TANGAZA NASI

Breaking

Jumanne, 31 Mei 2016

18:20

PRINCE AMIGO:- MKE WANGU HABIBA SI MKOROFI KAMA INAVYOSEMEKANA MIDOMONI MWA WATU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


PRINCE AMIGO AKIWAJIBIKA STEJI SAMBAMBA NA WACHEZA SHOW WA JAHAZI.

         Kwanza kabisa napenda niwaombe radhi wapenzi wasomaji wa blog hii bora ya ubuyu wa taarab kwa kuchelewa kuwaletea kikaango hiki kilichokuwa kikimuhusu prince amigo wa jahazi modern taarab na hii ni kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu ila leo nawaletea mfululizo huu wa maswali na majibu kama ifuatavyo:- 


 SALMA WA MAISHA FM DODOMA:- Amigo napenda kujua safari yako ya muziki wa taarab ulianza lini, na je ni nini siri ya mafanikio yako katika bendi ya jahazi modern taraab maana una muda mrefu licha baadhi ya wasanii kuhamahama bendi.


PRINCE AMIGO:- Safari yangu ya muziki wa taarab ilianza mwaka 2007 na kuhusu mafanikio niliyoyapata sihaba mpaka sasa najenga na pia nina usafiri wangu binafsi na maisha yangu mazuri tu namshukuru mwenyezimungu.


HOTIE GENERATION FM MBEYA:- Wewe kama msanii wa taarab unazungumziaje suala la wasanii kudharau wito wa watangazaji wa mikoani katika kufanya interview?.


 PRINCE AMIGO:- Ahsante sana bibie hotie, kwa mimi binafsi sina hiyo tabia pale ninapohitajika huwa nafika kwa wakati, na mimi namilikiwa kwahiyo naamlishwa tu na viongozi, kuhusu wasanii wengine kiukweli sijui, labda wengine wanafika huko mikoani wamechoka wanahitaji walale kidogo ili usiku waingie katika show nahisi hiyo ndio sababu ila kama wanakuwa na sababu tofauti mimi sijui.


NADYA BOMBA FM ZNZ:- Skendo zinasaidia kumpushi msanii kijina, kwa upande wako wewe skendo unazikubali kama ndio ni kwanini na kama hapana ni kwanini?.


 PRINCE AMIGO:- Aaah! kwangu mimi skendo sina, na kwanza haziwezi kunisaidia chochote sana sana zitaniharibia tu kwasababu kwanza ni kijana ambae natafuta maisha kwa njia kubwa ya kufika mbali alafu leo hii skendo za kijinga sio nzuri, kwangu mimi skendo haziwezi kunisaidia maana hazina faida, mimi kwangu kazi tu ndio ambayo inanisaidia.


 MC CHINGA DODOMA FM:- Inasemekana umetengana na mke wako mkubwa mama man je ni kweli? na pia kuna tetesi kuwa unampenda sana mke mdogo sababu ana pesa na kichokufanya umrudie mke mdogo ni nini?.


  PRINCE AMIGO:- Aaah! ni kweli nimemuacha mke mkubwa na sijarudiana na mke mdogo eti sababu ana pesa, mapenzi ni kupendana mioyoni na wala mapenzi sio pesa, kama ingekuwa ni pesa basi naamini nisingeweza kumuacha kwanza alafu nikamrudia, nilimuacha nikamfundisha na atambue kuwa mume wake nahitaji hiki na hiki na nilipomrudia ni sababu ya mapenzi na nyota yake na yangu zilikuwa zinaendana, na mku mkubwa nimemuacha kwasababu zangu mwenyewe binafsi na ni ngumu sana mtu mwingine kufahamu.


  SHUFAA KAYA FM BAGAMOYO:- Amigo, kuna tetesi kuwa mke mdogo ni mkorofi sana na amekuwa akimrusha roho mama man kila walipokuwa wakikutana, wewe kama mume ulikuwa unachukuwa hatua gani kwa tabia hii ya mke mdogo?.


 PRINCE AMIGO:- Bibie shufaa, kwa sasa nina mke mmoja tu anaitwa habiba ama zuu kama anavyofahamika mitandaoni, na hilo suala kwamba walikuwa wakikutana na kurushana roho ilikuwa kipindi hiko sana wakati nipo nao wote wawili lakini baada ya kumuacha mmoja na yule mwingine alitulia kwahiyo sikweli kwamba mke wangu huyu ni mkorofi au eti akikutana na mwenzie anamrusha roho hapana, wanawake mnajitambua jinsi mlivyo shufaa! kifupi mke wangu mdogo hana tatizo kabisa.


 FORTNA CG FM TABORA:- Prince amigo napenda kujua toka kwako mpaka sasa ni ndoa ngapi umeoa na umeacha ndoa ngapi na kwanini?.


 PRINCE AMIGO:- Mimi nilikuwa na ndoa mbili nimeacha ndoa moja na nimebaki na ndoa moja na ukiniuliza sababu ya kwanini hilo ni suala langu mimi mwenyewe binafsi ni vigumu kuliweka wazi.


 MWAJUMA RAS FM DODOMA:- Amigo una mikakati gani katika kujiendeleza kimuziki nje ya bendi yako ya jahazi modern taarab?.


  PRINCE AMIGO:- Suala la kujiendeleza kimuziki nje ya bendi yangu ya jahazi modern taarab, sijalipa nafasi ya kuliongelea sana ila naamini ni hivi karibuni tu wapenzi watafahamu mimi ni kitu gani ninachofanya, lakini kwa sasa nafuata kile ninachoambiwa kufanya ndani ya kampuni ya jahazi entertainment, mimi ni mwanamuziki ambae nina nidhamu kubwa sana wala sio mtu wa kukurupuka ovyo! ila nina plani kubwa sana ya kufanya kazi kubwa sana nje ya jahazi modern taarab lakini kwa sasa sijafikilia kufanya.


 AISHA WA BARMEDA'S TV MWANZA:- Mie nataka kujua kuna taarifa kwamba gari unayotembelea ni mali ya bi mdogo habiba, na kwake umefuata pesa sio mapenzi je swala hili ni kweli amigo?.


 PRINCE AMIGO:- Unajua siku zote anaejua siri ya mwenzie ni moyo wa mwenzie kwahiyo mara nyingi ukiruhusu kusikiliza sikio lako likasikia kila kitu basi mimi naamini unaweza kuja kusikia taarifa ukajakufa kwa presha katika kipindi unachotangaza bibie aisha, hayo yanayoongeleka yanaongeleka tu ila unatakiwa utambue kuwa mimi nafanya kitu gani katika maisha mimi ni mwanamuziki ambae ni mkubwa na najiamini kwenye hilo kwahiyo siwezi kusema mengine zaidi ila yoyote yanayoendelea katika maisha yangu ni maendeleo yangu mwenyewe binafsi na maisha yangu ninayoishi sasa hivi kila kitu kina chanzo na chanzo kinakuwa kina mmoja kwahiyo kupata kwangu mimi kuna mwingine nyuma yangu kwahiyo kila mafanikio yangu yana mtu nyuma kama ni mke kama ni bosi kama ni wafanyakazi wenzangu kama ni mama kama ni baba lakini yote ni maisha yangu mimi.


 EDNA WA AFM DODOMA:- Amigo kwanini ukija dodoma huzunguki redio nyingi kama wasanii wengine hii ni mara ya pili nimejaribu kutaka kufanya interview na wewe unaniambia upo bize ni kwamba unaenda kwa uliowazoea au inakuwa vipi au kukupata mpaka tuandike barua na takrima?.

 

 PRINCE AMIGO:- Bibie edna hujawahi kuniambia mimi hata siku moja, na nikifika dodoma huwa kwa niaba yaani tupo kikampuni zaidi kwahiyo sisi huwa tunaambiwa tunatakiwa tukafanye interview redio flani siwezi kukurupuka eti nizunguke redio zote inawezekana kweli! labda edna ulimpigia amigo mwingine sio amigo mimi.

