05:59

KIVURANDE JUNIOR "LIVE" NDANI YA SINDANO ZA MOTTO PAMBE ZA TAARAB WHATSAP GROUP JUMATATU.

Na pambe za taarab.


Ile segment pendwa inayowahusu wasanii wa taarab, kibao kata, segere, mduara, Baikoko na singeli iitwayo "sindano za motto" wiki hii Kivurande junior mfalme wa kibao kata ndio anawekwa kikaangoni na wanachama na wadau wa group hilo bora kabisa kwa sasa hapa nchini tanzania.


Akizungumza na mtandao huu admin msaidizi wa group hilo Aunty shija mwenye makazi yake dodoma nchini tanzania alisema kuwa Kivurande alipendekezwa na wanachama wa group hilo kuwa yeye ndio ahojiwe kwani wana maswali mengi sana dhidi yake ukizingatia kuwa yeye ndio mfalme wa kibao kata kwa sasa hapa nchini.
Nae Kivurande junior kwa upande wake alisema kuwa anawashukuru sana viongozi na wanachama wa group hilo la whatsap kwa kumpendekeza yeye kuhojiwa ndani ya group hilo, nimekuwa nikiiwania sana nafasi hii kwa muda mrefu sasa na nashukuru nimeipata kikubwa nawaahidi nitashirikiana nao vizuri kwa kujibu maswali yote na kamwe sitowaangusha alisema Kivurande junior.


Sindano za motto ni segment inayowahusu wasanii na kila siku ya jumatatu kuanzia saa moja kamili usiku ndio rasmi huanza hewani rasmi.


KIVURANDE JUNIOR AKIWA KATIKA POZI.

Jumatano, 21 Februari 2018

03:46

OMARY SOSHA MUIMBAJI TEGEMEO WA HALICHACHI CLASSIC MWENYE NDOTO

Na pambe za taarab.


Uimbaji ni kipaji changu nilichojaaliwa na mwenyezimungu, haya ni maneno ya Omary Sosha muimbaji tegemeo katika bendi ya halichachi classic yenye maskani yake magomeni jijini dar es salaam.


Omary ameanza kuimba kaswida madrasa maeneo ya tandika, hapo ndipo kipaji cha uimbaji kilipoanza kuonekana na mpaka sasa bado anasoma madrasa na kutunga kaswida kadhaa wa kadhaa ikiwemo na kuimba pia. Sosha katika safari yake ya muziki aliwahi kupitia Dar modern taarab ambapo alikutana na muimbaji mwenzie Twaha malovee ingawa hawakukaa sana, baada ya Omary kuondoka Dar modern alikuwa akiimba katika bendi mbalimbali za taarab zinazoimba old is gold taarab zikiwemo gusagusa min bendi, Raha original, Aljazeera pamoja na Kongamoyo.


Lakini baadae alienda washawasha modern taarab ambapo alikutana na director Amour magulu ambae walikuwa wote Dar modern, lakini kutokana na mgogoro wa kiuongozi bendi hiyo ilivunjika ndipo wakaanzisha bendi hii ya halichachi classic yeye akiwa ni mmoja wa waanzilishi wengine wakiwa ni Amour magulu, mwanahawa Chipolopolo, Amrani na wengineo.


Mtandao huu ulitaka kujua toka kwa Omary Sosha nini matarajio yake katika muziki huu wa taarab?, nae alijibu kuwa nina ndoto ya kuutangaza muziki huu kimataifa zaidi, unajua mimi naimba aina zote za taarab yaani old is gold na hii taarab ya kisasa, naamini nitafanikiwa kwani mwenendo wangu sio mbaya unanilidhisha maana nikiangalia nilipotoka mpaka hapa nilipo sio pabaya namshukuru mungu.


Pia tulitaka kujua ni changamoto gani ambazo huwa anakutana nazo katika safari yake ya muziki?, alijibu kuwa changamoto ni za kawaida na wakati mwingine haziepukiki unaweza kuandaa nyimbo au wimbo  kwa gharama kubwa lakini ajabu media zinakuwa hazikusapoti hii inarudisha nyuma sana juhudi zetu sisi wasanii ambao tunachipukia, ila kwa sasa kiasi media zimeanza kubadilika na zinacheza nyimbo zetu alisema Omary Sosha.
Huyu ni muimbaji tegemeo kwa taifa na halichachi classic modern taarab muite Omary Sosha!, mtandao huu unapenda kumpongeza kwa juhudi zake na tunamuasa asivunjike moyo kwani safari siku zote huwa na vikwazo na mitihani mingi kikubwa ni kugangamara na mungu atamfikisha pale anapopataka.


