TANGAZA NASI

Breaking

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tetesi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tetesi. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 28 Desemba 2017

03:27

TETESI:- PRINCE AMIGO KUJIUNGA RASMI NA YAH TMK MODERN TAARAB SIKU YA BIRTHDAY YA BENDI.

Na pambe za taarab.

Muimbaji machachali prince amigo unatarajia rasmi kujiunga na bendi ya yah tmk modern taarab katika sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bendi hiyo ambayo itafanyika hivi karibuni hapa hapa jijini dar es salaam.

Akizungumza na mtandao huu makini wa pambe za taarab meneja wa bendi ya yah tmk modern taarab Said kessy alisema kwamba tayari tumeshafanya mazungumzo ya awali na prince amigo na tulipofikia kunaleta matumaini naamini kwa uwezo wa mungu tutamalizana nae kila kitu alichokuwa akikihitaji kabla ya sherehe yetu ya kuadhimisha birthday ya bendi.

Mtandao huu ulinyanyua simu na kumpigia prince amigo na kumuulizia juu ya issue hii ambapo alisema ni kweli viongozi wa yah tmk modern taarab walinifuata na kuniomba nijiunge na bendi yao na kuna baadhi ya mambo niliwaambia wanikamilishie ila mpaka sasa bado hamna chochote vijana wanasema ni sound tu!, mimi nina matarajio yangu brother nahitaji kuwa na bendi yangu mwenyewe mungu akijaalia so! muziki ni kazi yangu nafikili mpaka mwakani nitakuwa na la kusema zaidi tuombe uzima alimaliza kusema prince amigo.

Mtandao huu unawaahidi wasomaji wetu kuwa tutakuwa katika sherehe za birthday ya bendi hiyo ili kuona je ni kweli prince amigo atatangazwa kujiunga na yah tmk modern taarab ama lah!.

Jumatano, 27 Desemba 2017

20:22

TETESI:- JEURI YA FEDHA, WASANII WAWILI NGULI WA YAH TMK KUTIMKIA JAHAZI MODERN TAARAB?.

Na pambe za taarab.

Waswahili wanasema siku zote mwenye kisu kikali ndie mla nyama, kuna habari za kunyapianyapia zimetufikia kwamba jahazi modern taarab baada ya kuundwa bodi ya wakurugenzi imepania kuchukuwa msanii yeyote wanaemtaka na jeuri hiyo wanayo maana zimetengwa pesa zaidi ya milioni 30 maalum kwa kuiboresha bendi hiyo.

Mnyetishaji wetu aliendelea kumwaga unyunyu kuwa pale yah tmk modern taarab kuna wasanii wawili maarufu ambao wapo katika mazungumzo ya mwisho mwisho na matajiri hao wa jahazi modern taarab ambao wameamua kuja kuleta mapinduzi ya kweli katika muziki huu wa taarab nchini Tanzania na mambo yakisha kamilika watu wataacha midomo wazi kwa kushikwa na butwaa!.

Hawa mabosi wa jahazi modern taarab kwa pesa ambayo wamepanga kuwapatia wasanii wale wa yah tmk taarab ni vigumu kwa mtu mwenye akili timamu kuikataa hususani kipindi hiki ambapo karibia bendi zote zimekuwa zikilia ukata wa fedha kuwaandama alisema ripota wetu huyo.

Mtandao huu unayo majina ya wasanii hao nguli lakini ni mapema sana kuyaanika ni Sawa sawa na kuharibu usajili wa Dornad ngoma kutoka yanga kwenda simba! jambo kubwa lililo mbele yetu ni kusubili ili tuone nguvu waliyonayo matajiri hao wa jahazi modern taarab je ni kweli au tisha toto tu?...hiyo ndio taarab ya kisasa msanii unanunuliwa kwa fedha nyingi kama mcheza mpira wa miguu.

Jumatatu, 18 Septemba 2017

05:23

TETESI:- MWINYIMKUU NA MAINA THADEI WAACHANA KWA TALAKA?.

Na pambe za taarab.

Khali ya sintofahamu katika ndoa ya Mwinyimkuu na Maina thadei imezua utata baada ya kuzagaa taarifa kwamba wawili hao kwa sasa hawapo tena ndoani!, habari hii iliyoshtua wapenzi na wadau wa muziki wa taarab ilipofika katika dawati la habari la mtandao huu ulianza kufanya juhudi za kuwatafuta wana ndoa hawa ambao kwa sasa wanaishi zanzibar.