 

       Jamani maswali yalikuwa mengi sana ila kwa leo naomba niishie hapa maana amigo alikuwa katika wakati mgumu mno kujibu maswali ambayo yalikuwa yakimiminika kama mvua, ila napenda nimpongeze sana amigo kwa ushirikiano mkubwa ambao aliuonyesha siku ile...tupo pamoja sana!.

16:36

WAKALIWAO MODERN TARADANCE KUINGIA STUDIO ALHAMISI YA TAREHE 2/6/2016 KUREKODI NYIMBO 2 MPYA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


          Bendi yako uipendayo ya wakaliwao modern taradance chini yake mkombozi thabit abdul siku ya alhamisi wanatarajia kuingia studio soundcrafters kwa producer bora enrico temeke jijini dar es salaam kurekodi nyimbo mbili mpya.


         Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo thabit abdul alisema kuwa ameamua kurekodi nyimbo zingine mbili baada ya msanii wake hamuyawezi kondo kurejea kundini na pia ikumbukwe salha abdallah hakuwa na wimbo mpya kwahiyo hii ni nafasi yake kuonyesha uwezo wake katika uimbaji, alizitaja nyimbo hizo ambazo wanatarajia kwenda kuzirekodi na majina ya waimbaji kuwa ni chozi langu utalilipa utakaorekodiwa na salha abdallah na wimbo wa pili unaitwa mchawi ndugu ambao utaimbwa na hamuyawezi kondo, aliendelea kuzungumza kuwa ukimya wa muda mrefu wa wakaliwao modern taradance sasa wameupatia jibu.


      Mtandao huu wa ubuyu wa taarab unawatakia mafanikio bendi ya wakaliwao katika harakati zake za kuhakikisha tasnia hii inasonga mbele kwa kutoa vibao vikali kama ilivyo kawaida yao.

02:30

JOKHA KASSIM:- MAPROMOTA WAMEKUWA SI WAAMINIFU, WAMENITAPELI SANA PESA ZANGU IPO SIKU NITAWATAJA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


JOKHA KASSIM AKIFANYA YAKE STEJINI.

        Jokha kassim mamaa wa domo la udaku wimbo ambao unaendelea kufanya vizuri kupitia media mbalimbali hapa nchini tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi hii, amezungumza na mtandao huu kwa njia ya simu na kufunguka juu ya mapromota ambao wamekuwa wakichukua show huko mikoani na kuwadhurumu.


       Aliyasema haya baada ya kutupiwa swali kuhusu pesa ambazo jokha kassim ilisemekana ametapeli huko kilosa baada ya kupatiwa advance ya show na yeye kutotokea kabisa jambo lililopelekea promota huyo kumchafua sana jokha kassim mitandaoni akilalama kwa kile alichofanyiwa na msanii huyo. Akijibu tuhuma hizo jokha kassim alisema kwamba ni kweli nilitumiwa pesa na huyo kaka lakini nami nilipatwa na tatizo la ghafla mwanangu alirudishwa toka shuleni anaposoma maana yupo bording na kufikishwa moja kwa moja muhimbili maana alikuwa ana homa kali sana na alilazwa pale, sasa mimi kama mzazi naanzaje kusafiri katika show kilosa katika mazingira kama hayo? alihoji jokha kassim.


       Ila baadae nilizungumza na yule promota na kumuahidi kumlipa pesa yake ambayo alinitumia, ila hawa mapromota ni watu wabaya sana kwani mimi nimeshatapeliwa sana huko mikoani, mtu anakuita katika show ukifika mnafanya show lakini inapokwenda kinyume na matarajio yake anakukimbia na kukuacha solemba! mimi yameshanitokea sana huko mikoani lakini nanyamaza tu ila naahidi ipo siku nitawaanika wale wote ambao walinitapeli na kuniingiza mjini, wasinione mimi mjinga kunyamaza kimya!, siku hizi nimejifunza kutokana na makosa, promota anaponihitaji mimi basi anatakiwa kunilipa asilimia 80% ya tulichopatana alafu baadae kilichobakia tutalipana nitakapofika huko maana nimechoka kutapeliwa kusema kweli alimaliza kwa kusema jokha kassim.

01:48

TAZAMA PICHA "13" ZA SHEREHE YA HARUSI YA SAID MITUTU MSANII WA COAST MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.

         Msanii wa bendi ya coast modern taarab said mitutu siku ya jumapili alifunga ndoa na zainab juma maeneo ya mtoni jijini dar es salaam na kufuatiwa n sherehe kubwa ya kukata na shoka iliyofanyika katika ukumbi wa ikweta grill siku ya jumatatu, zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopatikana katika sherehe hiyo!.

SAID MITUTU AKIWA NA MKEWE ZAINAB JUMA

SAID MITUTU NA MKEWE WAKIJIANDAA KUKATA KEKI.

KEKI MFANO WA GITA IKIWEKWA MEZANI KWA HESHIMA ZOTE.

SAID MITUTU NA MKEWE ZAINAB JUMA WAKICHEZA MUZIKI WA TAARAB.

SAID MITUTU NA MKEWE ZAINAB JUMA WAKIMSIKILIZA MC WA SHUGHULI.

ZAINAB JUMA NA MUMEWE SAID MITUTU WAKIITAZAMA KEKI KWA FURAHA KUBWA.

SAIDI MITUTU NA MKEWE WAKIWA NA WATU WAO WA KARIBU.

BINTI WA SAID MITUTU MWANA-ASHA AKIFURAHIA NDOA YA BABA YAKE.

MC WA SHUGHULLI MKUBWA DAWA AKIELEKEZA MAHARUSI NINI CHA KUFANYA.

ZAINAB JUMA NA MUMEWE SAID MITUTU WAKIKUMBATIANA KWA FURAHA KUBWA.

ILIKUWA NI FURAHA KUBWA KWA WANANDOA HAWA SIKU YA JANA.

SAID MITUTU NA MKEWE ZAINAB JUMA WAKIWA KATIKA RED CAPET.

ALLY J AKIFUNGUA SHAMPENI KWA MADAHA NA MBWEMBWE NYINGI.

Jumatatu, 30 Mei 2016

17:37

HIVI UNAJUA NI SABABU IPI ILIYOPELEKEA HUYU JAMAA AKAITWA ALLY JEULI?...ISOME HABARI HII HAPA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

ALLY J MKURUGENZI WA FIVE STAR'S MODERN TAARAB.

         Unapolitaja jina la Ally J katika tasnia hii ya taarab hapa nchini juwa wazi umetaja mtu muhimu sana tena nguli wa muziki huu tanzania, hivi unajua sababu iliyopelekea akaitwa Ally jeuli na wadau wa muziki huu?.

 

        Ilikuwa ni siku ya jumatatu ya tarehe 30/05/2016 pale katika ukumbi wa ikweta grill mtoni kwa azizi ally jijini dar es salaam ndipo nilipokutana na Ally J akiwa ni mmoja wa waliohudhulia sherehe ya ndoa ya msanii wa coast modern taarab aitwae said mitutu ambae amemuoa binti aitwae zainab juma, pamoja na mambo mengi tuliyoongea lakini lililonifurahisha ni hili la yeye kupewa jina la Ally jeuli na wadau wa muziki huu.

 

       Alianza kwa kusema kuwa unajua kais, mimi ally J, sio mtu wa kuburuzwa na wamiliki wa bendi mbalimbali za taarab hapa nchini watu wamenipa jina la ally jeuli sababu mimi sio mtu wa kuitikia tu kila ninaloambiwa na hawa wanaojiita wakurugenzi wa bendi, mimi huwa nakuwa na misimamo yangu ambayo nataka ifuatwe lakini kiongozi anapokwenda kinyume na kile tulichokubaliana ndipo linapopatikana jina la "jeuli".