OMARY SOSHA AKIWA KWENYE POZI.

Jumanne, 20 Februari 2018

03:32

HASSAN VOCHA:- ABDALLAH FERESH NI ZAIDI YA MZAZI KWANGU!.

HASSAN VOCHA.
Na pambe za taarab.


Wakati said fellah ananitoa mkubwa na wanawe na kunipeleka pale G5 modern taarab kwake Hamisi slim sikutegeme kama siku moja nitakuja kukutana na Alhaji Feresh mtu muhimu kwangu ambae kwa kiasi kikubwa ni mzazi kwangu kwa maana amekuwa akinifanyia mengi sana ya kimaendeleo kama mwanawe.


Safari ya kimuziki ina mabonde na milima inatakiwa uwe mvumivu na busara ili uweze kufanikiwa, nilipofika pale G5 sikuwa mzoefu sana na muziki huu wa taarab isipokuwa kwakuwa nilikuwa muimbaji mzuri wa bongo fleva sikupata shida kuzoea mazingira haya. Kuna siku moja wakati nipo pale mazoezini G5 alikuja Adam mlamali huyu ni nguli wa muziki wa taarab ambae aliwahi kutamba na bendi za zanzibar stars na east african melody kipindi hicho, aliponiona nikiimba alivutiwa nami akaniomba ikiwezekana nijiunge dar modern mimi na msanii mwenzangu Hasna, nasi kwakuwa tulikuwa tuna nia ya kujifunza zaidi tulikubali nikiwa na mwenzangu Hasna.


Huo ndio ukawa mwanzo wa mimi kukutana na mkurugenzi wangu Alhaji Abdallah Feresh, tokea nimeanza kumfahamu nimekuwa ni mtu mwenye furaha kila siku kwani Feresh kwangu amekuwa ni kama mzazi haswa ukizingatia nimeondokewa na wazazi wangu hivyo amekuwa akinifariji sana na kunichukulia kama mtoto wake wa kunizaa! naweza kusema kuwa sijutii kumfahamu, amekuwa ni msaada mkubwa kwangu kuanzia kwenye sanaa mpaka katika maisha!, napenda nimpongeze Bosi wangu kwa kunijali na kutujali wasanii wote wa dar modern.


Mimi kwa upande wangu sifikilii kuhama dar es salaam modern taarab kwani hapa nakuwa kama nipo nyumbani, sina shida kabisa naishi kwa amani kabisa, kwa sasa muda na wakati wowote dar modern tutatoa nyimbo zetu mpya nami kuna kitu kipya kabisa nitakuja nacho hivyo wapenzi na wadau wangu wajiandae kwani mara zote huwa sibahatishi alimalizia kwa kusema Hassan vocha!.

Ijumaa, 16 Februari 2018

00:00

PILI AOGWA KUHOJIWA NDANI YA GROUP LA PAMBE ZA TAARAB JUMAMOSI HII.

Na pambe za taarab.


Mdau mkongwe aliewahi kutamba sana katika tasnia ya watuma salamu ndani ya redio mbalimbali na pia ametajwa katika nyimbo kadhaa za taarab nchini Pili aogwa au ukipenda muite mrembo wa kigamboni jumamosi ya wiki hii anatarajiwa kuhojiwa ndani ya group la pambe za taarab "wadau" kuanzia saa moja kamili usiku mpaka mbili kamili.


Segment ya kijamvi cha motto ndipo ambapo atahojiwa mdau huyo mpole na asie na makuu, akizungumza na admin Shija muwakilishi wa ma-admin tokea mkoani dodoma Pili aogwa alisema kwanza amefurahi kupata nafasi hiyo adhimu na muhimu kwake ili kuwajulisha wadau wachanga nini maana halisi ya udau, na ni kwa vipi alifanikiwa kufahamika mpaka kupata heshima mbalimbali tokea kwa watangazaji wa taarab na wasanii mbalimbali hapa nchini.


Mtandao huu wa pambe za taarab una vyanzo vyake vya habari mbalimbali likiwemo hili group la wadau wa muziki wa taarab, group la watangazaji wa taarab nchini, magroup mbalimbali ya facebook kama kashda na raha za pwani, ubuyu wa taarab. Pages Pambe za taarab na nyinginezo.


PILI AOGWA AKIWA KATIKA BIASHARA ZAKE.