Tulianza kwa kuzungumza na Maina thadei ambae kwanza alipoambiwa kuwa habari zao zimefika katika mtandao wetu alishtuka sana!, lakini kwa upande wake Maina alisema ni kweli kwa sasa wana matatizo na mume wake ambayo yamepelekea kutozungumza na kuishi mbalimbali lakini mpaka sasa bado hajapewa talaka ina maana ni wanandoa!, unajua ndugu mwandishi, mimi mara nyingi huwa sipendi kuweka hadharani mambo yangu binafsi hivyo sina la zaidi ktk kukueleza hili na sipo tayari kumpa mtu kiki bila ya sababu ya msingi alimaliza kwa kusema.

Tulipomtafuta Mwinyimkuu ili nae aseme chochote juu ya issue hii, alisema:- Maina bado mke wangu mpaka sasa na wala hatuna tatizo lolote lile na kama unasema Maina amesema sisi tuna matatizo ktk ndoa yetu basi hilo mimi silijui ninavyofahamu tupo sawa tu!, alipoulizwa imekuwaje ukafuta picha zote ambazo unaonekana upo beneti na Maina ktk account zako zote mitandaoni? alisema huu ni uamuzi tu na yeyote anaweza kufanya hivyo kama ana picha nyingi ambazo ameplan kuziweka tena ndivyo pia ilivyo kwangu mimi. Watu wanaongea sana juu yetu lakini niwaambie tu kama itafikia sisi kuachana basi tutaweka wazi tu wala haina shida ndugu mwandishi alimaliza kwa kusema Mwinyimkuu.

Mtandao huu haukuridhika na majibu ya wawili hao ndipo alipotafutwa rafiki wa karibu wa wawili hawa ambae wanaishi nae huko zanzibar na kumuuliza juu ya issue hii nae alianza kuzungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake! hawa jamaa kwa sasa sio mke na mume tena kwa kifupi wameshaachana kabisa kwa talaka isipokuwa wenyewe wanaficha ila Maina yupo kivyake na Mwinyimkuu yupo kivyake ndoa imeshavunjika kabisa. Mwinyimkuu na Maina thadei ni wasanii wa muziki huu wa taarab ambao walioana na kuvuta hisia za wadau, wapenzi na mashabiki wa tasnia hii ambao walikuwa wakiwapenda sana! kwa sasa wawili hao wamehamishia shughuli zao visiwani zanzibar, Mwinyimkuu akiwa katika bendi ya wajelajela ambapo inasemekana anatoka kimapenzi na muimbaji machachari Husna Hassan chitoto nae Maina anafanya show katika mahotel mbalimbali ya kitalii visiwani humo.

Jumatano, 9 Agosti 2017

01:42

CHIPUKIZI WA JAHAZI KHADIJA MBEGU ANAWANIWA NA BENDI MBILI KUBWA ZA TAARAB NCHINI....

Na pambe za taarab.

Muimbaji chipukizi ambae anafanya vizuri kwa sasa katika bendi ya Jahazi modern taarab khadija mbegu yupo katika kuwindwa na bendi mbili kubwa za taarab nchini na hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa alionao pindi anapokuwa stejini.

Bendi hizo mbili ambazo zote zinapiga muziki wa "gate collection" kiingilio pesa!, kwa nyakati tofauti zimeonekana zikimsaka khadija mbegu bila mafanikio na hii ni kuhofia viongozi wa Jahazi wasije wakawashitukia. Unajua kwa sasa yule msichana anafanya vizuri sana naamini kama nitampata bendi yangu itakuwa imepata kifaa cha nguvu mno, tatizo lililopo mwenyewe anaonekana ana mapenzi makubwa sana na bendi hii ya jahazi modern taarab, sio kama siwaoni wengine hapana ila uwezo wa kuimba na kucheza kwa msichana huyu ndio ushawishi mkubwa kwangu...namuhitaji sana kiukweli alisikika kiongozi huyo.

Mtandao huu unazijua bendi hizo ila ni mapema sana kuzitaja kwa sasa, tulimtafuta khadija mbegu mwenyewe na kumuuliza je tayari amepata taarifa hizi za yeye kutakiwa na bendi mbili kubwa? Na khadija alijibu kuwa hana taarifa hizo ndio kwanza anasikia, na hata kama hizo bendi zitamfuata jibu lake ni kwamba hana mpango wa kuihama jahazi modern taarab sababu kwanza ana mapenzi ya dhati na bendi hii na vile vile hana tabia ya kuhamahama bendi. Napenda niwatoe wasiwasi viongozi wangu, wasanii wenzangu na mashabiki wa jahazi kwamba sina mpango wa kuhama na wala sitarajii kamwe...mimi ni jahazi damu alimaliza kusema huku akicheka.

Jumapili, 30 Julai 2017

08:22

TETESI:- WAIMBAJI WATATU WA OGOPA KOPA WAHISIWA KUTIMKA.......

Na pambe za taarab.