 

         Kwa mfano unaweza kukuta tupo katika bendi kwa pamoja tunatengeneza wimbo mpya lakini ajabu wimbo unapotoka utakuta katika albam inaandikwa mtunzi fulani, muziki kaweka fulani huku ukichunguza kwa undani utakuta muziki labda nimeweka mimi ally j na utunzi wala sio wa huyo aliejiandika hapo kwenye kava, lakini kwakuwa yeye ni mkurugenzi basi anatumia mabavu kuandika tu! mimi siwezi kukubali jambo kama hili na nimekuwa nikilumbana sana na wamiliki wa mabendi kipindi hiko cha nyuma enzi za kutumwa, hivi ukiandika muziki huu kuweka ally j labda itakuwa umeharibu au? alihoji ally j.

 

        Hii ni moja ya sababu ya mimi kupewa jina hilo na viongozi pamoja na wadau wa muziki huu hapa nchini, issue ni misimamo yangu mikali tu wala sio kitu kingine, lakini hivi karibuni nitatoa tamko langu rasmi juu ya muziki wa taarab na mimi ally j alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyu wa five stars modern taarab.

Alhamisi, 26 Mei 2016

16:21

USIKOSE SHOW KABAMBE YA VUNJA JUNGU TOKA KWA TOT TAARAB NA TOT DANSI.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MALKIA WA MIPASHO NCHINI KHADIJA OMARY KOPA.

       Bendi yako uipendayo ya t.o.t. taarab chini yake khadija omary kopa wakiwa sambamba na t.o.t. bendi wana achimenengule watashusha burudani ya nguvu ndani ya ukumbi wao wa nyumbani c.c.m. mwinyijuma siku ya vunja jungu yaani tarehe 3/6/2016, kumbuka huo utakuwa ni usiku wa vunja mungu show, kiingilio mlangoni itakuwa ni shilingi elfu tano tu za kitanzania.


     Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi hiyo Gasper tumaini alisema kuwa ameamua kurudisha fadhira kwa wakazi wa mwananyamala na vitongoji vyake maana wamekuwa wakiwaunga mkono katika nyanja zote akimaanisha bendi ya dansi, kwaya pamoja na taarab, siku hiyo tunatarajia kutambulisha nyimbo zetu mpya kabisa za taarab pamoja na dansi vile vile tutatambulisha wasanii wetu wapya kabisa ambao wamejiunga nasi kwa upande wa taarab na dansi, kwakweli nawaasa wadau na mapenzi wa t.o.t. kuwa hii si show ya kukosa nawaomba wajitokeze kwa wingi waje wawaone vijana wao alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo.


       Bendi hii ya t.o.t. kwa sasa imesukwa upya na ina kikosi imara kilichosheni wakongwe kama ally star, abdul misambano, khadija kopa, J.j. mzee wa mbezi bila kumsahau mohamedy mbange ambae ndie director kwa sasa, wakongwe hawa ukiwajumuisha na damu changa unapata t.o.t. iliyo tayari kwa kazi muda na wakati wowote, kubwa wadau tujitokeze katika show yao hii ya vunja jungu ambayo itafanyika c.c.m. minyijuma mwananyamala A jijini dar.


Ijumaa, 20 Mei 2016

18:47

TAZAMA PICHA "8" JINSI KHADIJA KOPA NA MSAGASUMU WALIVYOTIKISA BUGURUNI NA VITONGOJI VYAKE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Siku ya jana ijumaa ndani ya ukumbi wa lekham hotel buguruni bendi yako ya ogopa kopa classic wakishirikiana na msagasumu Rais wa uswazi walifanya mambo makubwa sana kwa kupiga show ya pamoja na ya nguvu sana iliyopelekea washabiki kubaki midomo wazi wasiamini kinachoendelea na kuomba onesho hilo lirudiwe tene siku ingine, zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo zilipatikana katika onyesho hilo.


KHADIJA OMARY KOPA NA MSAGASUMU WAKICHEZA STYLE YA CHEZA JIANGALIE.


MSAGASUMU KABALI YAO AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI.

HANIFA MAULID 'JIKE LA CHUI" AKICHEZA KWA UMAHILI MBELE KHADIJA KOPA!.


WAIMBAJI WA OGOPA KOPA WAKICHEZA STYLE YA CHEZA JIANGALIE!.


KAMONGO MR BEAN AKIPAPASA KINANDA KWAUFUNDI MKUBWA.



FUNDI MITAMBO DIKA SOJA AKIFANYA YAKE.


JORDAN SOLLO AKIPAPASA CHOMBO CHAKE KWA UMAKINI MKUBWA.


HANIFA MAULID NA KHADIJA KOPA WAKIWA STEJINI.


17:57

ALJAZEERA OLD & MODERN TAARAB KUFANYA YAO NDANI YA UKUMBI WA D.D.C. KARIAKOO LEO JUMAMOSI...USIKOSE!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


        Wale mabingwa wa taarab asilia kwa sasa hapa jijini dar es salaam aljazeera old & modern taarab siku ya leo jumamosi watashusha burudani ya kukata na shoka ndani ya ukumbi wao wa nyumbani D.D.C. kariakoo kuanzia saa tatu usiku hadi majogoo.


      Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hiyo Dot Do! alisema kwamba vijana wake wa aljazeera wamekuwa wakifanya mazoezi kwa takribani kila siku na hii ni maalum kwa wadau na mashabiki wao kupata ule muziki ulio sahihi kabisa na sio kubahatisha, kwani hiyo sio sifa ya aljazeera old & modern taarab, nashukuru kuona wiki iliyopita mashabiki walikuwa ni wengi sana kupita siku zote kwahiyo na jumamosi ya leo pia waje kwa wingi kwani kuna nyimbo kali sana ambazo zitapigwa na kamwe huwezi kuzisikia popote pale alimaliza kwa kusema mkurugenzi huyo.


     Bendi ya aljazeera imeendelea kujizolea umaarufu kutokana na utendaji wake na pia nidhamu kwa wasanii wake pia imekuwa ni kivutio kikubwa sana, aljazeera wamekuwa wakipiga katika ukumbi huo wa D.D.C. kariakoo kila siku ya jumamosi kama ilivyo leo, wapenzi tujitokeze kwa wingi leo ili kupata burudani mwanana kabisa toka kwa vijana hawa, kiingilio katika show hiyo ni shilingi elfu sita kwa wanaume na wanawake wao wanaingia bure kabisa.

03:13

JUMATATU NI ZAMU YA PRINCE AMIGO WA JAHAZI MODERN TAARAB NDANI YA KIKAANGO CHA WATANGAZAJI WA TAARAB!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


PRINCE AMIGO AKIWAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE.

       Prince amigo ndie atakuwa katikati ya watangazaji siku ya jumatatu ijayo pale atakapojibu maswali ya watangazaji wa taarab wapatao tisini ndani ya group bora la whatsap la ubuyu wa taarab kwenye kile kipengele cha kikaangoni wiki hii.


      Akithibitisha kuwepo ndani ya kikaango hicho prince amigo alisema kwamba kwanza kabisa amefurahi sana kupata bahati hiyo maana kuhojiwa na watangazaji wengi kiasi hicho tena kwa wakati mmoja ni jambo la kushukuru maana naamini mashabiki wangu watapata kujua mengi sana toka kwangu maana naamini kuwa mimi bila wao siwezi kuwa prince amigo.


     Pia nawapenda watangazaji wote waliopo humo maana nimesikia wana maswali hatariii!!, nami nimejiandaa kuwajibu wote bila kuacha hata swali moja kikubwa tuombe mwenyezimungu atufikishe siku hiyo maana jumatatu ni mbali kiasi alimaliza kwa kusema prince amigo. mtandao huu unapenda kutanguliza shukrani za dhati kwa prince amigo na wasanii wote ambao tayari wamepita katika kikaango hiki! wewe ukiwa msanii basi jiandae muda na wakati wowote unaweza kupigiwa simu ukitakiwa kuwepo katika segment hii.

02:11

HASHIM SAID:- NIMEJAALIWA MAHABA NDIO SABABU DIANA HAWEZI KUNISAHAU KATIKA MAISHA YA NDOA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


HASHIM SAID AKIWA KWENYE POZI.

         Ile segment yetu pendwa ya kikaangoni wiki hii iliendelea na tulimbambanisha hashim said au mzee wa majanga kutoka mashauzi classic, aliingia katika group saa moja na dakika kumi na maswali yakaanza moja kwa moja, mtangazaji aliepata bahati ya kuanza kuuliza swali alikuwa ni:- 


ASHA VICTORIA FM MUSOMA:- Hashim karibu sana humu jandoni kwetu, ningependa kujua historia yako kimuziki na umeshafanya kazi bendi ngapi mpaka sasa na nini sababu ya kuhama hama kwako?.


 HASHIM SAID:- Mimi nimeanza kuimba tokea mwaka 1998 na bendi yangu ya kwanza inaitwa kimara connection bendi ambayo ilikuwa inapiga miduara na mchanganyiko wa dansi, baada ya hapo nikapenda kuimba taarab na bendi yangu ya kwanza katika taarab ilikuwa ni all star's iliyokuwa chini ya sabahah muchacho na mumewe salum abdul, baadae nilijiunga na egpytion music club iliyokuwa mtaa wa swahili kariakoo, baada ya pale nilijiunga na babloom chini yake seif kisauji na nilikaa kwa miaka mitano kisha mwaka 2004 nikajiunga na east african melody ambapo nilidumu kwa miaka minne kabla kuchukuliwa na dar modern taarab, lakini baadae nilirudi tena east african melody lakini ilipoanzishwa mashauzi classic nilikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo na nilidumu kwa miaka minne nikahama na kujiunga na wakaliwao ambapo nilidumu kwa miezi tisa tu, na hapa juzi tu nikaamua kurudi nyumbani yaani mashauzi classic, kuhama hama issue inakuwa maslahi tu na wala sio kitu kingine.


MC CHINGA DODOMA FM:- Hashim kuna tetesi kuwa unataka kurejea bendi yako ya zamani mashauzi classic je kuna ukweli wowote juu ya taarifa hizi?.


 HASHIM SAID:- Mc chinga nakupata sana ni kweli nimerudi mashauzi classic na siku alhamisi tarehe 19/5/2016 pale mango garden kuna bonge la party la kunikaribisha rasmi katika ule usiku wa nyumbani ni nyumbani.


SALMA MAISHA FM DODOMA:- Hashim kwanini umeamua kurudi mashauzi na sio bendi ingine nikimaanisha east african melody au dar modern maana mwenyewe unasema huko kote ni nyumbani kwako?, na tangu uanze muziki huu ni mafanikio gani umepata?.


HASHIM SAID:- Salma au kim nainai ni kwamba mafanikio niliyopata katika muziki nashukuru sasa hivi nina kibanda changu nakaa na watoto wangu pamoja na mke wangu nimetoka katika yale maisha ya kupangapanga maana majumba siku hizi kila kukicha yanapandishwa kodi, na kurudi kwangu mashauzi ni sababu niliishi vizuri sana na wenzangu pale kwahiyo kuna vitu nilikuwa navimiss sana kiukweli, ila kwa sasa nashukuru nimerudi nyumbani sasa.


SHUFAA KAYA FM BAGAMOYO:- Katika tasnia ya taarab inasadikika kwa asilimia kubwa kwamba kumejaa rushwa ya ngono je wewe kama msanii wa taarab nchini unalizungumziaje jambo hili?.


 HASHIM SAID:- Hata mimi nimekuwa nikisikia kuwa huku kwetu rushwa ya ngono ipo ila sijarithibitisha hilo, ila kwa upande wangu nimewasaidia sana waimbaji wengi na wengine wapo mashauzi mpaka sasa mfano zuhura, rahma na aziza  hawa ndio nimewasaidia kuwepo pale mashauzi na sijawahi kuwataka rushwa ya ngono


BLANDINA TK FM TANGA:- Hashim said, mimi swali langu fupi tu ndugu yangu, ni kwanini uliondoka wakaliwa modern taradance?.


 HASHIM SAID:- Nimeondoka wakaliwao modern taradance kutokana na kuna vitu vimenifanya mimi niondoke wakaliwao kwanza ucheleweshaji wa nyimbo yangu kupelekwa redio tumeurekodi tokea mwezi wa kumi na moja mwaka jana lakini umekuja kupelekwa redio mwezi wa nne mwaka huu jambo ambalo limenirostisha mimi kama mimi kisanaa, jambo la pili niliamua tu mimi mwenyewe kuachana na wakaliwao sababu nikiangalia heshima yangu mimi pale wakaliwao sikuwa napendeza na nikagundua kuwa nilikuwa napendeza zaidi mashauzi classic na kwakuwa sikuondoka vibaya basi nimeamua kurejea nyumbani na wakaliwao sijaondoka vibaya ingawa kitendo cha kuchelesha nyimbo yangu kiliniumiza sana ila nimepotezea tu ukweli ndio huo!.


KAKA ZEMA CITIZEN NAIROBI KENYA:- Hebu weka wazi maisha yako ya ndoa ulioa ukataliki...kisha ukaoa tena ukataliki...ukaoa tena ukataliki...ukaamua kumrejea mama watoto wako yaani mzazi mwenzio, je ni wanawake wana tatizo au tatizo unalo wewe mbona kusuasua kwenye ndoa kaka?.


 HASHIM SAID:- Kaka zema ni kwamba hili ni tatizo kubwa ambalo ninalo katika maisha yangu ya mahusiano, siwezi kujua kama tatizo lipo kwa upande wangu au wanawake ninao waoa, lakini mwisho wa siku ni kwamba nimerejea katika ndoa yangu ya awali kwa mke wangu ambae ana watoto wangu, mimi na yeye tulitengana kwasababu ya maneno ya watu walikuwa wakimlisha maneno kila siku mumoe malaya, mumeo sijui hivi mumeo sijui vile lakini katika maisha yetu ya ndoa hakuwahi kunifumania hata mara moja na talaka aliidai yeye mwenyewe, baadae nikaoa mke wa pili, mke huyu alikuwa akini-cheat yeye alikuwa akifanya kazi za sanaa kwani alikuwa ni mcheza show na nilimuachia huru tu nikijua sanaa sio uhuni lakini alikuwa akitumia nafasi hiyo kuni-cheat sana sana nikaamua kumtaliki. nikapata mke wa tatu fatuma fundikila nilimpenda sana katika wanawake niliowapenda alipata bahati ya kuuteka moyo wangu fatuma fundikila na tumedumu katika ndoa miaka mitatu na sababu kubwa ya mimi na yeye kuachana ni maneno ya familia kwanini anaishi na mimi mwanaume maskini, mwanaume muimba taarab mwanaume mwenye kipato cha chini maneno yalizidi mwisho wa siku miluzi mingi humpoteza mbwa! mwisho wa siku tuliachana na nilimuacha huku nikiwa bado nampenda sana!.


TNNA EBONY FM IRINGA:- Nafahamu ulikuwa na bibie Diana kwenye mahusiano lakini sasa yamefikia mwisho lakini mbona diana anakusumbua sana kiasi cha kusema katika redio flani kwamba yupo tayari umrejee hata leo kwani nini kubwa mno ulilokuwa unamfanyia mpaka anaonekana kuumia na penzi lako mpaka anataka umrejee?.