Bendi ya ogopa kopa classic inayomilikwa na malkia wa mipasho nchini khadija omary kopa inasemekana imekimbiwa na waimbaji wake watatu mahiri nao ni Mwamvita shaibu na Zena mohamedy ambao wanaonekana zanzibar stars na Naima mohamedy ambae anaonekana katika jukwaa la   jahazi modern taarab.

Kachero wetu alifanya mahojiano na kiongozi mmoja wa jahazi modern taarab ambae hakupenda kuwekwa wazi jin lake kwa kisingizio yeye sio msemaji wa bendi, kiongozi huyo alisema kuwa Naima mohamedy kwa sasa ni muimbaji wetu na yupo katika ratiba za kupewa wimbo mpya ndani ya bendi hii.

Kwa upande wa Mwamvita shaibu na Zena mohamedy wenyewe wamekuwa wakifichaficha kwa kusema kwamba wamekuwa wakienda katika show za zanzibar stars kwakuwa bendi yao ya ogopa kopa haina show kwa sasa na ukizingatia wao ni wasanii waandamizi wa iliyokuwa zanzibar stars kipindi hicho hivyo hawaoni ubaya kushiriki maonyesho yao. Habari zaidi za kiuchunguzi zinasema wasanii hao wamechukizwa baada ya kutegemea siku ya sikukuu ya Idd bendi ingesafiri kwenda mombasa kenya lakini matokeo yake ikawa kinyume na wasanii hawakusafiri.

Juhudi za kumtafuta mkurugenzi wa bendi hii malkia khadija omary kopa ili azungumzie sintofahamu hii zinaendelea, kikubwa tunawaomba wasomaji wetu tuendelee kuwa pamoja kwani mama mukubwa tutamtafuta athibitishe hili kwa kina zaidi.

Jumanne, 11 Julai 2017

02:26

YOUNG HASSAN ALLY:- THAMANI YANGU KWENYE MUZIKI WA TAARAB NI ZAIDI YA MESSI.

Na pambe za taarab.

Muimbaji wa ogopa kopa classic bendi young hassan ally au "mzee wa ngenga" amejinasibu kwa kusema thamani yake katika muziki huu wa taarab ni zaidi ya messi wa Barcelona.

      Aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa mtandao huu kwamba je yupo tayari kuihama ogopa kopa na kwenda bendi ingine? kulingana na kauli zinazozagaa kwamba hassan ally anatakiwa na zanzibar stars modern taarab. Unajua ndugu mwandishi thamani yangu mimi ni zaidi ya messi wa Barcelona hivyo hakuna wa kuweza kunilipa.

   Nitaendelea kubakia hapa ogopa kopa labda nikitoka hapa nikaanzishe cha kwangu mwenyewe sitaki kuajiliwa tena, nina ndoto zangu na naamini zitatimia kwakuwa naona muelekeo sio mbaya namshukuru mungu.

     Habari zinazo endelea kuzagaa miongoni mwa wadau wa muziki huu wa taarab nchini ni kuwa hassan ally anatakiwa zanzibar stars kwenda kuongeza nguvu baada ya kuonekana anaweza kuwa msaada mkubwa maana hassan anaimba, anatunga mashairi na pia anatunga muziki.

Jumamosi, 8 Julai 2017

02:25

TETESI:- KHADIJA YUSUPH ATAMANI KUREJEA JAHAZI MODERN TAARAB.

Na pambe za taarab.

      Muimbaji tegemezi wa bendi ya wakaliwao modern taradance khadija Yusuph au sauti ya chiriku, inasemekana tayari ameanza mchakato wa kuomba kurejea tena katika bendi ya jahazi modern taarab.

     Infoma wa kutegemewa wa mtandao huu wa pambe za taarab alizinyaka habari za chini ya kapeti toka kwa msiri mkubwa wa khadija Yusuph bila kujua kuwa huyo anaemueleza ni mwandishi wa mtandao huu. Unajua kwa sasa khadija yusuph hana maelewano mazuri na wakaliwao takribani show nne au tano mpaka sasa hajajitokeza alianza kwa kusema jamaa huyo.

      Khadija alipoona mambo yanazidi kwenda ndivyo sivyo baina yake na uongozi wa wakaliwao akaanza kumuomba rafiki mmoja aende akazungumze na uongozi wa jahazi modern taarab kwamba yupo tayari kurejea buree bila pesa yoyote ili mradi tu nae awe kundini.

    Mtandao huu utaendelea kufuatilia tetesi hizi ambazo bado hazijawa rasmi ili kubaini ukweli wa jambo hili uko vipi?, ikumbukwe kwa sasa khadija yusuph anaonekana sana katika show za zanzibar star's modern taarab huku akishindwa kuhudhuria show kadhaa za wakaliwao modern taradance.