 HASHIM SAID:- Diana ananipenda mpaka sasa hilo nalijua wazi ila tabia zake zimenishinda, sasa hivi nasikia yupo na mtu anaishi nae lakini kila siku haishi kunipigia simu na kuniambia kuwa bado ananihitaji, najua ni ngumu kunisahau yeye maana nilikuwa namfanyia vitu vingi vizuri vya mapenzi, nilikuwa namfulia, nilikuwa nampikia, nilikuwa namkata kucha akitaka kulala ni lazima nimlaze kifuani kwangu ndio apate usingizi na mambo mengi mazuri na matamu kwenye mapenzi hivyo ni ngumu sana kunisahau mtu kama mimi.


        Maswali yalikuwa mengi sana toka kwa watangazaji mbalimbali lakini siwezi kuorodhesha maswali yote hapa kutokana na nafasi na muda pia ila baadhi yao niwataje kwa majina tu ni Aisha wa barmed's televisheni mwanza, aisha saggaf wa k.b.c. nairobi, nadya wa bomba fm znz, malick wa hits fm znz, koleta wa redio free mwanza, edna wa afm dodoma, kitoroli wa mlimani redio dar, mamaa madikodiko wa pilipili fm mombasa,  hamida malick wa coconut fm znz, mamaa nyeupe wa upland's redio njombe, asha simba wa kilosa fm morogoro, fortina wa cg fm tabora na wengineo wengi. tukutane tena wiki ijayo...Ahsanteni sana!.

Jumatano, 18 Mei 2016

12:47

ALJAZEERA OLD & MODERN TAARAB YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA KARIAKOO, ILALA NA MAGOMENI KWA BURUDANI ZA UHAKIKA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.

WAIMBAJI WA ALJAZEERA OLD & MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI.

 

          Wale wajanja wa taarab asilia jijini dar es salaam kwa sasa aljazeera old & modern taarab wameendelea kuwa gumzo hapa jijini kwa burudani zao nzuri kwa mashabiki na wapenzi ambao wamekuwa wakimiminika kwa wingi karibia kila jumamosi pale katika ukumbi wao wa nyumbani wa D.D.C. kariakoo.

 

     Wakizungumza kwa nyakati tofauti mashabiki wa bendi hiyo waliisifia sana bendi hiyo na kukili wazi kwamba imekuja kuleta ushindani mkubwa katika aina hii ya taarab asilia hapa jijini dar, mama munirah mkazi wa ilala alisema kuwa unajua hapo zamani tulikuwa tumezoea kupata raha hizi kutoka kwa bendi moja tu "akaitaja jina" lakini kwa sasa aljazeera wamenifanya kila jumamosi kukimiss kitanda changu na kuja hapa D.D.C. kariakoo kupata raha, maana nyimbo wanazozicheza huwa sizisikii kule kwingine, kusema ukweli nawapongeza sana.

 

    Nae mc michambo mkazi wa magomeni mikumi yeye alisema kuwa, hapo mwanzoni sikuwa naipenda kabisa bendi hii, tena nilikuwa sijishughulishi nao kabisa!, lakini siku moja nilipata kazi ya u-mc maeneo haya ya kariakoo na ilikuwa jumamosi, basi nilipomaliza kazi nikaona nipitie hapa D.D.C. ili nipoteze muda kidogo kabla ya kuelekea nyumbani, lakini burudani niliyoipata siku hiyo ni balaah! sikutegemea kama hawa aljazeera wanaweza kupiga muziki kama huu, nimewapenda sana mpaka sasa sijawahi kukosa show yoyote ya hawa jamaa nawapongeza sana na nawaomba wasilewe sifa ila wakaze uzi maana ushindani ni mkubwa sana kwa sasa alimaliza kwa kusema shabiki huyo.

 

       Bendi hii ya aljazeera old & modern taarab hufanya burudani yake katika ukumbi huo wa D.D.C. kariakoo kila siku ya jumamosi kwa kiingilio cha shilingi 6,000/- za kitanzania kwa mwanaume na wanawake bure kabisa!.

11:49

SUPERSHINE MODERN TAARAB KUPAGAWISHA WAKAZI WA MBAGALA JUMAMOSI NA JUMAPILI HII.

NA KAIS MUSSA KAIS.


WAIMBAJI WA SUPERSHINE MODERN TAARAB WAKIWA STEJINI.

            Bendi yako ya supershine modern taarab wana rusharoho usitoe roho chini ya muimbaji wao kiongozi Queen salma jumamosi na jumapili ya wiki hii wanatarajia kuwapagawisha wakazi wa mbagala na vitongoji vyake katika ukumbi wa dragon kongowe na ngeme maeneo ya chamazi.


       Akizungumza na mtandao huu mkurugenzi wa bendi hii Dr No! amesema baada ya kukosekana kwa takribani wiki tatu sasa supershine tunarudi tena maeneo yetu ya kujidai kwa ajili yao mashabiki zetu, hivyo tunawaomba kujitokeza kwa wingi ili wapate raha walizozikosa kwa muda na pia tutapiga nyimbo zetu mpya kabisa ambazo hazijawahi kupigwa popote pale.


     Supershine modern taarab ni bendi kongwe ambayo imetoa wasanii wengi wanaoendelea kutamba sehemu mbalimbali hapa nchini wakiwemo ally j, hashim said mzee wa majanga, mussa machine wa jahazi modern taarab, ramla seif wa melody na wengineo wengi sana!.

10:59

KHADIJA YUSUPH:- SINA MPANGO WA KUIHAMA JAHAZI MODERN TAARAB, MTAENDELEA KUZUSHA SANA TU!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


KHADIJA YUSUPH-SAUTI YA CHIRIKU AKIWA KWENYE POZI.

            Muimbaji khadija yusuph au ukipenda muite sauti ya chiriku ameuambia mtandao huu makini ubuyu wa taarab kwa njia ya simu kwamba hayupo tayari kuihama bendi yake ya jahazi modern taarab kama ambavyo imekuwa ikivumishwa na wadau pamoja na baadhi ya vyombo vya habari.


         Khadija aliyasema hayo baada kusikia akizungumziwa sana juu ya yeye kuiacha bendi yake ya jahazi na kujiunga na bendi moja nguli ya taarab hapa nchini, napenda niwaambie wadau na wapenzi wangu kuwa mimi khadija yusuph au sauti ya chiriku sina muda wala mpango wa kuiacha bendi yangu kama inavyovumishwa!, mimi nashangaa sana watu wamekuwa wakinifuatilia sana sijui wanataka nini toka kwangu!, taarifa hizi zimekuwa zikinishushia heshima yangu sana na kuwafanya mashabiki wangu kupunguza imani na mimi.


     Mtandao huu ulitaka kujua ni kwanini khadija yusuph hakusafiri na bendi ya jahazi modern taarab katika ile safari yao ya mikoa ya iringa, mbeya na songea ambayo jahazi wamerudi jana dar es salaam? na yeye alijibu kuwa sikusafiri na bendi sababu nilikuwa naumwa homa sana, na hao wanaovumisha kwamba nilikuwa na mipango ya kujiunga na bendi flani ndio maana nikabaki na si kweli kwamba nilikuwa naumwa nawaambia wataishia kuvumisha mambo yasiyo na uhakika mpaka mwisho wa uhai wao!, najua nia yao ni kunigombanisha na kaka yangu lakini nawaambia wameshindwa na wataendelea kushindwa milele, mimi nipo jahazi modern taarab na nitaendelea kuwepo hapo daima alimaliza kwa kusema khadija yusuph.


      Mtandao huu umerekodi maongezi ya khadija yusuph wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ili iwe kama ushahidi siku ya siku!, na hii ni kwa nia njema tu maana huo ndio utaratibu wa mtandao huu wa ubuyu wa taarab.tunapenda kumpa pole khadija yusuph kwa tetesi hizi ambazo kwa namna moja ama ingine zitakuwa zimemuathiri kisaikorojia.

Jumatatu, 16 Mei 2016

16:29

KIVURANDE JUNIOR MFALME WA NGOMA YA KIBAO KATA ASIE NA MPINZANI TANZANIA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


KIVURANDE JUNIOR AKIWA KWENYE POZI.

         Kwa sasa unapozungumzia ngoma ya kibao kata ambayo asili yake ni mkoani tanga, basi ni lazima utamtaja kijana anaesumbua vichwa vya watu wazima kwa masongi yake ambae ni kivurande junior.


        Kijana huyu ambae pia ni mwenyeji wa mkoa wa tanga alianza kuimba taarab akiwa kwao tanga mjini, alipoona amepevuka kiasi alipanda basi na kuja dar es salaam kutafuta maisha na kuendeleza fani yake zaidi, bendi yake ya kwanza kuimbia hapa dar ni king's modern taarab iliyokuwa ikiongozwa na hamisi majaliwa sambamba nae director kijoka. pale kijana huyu alifanikiwa kurekodi wimbo wake wa kwanza kabisa ambao ulikuwa unakwenda kwa jina la "mtoto dot.com".


      Baadae aliihama bendi hiyo na kujiunga na bendi ya t motto modern taarab chini yake mkurugenzi Amin salmin, pale alikutana na wasanii nguli kama jokha kassim, nyawana fundikila, aisha masanja, nassor hussein "chollo" thania msomali, shinuna kassim na wengineo wengi, lakini safari hii hakufanikiwa kurekodi akiwa na t motto modern taarab, bendi illipoanza kuyumba alijisogeza east african melody ambapo alifanya sana mazoezi na bendi hiyo na kushiriki show mbalimbali za bendi.


     Kutokana na uimbaji wake mzuri, siku moja iliandaliwa show ya pamoja kati ya kibao kata na east african melody, aliponyanyuka kivurande kuimba ndipo viongozi wa kibao kata wakamuona na kuanza taratibu za kumnyakuwa moja kwa moja!, na kweli walifanikiwa kumchukuwa na sasa yeye ndio reader pale mbele katika uimbaji, unapomkuta stejini akifanya yake ndani ya billicanas club kila siku ya jumatano unaweza kumtunza pesa zote za mfukoni kwako ukakosa hata nauli ya kurudia nyumbani, wadau na wapenzi wake kwa sasa wamempachika jina wanamuita "mfalme wa kibao kata" jina ambalo kivurande amesema kuwa amelipokea kwa maana sio baya na mashabiki wake ndio wanaomkubali kwa kazi zake nzuri, mpenzi msomaji wa blog hii bora unaombwa kwenda pale billicanas club kila jumatano umuone kijana huyu anavyoisimamisha dar kwa kipaji chake alichojaaliwa na mungu.

15:10

BAADA YA KUONDOKA DAR MODERN HATIMAE KISOLO MWANA MALUI AJIUNGA NA T.O.T. MODERN TAARAB.

NA KAIS MUSSA KAIS.


KISOLO MWANA MALUI AKIWAJIBIKA.

        Ramadhan kisolo au ukipenda muite kisolo mwana malui, baada ya kuondoka katika bendi ya dar es salaam modern taarab mwezi uliopita hatimae amejiunga rasmi katika bendi ya tot modern taarab.


       Akizungumza na mtandao huu makini director wa tot modern taarab mohamedy mbange alisema kwamba ni kweli kisolo ameanza kazi rasmi na bendi yetu, na mimi kama kiongozi nimempitisha moja kwa moja hakukuwa na interview sababu kisolo kwa sasa ni msanii mkubwa sana ukizungumzia wapiga magita wanaofanya vizuri kwa sasa katika muziki huu wa taarab nchini basi jina la kisolo mwana malui ni lazima ulitaje, tutashirikiana nae bega kwa bega na kwa sasa kazi kubwa aliyonayo ni kuhakikisha anazijua nyimbo zetu vyema kabisa! na hilo halina shida kwa kisolo kwani ni mzoefu sana tu!.


       Nae kisolo mwana malui akizungumza kwa upande wake alisema amefurahi sana kupata nafasi ya kujiunga na tot kwani hii bendi ni taasisi rasmi ambayo inalipa mishahara wafanyakazi wake pamoja na huduma zingine muhimu, nilipoacha kazi pale dar modern kuna baadhi ya watu walihisi nimepotea lakini mimi napenda niwaambie kuwa hapa nilipo sasa ni sehemu sahihi kwa watu sahihi ambao wanapiga muziki sahihi, jambo kubwa napenda niwadhihirishie viongozi wangu hapa tot kwamba nitashirikiana nao bega kwa bega na kamwe sitowaangusha, vile vile wasanii wenzangu tutashirikiana katika kuipeleka mbele zaidi tot mpya na ya kisasa alimaliza kwa kusema.

Jumamosi, 14 Mei 2016

01:15

OGOPA KOPA CLASSIC NA SALAM TMK KUZINDUA BENDI ZAO NDANI YA TRAVETINE MAGOMENI JUMAMOSI YA LEO!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


             Baada ya bendi ya ogopa kopa kuzinduliwa kwa mafanikio makubwa ndani ya wilaya ya temeke wiki iliyopita, leo inatarajia kuzinduliwa katika wilaya ya kinondoni katika ukumbi wa travetine magomeni wakiwa sambamba na vijana wa salam tmk hawa ni vijana wengine wa mkubwa fellah ukiwaondoa yamoto bendi.


        Akizungumza na mtandao huu makini mkurugenzi wa bendi ya ogopa kopa malkia khadija omary kopa amesema kwamba leo wakazi wa kinondoni watapata burudani ya nguvu toka kwa vijana wake kwani wamejipanga kuwaburudisha kwa nyimbo mbalimbali mpya na hata zile za zamani zilizowahi kutamba.Ndugu mwandishi unajua wapenzi wetu wamekuwa na hamu kubwa ya kuona ogopa kopa wanakuwa vipi pindi wanapokuwa stejini hivyo kwa wakazi wa kinondoni leo ndio wakati wao muafaka nawaomba waje kwa wingi kushuhudia mambo mazuri alimaliza kwa kusema.


        Katika onesho hilo la leo hii jumamosi kiingilio cha mlangoni itakuwa ni shilingi 10,000/= tu za kitanzania na utapata burudani zote toka kwa ogopa kopa na vijana wa salam tmk, kumbuka show inatarajia kuanza saa tatu kamili za usiku hadi majogoo, show hii itasindikizwa na yamoto bendi chini yake dogo asley.

Alhamisi, 12 Mei 2016

17:14

NANI MKALI KIMBE G.OLD & MODERN TAARAB NA KONGAMOYO BENDI...NI NDANI YA TANGA TAREHE 27/5/2016.

NA KAIS MUSSA KAIS.


           Ni onyesho ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na wakazi wa tanga na vitongoji vyake pale wababe wawili kimbe G.old & modern taarab ya tanga na kongamoyo bendi toka dar es salaam zitakapo onyeshana kazi katika mpambano uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa splended uliopo tanga


        Akizungumza na mtandao huu muimbaji mkongwe wa kimbe G. na tanzania kwa ujumla Bi mwanahela alisema kwamba sisi tumejiandaa vya kutosha na tunawasubiri hao wapinzani wetu waje hapa tanga hiyo tarehe 27/5/2016 ijumaa ili tuwaonyeshe taarab haswa inavyopigwa na kuchezwa!, nimeshaziona bendi nyingi za dar zinapokuwa stejini hivyo nina uzoefu nazo najua udhaifu wao upo wapi, naamini siku hiyo patakuwa hapatoshi.


         Nae director wa bendi ya kongamoyo mohamedy mbange yeye kwa upande wake alisema anaheshimu sana uwezo wa kimbe G. haswa muimbaji wao Bi mwanahela lakini na sisi hatuendi kitoto kwani silaha za mahangamizi tumeshazinoa na tunasubiri tu siku ifike ili tukawafundishe taarab, waimbaji wangu Asya mariam, mwasiti suleiman, fatma kidude, shinuna khasim na mossi watawaduwaza hao wanaojiita wakongwe!, hii ni kongamoyo huwa hatubahatishi.


         Katika onyesho hilo kiingilio cha mlangoni itakuwa ni shilingi 5,000/= tu za kitanzania na show itaanza saa mbili kamili za usiku mpaka majogoo, kumbuka itakuwa ni katika ukumbi wa splended mkoani tanga nyote mnakaribishwa.

16:33

ASYA MARIAM "UTAMU" AJIFUNGUA SALAMA MTOTO WA KIUME HUKO TANGA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


              Muimbaji mwenye sauti tamu na ya kuvutia kuliko waimbaji wote chipukizi wa kizazi hiki cha Dot.com Asya mariam au ukipenda muite Asya utamu amejifungua salama mtoto wa kiume huko tanga.


ASYA UTAMU AKIWA NA MTOTO WAKE.

     Akizungumza kwa niaba ya mzazi huyo, mkurugenzi wa bendi ya kongamoyo Iqbar alisema kwamba Asya amejifungua salama mtoto wa kiume na khali yake pamoja na mtoto inaendelea vyema kabisa, unajua siku za kujifungua zilipokuwa zinakaribia nikaona nimruhusu msanii wangu aende kwao ambapo ataweza kupata huduma nzuri zaidi kabla yakujifunga na baada ya kujifungua.


MTOTO WA ASYA UTAMU AKIWA AMEPUMZIKA.

          Mtandao huu ulipomtafuta Asya utamu kwa simu hakuweza kupatikana kutokana na mambo kuingilia ikiwemo tatizo la network huko alipo, dawati letu la habari tunapenda kumpongeza Asya mariam kwa kujifungua salama na mwenyezimungu amkuze vyema mtoto.

16:00

KIBIBI SLIM:- WASANII WA TAARAB ACHENI CHUKI, UNAFIKI, MAJUNGU NA USHIRIKINA MAANA MMEZOEA!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


KIBIBI SLIM MUIMBAJI WA ZAMANI WA DAR MODERN.

            Muimbaji wa zamani wa bendi ya dar es salaam modern taarab kibibi slim amewaasa wasanii wa muziki huu wa taarab nchini kuacha chuki, unafiki, majungu na ushirikina ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo.


          Aliyasema hayo jana katika ukumbi wa dar live mbagala jijini dar alipokuja kupata burudani ya bendi ya east african melody ambao hupiga hapo kila jumatano, akizungumza kwa kujiamini kibibi slim alisema kuwa mimi nimeyaona sana haya wakati nipo dar modern taarab hivyo hakuna wakuniongopea juu ya hili.


       Unaweza kujishangaa umetoka nyumbani vizuri na sauti yako ipo sawa bin sawia lakini unapokanyaga stejini tu na kupewa kipaza sauti basi sauti haitoki kabisaaaa!, mimi mwenyewe ni muhanga wa jambo hilo kwani imenitokea mara kibao tu!, kama tukiendelea na tabia hii basi muziki huu hautoweza kufanya vizuri daima milele, hebu tubadilike jamani sio vyema na mungu hapendi.


        Muimbaji huyo ambae amesema anataka kurudi kwa kasi katika muziki huu wa taarab nchini alishawahi kurekodi nyimbo kadhaa akiwa na dar modern taarab na baadae alipumzika kwa muda mrefu sana akifanya biashara zake za kusafiri nje ya nchi ya tanzania, hebu tuvute subira ili tuone yupo vizuri, amejipanga? maana gemu imebadilika sana siku hizi ushindani umekuwa mkubwa sana baina ya bendi na bendi.

Jumatano, 11 Mei 2016

18:09

BAADA YA MATATIZO KUPITA, SALHA ABDALLAH AACHIA WIMBO MPYA KABISA USEMAO JIJI LA DAR!.

NA KAIS MUSSA KAIS.


MUIMBAJI SALHA ABDALLAH.

            Salha abdallah muimbaji mwenye sauti ya kuvutia ameachia wimbo mpya uitwao "jiji la dar" wenye mahadhi ya mduara siku chache tu baada ya kupita matatizo yake na mumewe hammer Q.


         Akizungumza na mtandao huu ofisini kwetu, salha alisema kuwa, nimekaa muda mrefu sana pasipo kuwa na wimbo mpya hivyo naamini wadau na mashabiki zangu walinimiss mno, nimeamua kuja kwa style ya mduara ili kuwadhihirishia kuwa mimi ni mwanamuziki naweza kuimba aina yoyote ile ya muziki. kwa sasa nipo katika project nzito sana ya kuandaa albam yangu binafsi ambayo itasheheni nyimbo kali na zenye ujumbe mzito.


         Ijapokuwa nipo katika bendi ya wakaliwao modern taradance lakini nimeamua kuandaa albam yangu binafsi ili kujiongezea kipato zaidi, mimi katika albam mpya ya wakaliwao modern taradance sina wimbo mpya mule hivyo nimeamua kurekodi albam yangu binafsi mwenyewe. Ila naomba nisieleweke vibaya! mimi bado ni muimbaji wa wakaliwao mpaka sasa alimaliza kwa kusema salha abdallah.

Jumanne, 10 Mei 2016

17:33

HASHIM SAID "MZEE WA MAJANGA" KIKAANGONI MBELE YA WATANGAZAJI JUMATATU IJAYO.

NA KAIS MUSSA KAIS.


HASHIM SAID "MZEE WA MAJANGA" AKIPOZI KWA PICHA.

          Group la watangazaji wa muziki wa taarab kupitia redio na televisheni jumatatu ya wiki ijayo watapata nafasi ya kufanya mahojiano na Hashim said au ukipenda muite 'mzee wa majanga' katika kile kipengele kinacho endelea kujizolea umaarufu cha "kikaangoni wiki hii".


        Hashim said ambae wiki iliyopita alitangaza rasmi kuipa kisogo bendi ya wakaliwao modern taradance atawekwa mtu kati na watangazaji zaidi ya tisini kwa maswali, watangazaji hawa wanatoka mikoa tofauti ya tanzania nikimaanisha unguja, pemba na mikoa ya tanzania bara, pia kuna watangazaji tokea nchini kenya ambao nao hupatikana humo. anachotakiwa kufanya hashim said ni kujibu maswali yote toka kwa watangazaji hao na muda ukifika wa yeye kuondolewa katika group hilo basi admin hufanya hivyo na kuwaacha watangazaji wakiendelea kupiga stori zao kama kawaida.


          Kubwa wapenzi wa blog hii ya ubuyu wa taarab kuweni tayari kusoma kile ambacho hashim said atakuwa ameulizwa na kuweza kujibu, hii ndio blog bora ya taarab kwa sasa hapa nchini tuendelee kuwa pamoja kwa maoni na ushauri wasomaji wangu.

16:35

PRINCE BLACK KOPA ALUMBANA NA MWAJUMA WA RAS FM MBELE YA WATANGAZAJI 98 NDANI YA KIKAANGONI.

NA KAIS MUSSA KAIS.

PRINCE BLACK KOPA.

             Kile kipengele chetu cha "kikaangoni wiki hii" ambacho hurushwa kila jumatatu saa moja kamili ndani ya group la watangazaji wa taarab liitwalo "ubuyu wa taarab" kiliendelea tena wiki hii na mgeni alikuwa prince black kopa tokea pale ogopa kopa classic bendi na kama kawaida baada ya kusalimia maswali yakaanza kama ilivyo ada.

 

DIVA WA HITS FM ZNZ:- Mambo vipi black kopa, nataka kufahamu toka kwako hivi ni kweli yule wifi uliekuwa nae na mwisho wa siku kupigana chini eti alisutwa na mama mkwe I mean khadija omary kopa? au maneno ya watu tu? lakini pia kuna siku ulifanyiwa interview katika redio flani ukaulizwa kuhusu yeye ukamkana kuwa humfahamu licha ya kumpandisha juu ya jukwaa kwenye show flani hivi, naomba majibu.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Sikiliza Diva, huyu mwanamke mimi sikuwa nae na mahusiano, mambo hayo ya kuposti kuhusu mimi anajua mwenyewe alivyofanya, mimi najua matatizo ya kuwa na mahusiano na mtangazaji na kuhusu hiyo kusutwa na mama mkwe hakusutwa wala nini, na kupanda juu ya jukwaa ni kawaida sababu ile show pia nae alishiriki kuandaa kule dodoma kwahiyo alikuwa anapanda juu kuimbaimba kuchezacheza lakini hakuna chochote mimi sina mahusiano na mtangazaji jibu ni hilo.

 

AISHA WA BARMED'S TELEVISHENI MWANZA:- Ningependa kujua ni skendo gani ambayo uliwahi kukutana nayo tangu umeingia katika tasnia hii ambayo ilikukwaza sana na je ilikuwa ya ukweli?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Mimi sipendi sana maskendo na wala skendo sina, zaidi nina skendo moja ambayo ndio hiyo imetokezea juzi ya kutembea na mtangazaji na iyo skendo sio ya ukweli, jibu ni hilo.

 

FORTINA WA CG FM TABORA:- Juzi mmezindua bendi sambamba na albam mpya, je kuna project yoyote mnategemea kuiachia hivi karibuni?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Sasa hivi kuna project ya nyimbo zetu hizo mpya kama nimempata mwenye maslahi ambayo niliimba pale dar live na kuna wimbo wa mama yangu khadija kopa ambao unaitwa hakuna mwenye mji wake, kuna wimbo wa shadya shombeshombe, kuna wimbo wa bi eshe mohamedy kuna wimbo wa mwamvita shaibu kuna mambo mengi tumeandaa huko katika siku zijazo na muda si mrefu mtaona wenyewe kwasababu sisi ogopa kopa huwa hatupendi kuongea hapa ni vitendo tu.

 

SHARIFA WA KAYA FM BAGAMOYO:- Ni kwanini uliamua kujikita kwenye muziki wa taarab kwa kipindi hiki ulikuwa unapenda tokea utoto au ulipoona mama anaimba na wewe ukataka kuimba?.

 

PRINCE BLACK KOPA:- Hapana mimi nilikuwa ni muimbaji tokea zamani sababu kabla ya kuimba taarab, nimeimba sana bongo fleva wakati nipo zanzibar, hivyo muziki upo kwenye damu kuanzia kizazi na kizazi.

 

       Wakati mahojiano yakiendelea Mwajuma wa ras fm dodoma aliingilia kati na kutuma voice note kujaribu nae kuweka wazi na kutolea ufafanuzi kwa yale anayo yazungumza black kopa na watangazaji wenzie yaani mwajuma, alianza kwa kusema kuwa yeye hana shida ya kumnadi mwanaume eti aonekane ametoka na superstar, au aonekane ametoka na mtoto wa flani nakumbuka huyu huyu black kopa ambae anasema eti mimi hajawahi kuwa na mahusiano na mimi kashfa kibao, kunitolea dharau kibao na kunidhalilisha pia mbele za watu kwamba hajawahi kuwa na mahusiano na mimi, siku alipokuwa akinitongoza kuna swali nilimuuliza wewe unanifuata mimi, lukini kumbuka kuwa mimi ni mtu ambae hali yangu ni ya duni sana hata wazazi wangu pia ni maskini hakuna hata anaewajua kwanza wazazi wangu wanaishi kijijini, mimi mwenyewe maisha yangu ndio kama haya unayoyaona ndio kwanza naanza kutafuta maisha, nakumbuka nilimuuliza huwezi kuhisi litakuja tokea tatizo hapo mbeleni itaonekana kama natoka na wewe ili nitafute kiki?.

 

        Lakini black kopa hakujibu swali hili la mwajuma zaidi ya kulalamika kwa admin kwamba asimamie utaratibu kwani anaetakiwa kurekodi voice note ndani ya kipengele cha kikaangoni ni yeye tu black kopa na wala si mtangazaji yeyote na ukweli upo hivyo hivyo kama alisema black kopa.

 

      Mwajuma aliendelea kueleza kuwa naumizwa sana na hayo unayo endelea kuyazungumza black, ni kweli mimi na wewe hatupo pamoja kimapenzi kwa sasa lakini sio kukataa kwamba hukuwahi kuwa nami kimapenzi au unataka niziposti humu kwa watangazaji sms zako za mapenzi ulizokuwa ukinitumia wazione? sikung'ang'anii no! ila naumizwa na kashfa zinazoendelea juu yangu, hizi sms niliziifadhi kama ushahidi kama lolote baya litatokea juu yangu, unachofanya black kopa ni kitu cha kitoto, binadamu sisi black kopa kuna kukoseana na mimi sijawahi kukukosea hata mara moja hujawahi kunifuma nipo na mwanaume wala kuifuma sms ambayo mimi nimetumiwa na mwanaume chochote kile hujawahi kufuma toka kwangu, kuachana ni kitu cha kawaida, kwani ukisema kuwa mimi na wewe tulikuwa na mahusiano tumeachana utakuwa umekufa?.

 

    Kikaango kilikuwa kimepamba moto na maswali yalikuwa yakiendelea toka kwa watangazaji wengine na black kopa alijibu kwa ufasaha mkubwa, kuhusu issue ya mwajuma black kopa alishikilia msimamo wake kwamba sio mpenzi wake na hakuwahi kuwa nae kimapenzi, habari ndio hiyo...kwaleo naona niishie hapo ila wiki ijayo kikaangoni tutakuwa na Hashim said mzee wa majanga, mwanamuziki ambae ameondoka pale wakaliwao modern taradance.

14:34

TAZAMA PICHA "12" ZA UZINDUZI WA OGOPA KOPA CLASSIC BENDI ULIOFANYIKA DAR LIVE MBAGALA.

NA KAIS MUSSA KAIS.


            Siku ya jumamosi tarehe 7/5/2016 ni siku ambayo malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa hatoisahau katika maisha yake ya muziki nchini, kwani kwa mara ya kwanza alifanikiwa kuzindua bendi yake mwenyewe ya ogopa kopa classic kwa kishindo kikubwa ambacho hakijapata kutokea ndani ya ukumbi wa dar live mbagala jijini dar es salaam, zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopatikana katika onesho hilo:- 

WAIMBAJI WA OGOPA KOPA CLASSIC  WAKISEREBUKA KWA RAHA ZAO.

OMARY ZUNGU AKIPAPASA KINANDA HUKU KAPTEN TEMBA AKITAZAMA.
PRINCE BLACK KOPA AKICHEZA SAMBAMBA NA KHADIJA OMARY KOPA.

YOUNG HASSAN ALLY AKIWASHIKA MIKONO MASHABIKI WAKE.

KAMONGO MR BEAN AKIPAPASA KINANDA KWENYE UZINDUZI HUO.

MALKIA KHADIJA KOPA AKITOA NASAHA CHACHE PAMOJA NA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI.


PRINCE BLACK KOPA AKIWA NA MAMA YAKE KHADIJA OMARY KOPA.

YOUNG HASSAN ALLY AKIIMBA STEJINI.

HAWA WALIKUWA KAMA WALINZI WA MTOTO WA MALKIA YAANI PRINCE BLACK KOPA.

SHAMPENI IKIFUNGULIWA KWA SHANGWE NA FURAHA NA TEAM OGOPA KOPA.

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AKIONGOZA WAIMBAJI WAKE KUCHEZA KWA FURAHA.

HUU NI UMATI WA MASHABIKI ULIOJITOKEZA KATIKA UZINDUZI HUO DAR LIVE.